TOP 10 za Rais Kikwete

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,614
"Tumeuanza mwaka wa tano na wa mwisho wa Term ya kwanza ya Rais Kikwete.................Tunaweza kutaja mambo 10 ambayo Rais Jakaya Kikwete ameweza kuyafanya na kuyafanikisha na yaliyomshinda kwa miaka minne iliyopita?"

Ansbert Ngurumo
Tanzania Daima 10 january 2010
 
Ameweza Ameshindwa
1 Chuo Kikuu cha Dodoma 1. Muafaka wa kisiasa zanzibar
 
AMEWEZA-Kuwaingiza kwenye utawala wanamtandao wote

AMESHINDWA-Kukemea uozo wowote japokuwa anawafahamu watendaji wabovu!
 
ameweza: kuwadai wezi walichoiba kama wakopaji wanavyodaiwa

ameshindwa: kuwafikisha wezi wa Mgodi wa kiwira mahakamani
 
Ameweza: Kuziba masikio na kuendelea na safari za nje kwa manufaa anayoyaelewa yeye na walio karibu yake...

Ameshindwa: Kutekeleza kauli mbiu yake ya uchaguzi ya maisha bora kwa kila mtanzania...


Annina
 
Ameweza: Kuthibitisha kuwa Watanzania huwa wanatoa kura zao kwa kuvutiwa na tabasamu la mgombea.

Ameshindwa: Kuthibitisha kuwa nyuma ya tabasamu ni Rais makini anayeweza kusimamia katiba ya Jamhuri.
 
Ameweza:
1.Kutembelea nchi nyingi kuliko raisi yeyote aliemtangulia
2. Kubembea Jamaica
3. "Kupimwa akili"

Ameshindwa:
1. Kutembelea sehemu za Tanzania (Tanganyika) ambako si ajabu bado wanafikiri Nyerere ndie rais wa Tanzania!
2. Kuonesha mfano kwa kutembelea vivutio vya ndani, zaidi ya kufungua hoteli za kitalii
3. Kupata ufumbuzi wa shida yake ya "akili", jambo ambalo lingekuwa rahisi, kwa KUKAA NYUMBANI
 
Kauli mbiu ya Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya haikuwa na manufaa yoyote kwani tuliona uzembe wa hali ya juu katika utendaji wake na kufanya maamuzi muhimu ya nchi.

Kauli mbiu ya Maisha bora kwa kila Mtanzania haikuwa na manufaa yoyote kwani katika kipindi chake maisha ya Watanzania walio wengi yameendelea kuwa magumu zaidi.

Ahadi zake za kuipitia mikataba ya uchimabji wa madini ambayo Watanzania wengi tumeikuwa tukiilalamikia tangu ipitishwe 2000 kwamba haina maslahi kwa Watanzania hadi hii leo bado hajazitekeleza. Bado tunapata 3% ya mapato yanayotokana na rasilimali zetu wakati "wachukuaji" wakiendelea kuondoka na 97% na hivyo kuijipatia faida kubwa sana na kuongeza faida kwa shareholders wao.
 
Ameweza kuthibitisha kuwa watanzania hata uwe
kiongozi mbovu kiasi gani.hawatachukua hatua yoyote
 
hajaweza hata kitu kimoja

Humtendei wema ndugu yangu...ameweza kubembea kule Jamaica, kuendeleza uVDG, kupiga picha na kina Drogba na kuwapa mlo wa nguvu uliowagharimu walipa kodi shilingi bilioni 9.7 (inasemekana) labda Ikulu watatoa gharama rasmi zilizohusiana na mlo huo wa nguvu. Of course with a ligh touch....:)
 
Ameweza: Kutawala Tanzania huku akiishi ughaibuni (80% ya muda wake anautumia kwa safari za nje)

Ameshindwa: Kusoma alama za nyakati
 
AMEWEZA kuwa na orodha ya wauza unga(madawa ya kulevya) wote nchini.
AMESHINDWA kuwachukulia hatua wauza unga wote ikiwa ni kuwafikisha mahakamani.
(2) AMEWEZA kupindisha sheria rafiki yake ditopile atuhumiwe kuua bila kukusudia badala ya kushitakiwa kwa mauaji.
AMESHINDWA kuzuia rafiki yake Dito asifariki dunia ghafla.
 
Ameweza: Kuwaaminisha watanzania kuwa mafisadi wanaomzunguka ni wajanja sana na hawakamatiki.

Ameshindwa:Kujua kwa nini nchi anayoiongoza ni masikini.
 
Ameweza kumleta kocha wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Maximo na kuweza kuhamasisha mchezoo wa soka kwa kushiriki mechi nyingi uwanjani.

Natumai huenda kipindi kijacho akaahidii kutuachia uwanja mwingine wa kisasa wa soka.
 
Hii sasa ni chuki. Hata kitu kimoja hajaweza?


sasa kama wewe unacho alicho weza si uandike au utuambie mbona unapinga tu wakati kila kitu umepewa unaruhusiwa kuandika mazuri yote na aliyo fanikisha. kila mtu ana mtazamo wake kwa hiyo sema mtazamo wako na ikiwezekana list mazuri yote aliyo fanya kwa mtazamo wako.

kwa sababu tunatofautiana kwa mfamo mimi baba yangu ni muuza unga kitendo cha kutowafunga ingawa analist ya wauza unga wote wakubwa nchini kama alivyo tuambia kwangu itakuwa ni kitu kizuri ila kwa watanzania ni kushidwa kutekeleza majukumu yake
 
Ameweza: (1) Kujenga shule nyingi za kata, maarufu kama (Voda fasta) ambazo anaogopa yeye na mawaziri wake kupeleka wanao wakasome huko
(2) Kufumbia macho suala la udini (Mahakama ya Kadhi na OIC) kujadiliwa ili liingizwe kwenye Katiba ya nchi (3) Kuhudhuria mechi nyingi za mpira wa miguu kuliko Nyerere, Mwingyi na Mkapa

Hakuweza na hatoweza: kuleta maisha bora kwa kila mtanzania
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom