Top 5 Conspiracy theories ever happened in Tanzania in 2000s (Swahili Discussion)

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,028
2,000
Habari wana JamiiForum. Awali ya yote natanguliza shukrani kwa wadau wote wa JF. Nimejiunga Jamii Forum ili kupata ujuzi, ku-share mawazo na kuongeza maarifa mbalimbali maana naamini humu kuna watanzania wengi wenye akili na uwezo mkubwa wa kufikiri.

Leo nimeandaa uzi wangu wa kwanza. Karibuni wote kushiriki.

Conspiracy theories (Nadharia za uongo) ni nadharia zinazotengenezwa katika jamii na mtu au kikundi cha watu ambazo hazina ushahidi wa kihistoria au utafiti wa kisayansi zikiwa na lengo la kuhamisha akili na hisia za watu ili kuacha kufikiri masuala ya msingi na kuelekeza mawazo yote huko. Mtu au watu wanao anzisha nadharia hizi huwa wana lengo au malengo ya muda mfupi na mrefu kwa maanufaa yao binafsi.

Zifuatazo ni Conspiracy theories kubwa kuwahi kutokea katika karne hii ya 21 katika nchi ya Tanzania.
1. BABU WA LOLIONDO.
Nadharia hii ililikusanya taifa zima kuanzia viongozi wakubwa wa serikali, dini na watu maarufu, hadi kufikia kipindi taifa la tanzania lilipanda kwenye orodha ya nchi zinazoamini uchawi na ushirikina. Najua wengi mtasema kuwa Babu wa loliondo ndio aliyezusha nadharia hii, lakini swali la kujiuliza kwa nini ilivuma sana kwenye vyombo vya habari na kuwa national topic. Je katika kipindi hicho nini kilikuwa kikiendelea katika taifa wakati watanzania wengi wakiwa loliondo wanasubiri kikombe huku wengine wakifuatilia sakata hili kwa makini?

2. KUVUMA KWA UWEPO WA POPO BAWA
Popo bawa ni kiumbe wa aina gani? Anafananaje? Leo hii ukifanya utafiti kwa watanzania kama wanafahamu au wanajua wapi alipoishia huyu popo bawa hawajui na huenda wamesahau kuvuma kwa popo bawa kulitoa mwanya kiasi gani watu kusahau mambo muhimu kwenye jamii na kuanza kufuatilia leo popo bawa kaingia kwa nani na kesho ni zamu ya nani.

3. WATU WASIO JULIKANA
Hii ni nadharia ya kufurahisha na kusikitisha sana imetoa majibu rahisi kwenye swali gumu. Nafikiri ni nadharia ambayo itaendelea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu yote yatakayokuja kutokea kwenye jamii.

4. UWEPO WA MTU AITWAYE ALBERT BASHITE
Ki ukweli kuna utafiti uliwahi kufanyika unao sema kati ya watanzania wanne mmoja ni kichaa. Sitaki kuamini utafiti huo maana unaweza kukuta hata mimi ni kichaa. Ila wakati sakata la ubatizo wa jina la bashite watu wengi walisahau majukumu yao na kudhani jina la Bashite litakuwa mkombozi wa taifa. Lilivuma mpaka watu wakasahau mambo mengi ya msingi katika taifa ambayo ni makubwa kuliko jina hilo. Magazati yaliandika nakala nyingi, Mitandao ya kijamii ndio usiseme. Lakini mwishowe nadharia hii ilipita na wenye kunufaika nayo wametimiza malengo.

5. BAO LA MKONO
Hii ndio nadharia ambayo inatoa majibu rahisi kwa watu walioshindwa jambo fulani, Ilivuma imevuna na huenda tutaisikia tena miaka ijayo.

