Top Ten makabila yenye wazungumzaji wengi Tanzania

Wewe ni muongo kabisa Kwa hizo takwimu inaonekana wewe huijui Tanzania na makabila yake vizuri. Umeandika pasipo utafiti wowote ule
Huu ni utafiti(usiokua rasmi) juu ya uwingi wa wazungumzaji wa makabila yaani wale ambao kiasili ni wenyeji wa kabila husika pamoja na wale ambao wamejifunza makabila husika kutokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimaisha.

1. WASUKUMA
-Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 10. Ni kabila pekee linalopatikana zaidi ya mikoa 6. Wasukuma (ukijumlisha na matawi yake kama Wanyamwezi, Waikizu n.k) wanapatikana mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Tabora na Kigoma pia.

2. WAGOGO
-Wanapatikana kwa wingi mkoani Dodoma. Pia wanapatikana Morogoro/Gairo(huitwa pia Wakaguru). Mkoani Singida wanapatikana wilayani Manyoni (huitwa Wagogo wa Manyoni). Mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa pia wanapatikana kwa wingi.

3. WANGONI
Ukijumlisha pamoja na Wandendeule na Wamatengo ambao lughazao huendana sana, basi Wangoni wanafanya kuwa kabila la tatu kwa uwingi Tanzania. Wanapatikana Mkoani Ruvuma.

4. WAMASAI
Hawa wanapatikana Mkoani Arusha pamoja na baadhi ya wilaya za mkoa wa Manyara kama Simanjiro na Kiteto.

5. WARANGI
-Ukiwajumlisha pamoja na matawi yake kama Waburunge na Wanguu hawa nao wanapaswa kuingia kwenye top ten.Wanapatikana kwa wingi wilaya ya Kondoa na Chemba. Pia wanapatikana maeneo ya Mpakani mwa mkoa wa Manyara na Dodoma.

List Itaendelea...

NB: NAJUA UTASHANGAA KUTOYAONA MAKABILA YA WANYAKYUSA, WAHAYA NA WACHAGA HAPO JUU, UKWELI NI KUWA KWA KIPIMO CHA UWINGI WANAPWAYA SANA ILA WAMEFANIKIWA KWENYE UMAARUFU NA ELIMU TU.

Karibuni kwa mjadala
 
Uzi wa kikabila huu
Ujinga mtupu watu wataanza kujitaja kwa makabila yao hapa, tutajadili ujinga usiokuwa na tija wala faida kwa taifa
 
Hiki hapa kiikizu.
Mwakola zesoni bamule alafu mwingine anaweza kujibu hivi Toleho mwana weto na nangweno nele marambela abhikizo bhu twimenye kwi kikundi cheto!

Wewe kama ni Msukuma au Mnyamwezi nini hutaelewa hapo?

Waikizu hawana uhusiano na wasukuma hicho ulichokiandika bora ungeongelea ubantu.

Waikizu labda ungeniambia ni tawi la wakurya au wazanaki.
 
5. WARANGI
-Ukiwajumlisha pamoja na matawi yake kama Waburunge na Wanguu hawa nao wanapaswa kuingia kwenye top ten.Wanapatikana kwa wingi wilaya ya Kondoa na Chemba. Pia wanapatikana maeneo ya Mpakani mwa mkoa wa Manyara na Dodoma.
Huu sasa ni upotoshaji wa Makusudi. Eti Wanguu na Warangi wapo kundi moja. Kwanza hata maeneo wanaoyoishi hawapakani. Wanguu wapo karibu zaidi na WAZIGUA wa Handeni na wote walikuwa Wilaya moja kabla Kilindi haijapata Wilaya. Wanguu wapo Kilindi wajameni, ndiyo asili yao huko. Pia Waburunge moja ya jamii Kikuishi hapa Tanzania. Hawa walimeguka kutoka kwa Wairaq miaka hiyo ya maisha ubabe.
 
Kwa hiyo wanyaturu walikuwa hawaolewi na makabila mengine ?
Kwa miaka hiyo hapa kwetu kuna kabila zilikuwa haziolewi na nyingine. Mfanl nikueleze kuna kabila nyingine zilikuwa zinasemwa na zingine kuwa wao ni chakula cha mkuki. Hapa kuna kuoleana? ULIZIA JUU YA KUOANA KATI YA MAKABILA ILIKUWAJE. LABDA KAMA UMEZALIWA MJINI HUNA WAZEE WENYE MIAKA 80 MPAKA 90 WATAKUSIMULIA. Ukikuta ameolewa atakuwz ni mateka wa vita vya kikabila. Kote huko ulaya kuna kabila mbalimbali lakini hawatuelezi. Ila tu wengine wamepoteza lugha zao kama watotl wa mijin hapa kwetu wanavyoendelea kuzipoteza kwa kiswahili kama ilivyokuwa kwa kiingereza, kitaliano,kigiriki,nk.
 
Acha uzwazwa,Rais wetu ana uwezo wa kuongea lugha mbalimbali kubwa na ndogo hapa nchini na anaongea popote pale anapokutana na watu wa kabila husika,hivyo bado ni mtu ambaye anaendelea kuunganisha makabila tofauti tofauti.
Lugha kubwa anazoweza kuongea rais wenu ni zipi ?

It takes one zwazwa to identify another zwazwa
 
1. WASUKUMA
-Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 10. Ni kabila pekee linalopatikana zaidi ya mikoa 6. Wasukuma (ukijumlisha na matawi yake kama Wanyamwezi, Waikizu n.k) wanapatikana mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Tabora na Kigoma pia.

Hapo kwa wasukuma matawi yake kuwa ni waikizu umekosea....nadhani ulitaka kumaanisha wanyantuzu pia wasukuma hupatikana mkoa wa Mara maeneo ya Bunda na Musoma.

Ila kuna wajita pia wana waongeaji wengi mfano wajita wapo musoma na Bunda taktibani laki 8,, mfano wakerewe, wakara, wazinza, wasweta,huongea kijita.
 
Wala sio ndoto.
Unaweza kustaajabu tukawa hata tunaikaribia robo.
.
Morogoro tumejaa kila sehemu, Dodoma, Singida soon tunaiteka, Katavi ni yetu, Rukwa hata hatuhitaji mjadala, Mbeya hadi wanalia maana ni new territory!
.
Kila sehemu tulipo tunateka vijiji vinakuwa vyetu, nitakupa mfano hai kijiji cha Kitila Mkumbo ambako ni sehemu asili ya wanyiramba ukienda unawatafuta. Ni ulimhola bhabha, wamisha mhola, eng'washi n.k
Usiumie ndiyo hali halisi
Nendeni na wakati, mfanye kazi kwa tija, msomeshe watoto wenu, mzae kwa mpangilio, muwe na familia Bora zenye maisha mazuri
Mambo ya kufunga ming'ombe mingi Huko maporini, kuzaa mitoto msiyoweza hata kuipeleka shule, kuhama hama hovyo hayatawasaidia chochote, mtabaki kuishi maisha ya dhiki huku watoto wenu wasiojua kusoma wakiendekea kuwa mabeki tatu mjini,
Mnajisifu eti mpo wengi, utafikiri Kuna gawio mnalopata
 
Huu ni utafiti(usiokua rasmi) juu ya uwingi wa wazungumzaji wa makabila yaani wale ambao kiasili ni wenyeji wa kabila husika pamoja na wale ambao wamejifunza makabila husika kutokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimaisha.

1. WASUKUMA
-Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 10. Ni kabila pekee linalopatikana zaidi ya mikoa 6. Wasukuma (ukijumlisha na matawi yake kama Wanyamwezi, Waikizu n.k) wanapatikana mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Tabora na Kigoma pia.

2. WAGOGO
-Wanapatikana kwa wingi mkoani Dodoma. Pia wanapatikana Morogoro/Gairo(huitwa pia Wakaguru). Mkoani Singida wanapatikana wilayani Manyoni (huitwa Wagogo wa Manyoni). Mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa pia wanapatikana kwa wingi.

3. WANGONI
Ukijumlisha pamoja na Wandendeule na Wamatengo ambao lughazao huendana sana, basi Wangoni wanafanya kuwa kabila la tatu kwa uwingi Tanzania. Wanapatikana Mkoani Ruvuma.

4. WAMASAI
Hawa wanapatikana Mkoani Arusha pamoja na baadhi ya wilaya za mkoa wa Manyara kama Simanjiro na Kiteto.

5. WARANGI
-Ukiwajumlisha pamoja na matawi yake kama Waburunge na Wanguu hawa nao wanapaswa kuingia kwenye top ten.Wanapatikana kwa wingi wilaya ya Kondoa na Chemba. Pia wanapatikana maeneo ya Mpakani mwa mkoa wa Manyara na Dodoma.

List Itaendelea...

NB: NAJUA UTASHANGAA KUTOYAONA MAKABILA YA WANYAKYUSA, WAHAYA NA WACHAGA HAPO JUU, UKWELI NI KUWA KWA KIPIMO CHA UWINGI WANAPWAYA SANA ILA WAMEFANIKIWA KWENYE UMAARUFU NA ELIMU TU.

Karibuni kwa mjadala
Ni dhahiri na sioni cha kujadili. Jamii yenye watu wengi zaidi ndiyo itakayokuwa na uwingi katika wanaoongea lugha ya jamii husika.
 
Huyu mjinga anatulisha matango ,waikizu na wasukuma wapi na wapi? Ungesema waikizu ,wakurya,wazanaki ,wakabwa hapo sawa,

Kwa hapo tu umesababisha kutoamini taarifa yako.

Fake news hiyo don't trust
 
Back
Top Bottom