Top 5 Conspiracy theories ever happened in Tanzania in 2000s (Swahili Discussion)

Wanao kuchallenge wapo sahihi ila hawakuwemo akilini mwako. Anyway umejitahidi
 
Habari wana JamiiForum. Awali ya yote natanguliza shukrani kwa wadau wote wa JF. Nimejiunga Jamii Forum ili kupata ujuzi, ku-share mawazo na kuongeza maarifa mbalimbali maana naamini humu kuna watanzania wengi wenye akili na uwezo mkubwa wa kufikiri.

Leo nimeandaa uzi wangu wa kwanza. Karibuni wote kushiriki.

Conspiracy theories (Nadharia za uongo) ni nadharia zinazotengenezwa katika jamii na mtu au kikundi cha watu ambazo hazina ushahidi wa kihistoria au utafiti wa kisayansi zikiwa na lengo la kuhamisha akili na hisia za watu ili kuacha kufikiri masuala ya msingi na kuelekeza mawazo yote huko. Mtu au watu wanao anzisha nadharia hizi huwa wana lengo au malengo ya muda mfupi na mrefu kwa maanufaa yao binafsi.

Zifuatazo ni Conspiracy theories kubwa kuwahi kutokea katika karne hii ya 21 katika nchi ya Tanzania.
1. BABU WA LOLIONDO.
Nadharia hii ililikusanya taifa zima kuanzia viongozi wakubwa wa serikali, dini na watu maarufu, hadi kufikia kipindi taifa la tanzania lilipanda kwenye orodha ya nchi zinazoamini uchawi na ushirikina. Najua wengi mtasema kuwa Babu wa loliondo ndio aliyezusha nadharia hii, lakini swali la kujiuliza kwa nini ilivuma sana kwenye vyombo vya habari na kuwa national topic. Je katika kipindi hicho nini kilikuwa kikiendelea katika taifa wakati watanzania wengi wakiwa loliondo wanasubiri kikombe huku wengine wakifuatilia sakata hili kwa makini?

2. KUVUMA KWA UWEPO WA POPO BAWA
Popo bawa ni kiumbe wa aina gani? Anafananaje? Leo hii ukifanya utafiti kwa watanzania kama wanafahamu au wanajua wapi alipoishia huyu popo bawa hawajui na huenda wamesahau kuvuma kwa popo bawa kulitoa mwanya kiasi gani watu kusahau mambo muhimu kwenye jamii na kuanza kufuatilia leo popo bawa kaingia kwa nani na kesho ni zamu ya nani.

3. WATU WASIO JULIKANA
Hii ni nadharia ya kufurahisha na kusikitisha sana imetoa majibu rahisi kwenye swali gumu. Nafikiri ni nadharia ambayo itaendelea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu yote yatakayokuja kutokea kwenye jamii.

4. UWEPO WA MTU AITWAYE ALBERT BASHITE
Ki ukweli kuna utafiti uliwahi kufanyika unao sema kati ya watanzania wanne mmoja ni kichaa. Sitaki kuamini utafiti huo maana unaweza kukuta hata mimi ni kichaa. Ila wakati sakata la ubatizo wa jina la bashite watu wengi walisahau majukumu yao na kudhani jina la Bashite litakuwa mkombozi wa taifa. Lilivuma mpaka watu wakasahau mambo mengi ya msingi katika taifa ambayo ni makubwa kuliko jina hilo. Magazati yaliandika nakala nyingi, Mitandao ya kijamii ndio usiseme. Lakini mwishowe nadharia hii ilipita na wenye kunufaika nayo wametimiza malengo.

5. BAO LA MKONO
Hii ndio nadharia ambayo inatoa majibu rahisi kwa watu walioshindwa jambo fulani, Ilivuma imevuna na huenda tutaisikia tena miaka ijayo.

Zipo conspiracy theories nyingi tu ila kwa leo niishie hapa. Karibuni tena wana JF katika kuchangia
6) WANYONYA DAMU

7)UGONJWA WA KIMETA ( ugonjwa uliokuwa unasemekana unasambaa kupitia barua)
 
Kwanza kabisa tafuta kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyoandikwa na TUKi uangalie maana ya Conspiracy theory.

Halafu umeandika habari za mtaani sana kama sio kijiweni nikiwa na maana hazifikirishi wasomaji.

Nilitegemea kuona walau nadharia kadhaa kuhusiana na kifo tata cha aliyekuwa Gavana.wa Benki Kuu ya Tanzania, Daudi Ballali.

Sasa wewe unatuletea mambo ya mtaani ya popobawa, utani uliopindukia.
221
20190803_074739.jpeg
 
Back
Top Bottom