Zipo conspiracy theories nyingi tu ila kwa leo niishie hapa. Karibuni tena wana JF katika kuchangia
 
Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
8,608
2,000
Mada ni nzuri Ila umeikosea ulipoingiza mambo ya Albert daudi bashite watu wasiojulikana na bao LA mkono kimsingi hizo mada 3 hapo juu sio conspiracy theories kwakuwa

1.DAB yupo kweli na fojali yake isiyoeleweka IPO kweli sasa hii haiwezi kuwa ct

2.watu wasiojulikana hii pia sio ct kwasababu watu wanapotea kweli watu wanapatikana kwenye viloba wakiwa maiti halafu majibu ya wenye dhamana hayaeleweki na wakati mwingine husema ni watu wasio julikana sasa hii haiwezi kuwa ct kwakuwa ni mambo yapo

3.bao LA mkono hili alilisema nape na alilotaka liwe likawa sasa hayo yote hayaswihi kuwekwa kwenye kategoria ya conspiracy theories hata kidogo

Nitarudi
 
kupukupu

JF-Expert Member
Aug 4, 2016
431
1,000
kwamba hizo ndo conspiracy theories zilizokuamisha wewe katika kufanya mambo ya msingi? huu upupu uupelekage huko huko vijiweni, haya sio mambo ya kuwaletea great thinkers.
 
Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,510
2,000
Nashauri uka-google zaidi ujue maana ya conspiracy theories. Umepuyanga zaidi ya 50%!
 
upendodaima

JF-Expert Member
May 23, 2013
4,073
2,000
Nakushauri uwe msoma sredi tu kama mimi na ukipata mwanya unachangia kiasi.Kuanzisha nyuzi bila kujipanga mwisho ni aibu kama hii..
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,581
2,000
conspiracy = a secret plan between two or more people to commit an illegal act/hostile plan
conspiracy theory = a belief that a particular event is a result of secret plot...
theory hasa ni nini?
mengine yanaweza kuwa "Myth" or a mistaken/false belief kama hili la babu wa loliondo
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,028
2,000
kwamba hizo ndo conspiracy theories zilizokuamisha wewe katika kufanya mambo ya msingi? huu upupu uupelekage huko huko vijiweni, haya sio mambo ya kuwaletea great thinkers.
Asante mkuu kwa kuchangia, next time nitajipanga. Mwanzo mgumu
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,028
2,000
conspiracy = a secret plan between two or more people to commit an illegal act/hostile plan
conspiracy theory = a belief that a particular event is a result of secret plot...
theory hasa ni nini?
mengine yanaweza kuwa "Myth" or a mistaken/false belief kama hili la babu wa loliondo
I passed through all those definitions before writing and posting this thread. I wanted to bring something basing on my intuition. Thank you though for reminding me a great thinker
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,028
2,000
Nakushauri uwe msoma sredi tu kama mimi na ukipata mwanya unachangia kiasi.Kuanzisha nyuzi bila kujipanga mwisho ni aibu kama hii..
I can't be a merely reader and commentator. I believe I can be better than this. I will take your text as a challenge to push me creating something new and interesting next time. Asante mkuu
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,028
2,000
Mada ni nzuri Ila umeikosea ulipoingiza mambo ya Albert daudi bashite watu wasiojulikana na bao LA mkono kimsingi hizo mada 3 hapo juu sio conspiracy theories kwakuwa

1.DAB yupo kweli na fojali yake isiyoeleweka IPO kweli sasa hii haiwezi kuwa ct

2.watu wasiojulikana hii pia sio ct kwasababu watu wanapotea kweli watu wanapatikana kwenye viloba wakiwa maiti halafu majibu ya wenye dhamana hayaeleweki na wakati mwingine husema ni watu wasio julikana sasa hii haiwezi kuwa ct kwakuwa ni mambo yapo

3.bao LA mkono hili alilisema nape na alilotaka liwe likawa sasa hayo yote hayaswihi kuwekwa kwenye kategoria ya conspiracy theories hata kidogo

Nitarudi
Asante kwa kuchangia great thinker. Napenda kukosolewa pale napoingia chaka
 
FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,256
2,000
Habari wana JamiiForum. Awali ya yote natanguliza shukrani kwa wadau wote wa JF. Nimejiunga Jamii Forum ili kupata ujuzi, ku-share mawazo na kuongeza maarifa mbalimbali maana naamini humu kuna watanzania wengi wenye akili na uwezo mkubwa wa kufikiri.

Leo nimeandaa uzi wangu wa kwanza. Karibuni wote kushiriki.

