Top 6 ya ving'amuzi bora Tanzania vyenye wateja wengi, Unachotumia kipo?

Ha..ha..ha..mimi walinibadilishiabadilishia setlait hadi nikasusa kutumia king'amuzi cha Continental. Kila wiki ilinibidi nimwite fundi na kumlipa ili aiseti upya.
Hadi nikachoka na kuamua kukitelekeza jumla.

Ivi bado kipo.
hahahaha aisee nomaa
 
Nilianzia startimes, baadae nikahamia strtimes, nilipotoka hapo dadeki nikahamia kwa Azam, hadi sasa namiliki king'amuzi cha Azam na Dstv.

Jamii Forums mobile app
 
Kama mtu anaujuzi wa ving'amuzi vya kukamata dishi la chaneli za Free to air naomba alete maujuzi hapa,
Mi nikifanikiwa kupata chaneli hizo sijisumbui na ving'amuzi vya kulipia hasa kutokana na ugumu wa maisha wa awamu hii ya tano.
 
Sina uzoefu wowote wa namna dish linavyofungwa isipokuwa ninajua nadharia ya nini kinachofanyika.

Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hujafunga dish.
1. Unahitaji kutazama chaneli zipi au zenye mambo zenye programu gani kama ni michezo, tamthiliya na filamu n.k

2. Ukubwa dish utalonunua utategemea sana aina ya chaneli unazotaka kutazama, mathalani dish la kuanzia futi 6 na kuendelea linakupa uhakika wa kupokea signal reception nzuri.

3. Kama mahitaji yako ni mpira wa miguu pekee na unataka kutazama ligi kuu kubwa za Ulaya, kwa sasa unahitajika kuwa na madish mawili maana uelekeo wa satellite ni tofauti.

4 Tambua kuwa cha bure huwa hakidumu. Mabadiliko ya mifumo, urushaji wa frequency, aina ya encryption n.k hubadilika kila mara hivyo si ajabu satellite ilikuwa ikihodhi channel fulani mwezi au mwaka huu ikabadilika na usiipate tena mwaka au mwezi ufuatao.

Note:
(I)
Kwa kawaida satellite huwa zinapatikana upande ama mashariki au magharibi mwa dunia (reference ikiwa ni mstari mkuu wa longtude). Kwa mantiki hiyo basi kulikangana na uwepo wa nchi mbalimbali kijiografia, uelekeo wa satellite huweza kuwa kaskazini magharibi, kaskazini mashariki, kusini magharibi, kusini mashariki, magharibi, mashariki etc.
Hivyo ni lazima dish lielekee upande husika kulingana na wapi satellite ipo huko angani kutokea uso wa eneo fulani kijiografia (latitude + longtude).

(II) Horizontal paning
Kitu kingine cha kujua ni azimuth yaani umbali wa nyuzi kiasi gani kutoka 0° kuelekea ama mashariki au magharibi.

Kwa kifupi huu ni uelekeo wa dish kulia ama kushoto kutoka katika muhimili wake (base support)

(III) Vertical paning
Jambo jingine kujua ni elevetion, yaani dish lako linyanyuke kiasi gani ama lishuke nyuzi kiasi gani.

Zaidi:
Utahitajika kuwa na dish la ukubwa uutakao/unaohitajika.
Utahitajika kuwa na LnB yaani kinasa mawimbi ambacho hufungwa mbele ya dish, sasa hapa kuna Ku au C band LnB
Mengineyo utahitajika kuwa na waya mrefu, viunganishi "connectors", cutter,
diseqc (km una mpango wa kufunga lnb mbili au zaidi), receiver (freesat, hellobox, alphabox, tiger etc).

Mengineyo
Tumia mtandao wa www.lyngsat.com kujua azimuth value, elevation value kwa kila satellite utayotaka kuitrack.

Google satellite footprint ili ujue kama ina covarage ya eneo ulilopo na ina nguvu kiasi gani (eirp), eirp value itakufanya ujue ukubwa wa dish gani utumie.

Zaidi soma mitandaoni kwa ujuzi zaidi au tafuta fundi ukiwa na vifaa vyako tayari, ukimuachia fundi akusaidie kununua jiandae kuwekewa cha juu kwa namna wabongo walivyo na roho ya ulafi wa fedha.

Mkuu Watu8,
Mie ni mpenzi sana wa Action Movies (za kizungu/american).
Decoder gani iko poa kwa action movies? Yaani vigezo viwili tu : Action Movies, na ubora wa picha (HD).

-Kaveli-
 
dstv ukiweka na explora ndio kiboko zaidi tamu mbaka basi full kurekodi catch up wanakuwekea series ambazo utaangalia kwa mda wako na box office unanunua movie rewind and foward nowmaa


Mkuu chokodari, hiyo 'box office' ni full movies tu eeh?
Mie ni mpenzi mnooo wa action Movies. Majuzi nimenunua startimes ila upuuzi mtupu... hawana action movies za maana, wamejaza mifilamu ya kichina na kinaigeria.

Tatizo la hao dstv... vifurushi vyao ni gharama juu.

-Kaveli-
 
Mkuu chokodari, hiyo 'box office' ni full movies tu eeh?
Mie ni mpenzi mnooo wa action Movies. Majuzi nimenunua startimes ila upuuzi mtupu... hawana action movies za maana, wamejaza mifilamu ya kichina na kinaigeria.

Tatizo la hao dstv... vifurushi vyao ni gharama juu.

-Kaveli-
yaa box office ni movie tu unanunua but catch up unachagua movie au series au kid films wamekuwekea bureee mkuu yaani dstv ukinunua na explora nomaa hakuna king'amuzi chochote kinachofikia sijaonaga kama unaitaka series ila hauna mda wa kuangalia unarekodi unakujakuona baadaye
 
yaa box office ni movie tu unanunua but catch up unachagua movie au series au kid films wamekuwekea bureee mkuu yaani dstv ukinunua na explora nomaa hakuna king'amuzi chochote kinachofikia sijaonaga kama unaitaka series ila hauna mda wa kuangalia unarekodi unakujakuona baadaye


Mkuu unamaanisha kuwa Box Office ni unanunua movie by Online Purchase?
Na Catch Up ni movies zinaoneshwa kwenye kifurushi husika?
Au sijakuelewa vizuri kiongozi.

-Kaveli-
 
1. DSTV
2. Azam
3. Zuku Tv
4. Ting HD
5. Startimes
6. Digtek
7. Continental decoder
My take; Dialo kashika mkia na awe analipa kodi na wafanyakazi wake
 
Back
Top Bottom