Conspiracy theories (Nadharia za uongo) ni nadharia zinazotengenezwa katika jamii na mtu au kikundi cha watu ambazo hazina ushahidi wa kihistoria au utafiti wa kisayansi zikiwa na lengo la kuhamisha akili na hisia za watu ili kuacha kufikiri masuala ya msingi na kuelekeza mawazo yote huko. Mtu au watu wanao anzisha nadharia hizi huwa wana lengo au malengo ya muda mfupi na mrefu kwa maanufaa yao binafsi.

Zifuatazo ni Conspiracy theories kubwa kuwahi kutokea katika karne hii ya 21 katika nchi ya Tanzania.
1. BABU WA LOLIONDO.
Nadharia hii ililikusanya taifa zima kuanzia viongozi wakubwa wa serikali, dini na watu maarufu, hadi kufikia kipindi taifa la tanzania lilipanda kwenye orodha ya nchi zinazoamini uchawi na ushirikina. Najua wengi mtasema kuwa Babu wa loliondo ndio aliyezusha nadharia hii, lakini swali la kujiuliza kwa nini ilivuma sana kwenye vyombo vya habari na kuwa national topic. Je katika kipindi hicho nini kilikuwa kikiendelea katika taifa wakati watanzania wengi wakiwa loliondo wanasubiri kikombe huku wengine wakifuatilia sakata hili kwa makini?

2. KUVUMA KWA UWEPO WA POPO BAWA
Popo bawa ni kiumbe wa aina gani? Anafananaje? Leo hii ukifanya utafiti kwa watanzania kama wanafahamu au wanajua wapi alipoishia huyu popo bawa hawajui na huenda wamesahau kuvuma kwa popo bawa kulitoa mwanya kiasi gani watu kusahau mambo muhimu kwenye jamii na kuanza kufuatilia leo popo bawa kaingia kwa nani na kesho ni zamu ya nani.

3. WATU WASIO JULIKANA
Hii ni nadharia ya kufurahisha na kusikitisha sana imetoa majibu rahisi kwenye swali gumu. Nafikiri ni nadharia ambayo itaendelea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu yote yatakayokuja kutokea kwenye jamii.

4. UWEPO WA MTU AITWAYE ALBERT BASHITE
Ki ukweli kuna utafiti uliwahi kufanyika unao sema kati ya watanzania wanne mmoja ni kichaa. Sitaki kuamini utafiti huo maana unaweza kukuta hata mimi ni kichaa. Ila wakati sakata la ubatizo wa jina la bashite watu wengi walisahau majukumu yao na kudhani jina la Bashite litakuwa mkombozi wa taifa. Lilivuma mpaka watu wakasahau mambo mengi ya msingi katika taifa ambayo ni makubwa kuliko jina hilo. Magazati yaliandika nakala nyingi, Mitandao ya kijamii ndio usiseme. Lakini mwishowe nadharia hii ilipita na wenye kunufaika nayo wametimiza malengo.

5. BAO LA MKONO
Hii ndio nadharia ambayo inatoa majibu rahisi kwa watu walioshindwa jambo fulani, Ilivuma imevuna na huenda tutaisikia tena miaka ijayo.

Zipo conspiracy theories nyingi tu ila kwa leo niishie hapa. Karibuni tena wana JF katika kuchangia
Kwanza kabisa tafuta kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyoandikwa na TUKi uangalie maana ya Conspiracy theory.

Halafu umeandika habari za mtaani sana kama sio kijiweni nikiwa na maana hazifikirishi wasomaji.

Nilitegemea kuona walau nadharia kadhaa kuhusiana na kifo tata cha aliyekuwa Gavana.wa Benki Kuu ya Tanzania, Daudi Ballali.

Sasa wewe unatuletea mambo ya mtaani ya popobawa, utani uliopindukia.
 
Basham

JF-Expert Member
Oct 10, 2014
741
500
Daah ila mleta mada amekua mvumilivu hataree pamoja na Chalenji zote izo amekua mstaarabu, kweli bado ni Mgeni

Karibu sanaa hata hao wanaokukashifu walianza kama wewe tuu uku sio pa kispot spot lazima ujipangee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom