Top 10 ya treni zenye mwendokasi zaidi duniani

Quinn

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
473
1,179
1. Shanghai Maglev (427.2km/hr)

Hii ndo treni inayoongoza kwa spidi kuwa duniani na Imetengenezwa nchini China.

Shanghai Maglev inasafifi umbali wa kilometa 30.4 kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Shanghai na kuelekea kituo cha treni cha Longyang nje ya mji wa Shanghai kwa dakika tano (5 minutes).

Treni hii utumia mfumo wa wa magnetic levitation technology.

2. Fuxing Hao CR400AF/BF (398.4 km/hr)

Hii ndo treni ya pili duniani yenye mwendokasi.

Treni hii pia imetengenezwa nchini China na inajulikana kwa jina la “Fuxing Hao” kwa kiingereza inamaanisha “Rejuvenation” (in swahili ni Ufufuo).

Kwenye uzao huu walitoa treni mbili ambazo ni CR400AF na CR400BF na walizipa majina ambayo ni “Dolphin Blue” kwa CR400AF na “ Golden phoenix” kwa CR400BF.

Treni hizo zinauwezo wa kusafirisha abiria 556 kutoka Beijing south kuelekea Shanghai Hangqiao ambao ni umbali wa 1,318km kwa masaa 4.

3. Shinkansen H5 na E5 ( 358.4km/hr)

Hichi ni kizazi kipya cha treni nchini Japan ambacho kilizinduliwa siku ya sherehe ya miaka 54 ya japan kwenye utumiaji wa usafiri wa treni zenye spidi kubwa ( High speed train travel).

Treni hii ufanya safari kutoka Tokyo na kwenda Osaka umbali wa kilometa 397 kwa saa (1hr).

4. Italo na Frecciarossa (352km/hr).

Hichi ndo kizazi cha treni chenye kasi zaidi kwa bara la ulaya ambacho kina uwezo wa kutoa abiria kutoka Milan kwenda Florence au Mji wa Rome kwa masaa 3.

Frecciarosa ujulikana kwa jina maarufu la “Red Arrow” ilizinduliwa mwaka 2015 mjini Milan nchini Italia.

5. Renfe Ave (347.2km/hr)

Hii ndo treni yenye mwendokasi zaidi nchini Hispania iliotengenezwa na kampuni ya Siemens.

Treni hii utoa huduma ya safari ndefu na ufanya safari zake kutoka mji wa Barcelona kwenda Paris nchini ufaransa kwa masaa 6.

6. Haramain western Railway (347.1km/hr)

Hii ni treni inayounganisha majiji matakatifu nchini Saudi Arabia.

Treni hii usafiri kutoka Mecca kwenda Medina umbali wa kilometa 449.6 kwa masaa 2 na 1/2 (2hrs 30minutes).

7. DeutscheBahn ICE (328km/hr)

Hii ni treni yenye mwendokasi zaidi nchini ujerumani. Treni hii ilitengenezwa na kampuni ya Siemens kama ilivyokuwa ile ya Hispania “Renfe AVE”.

Treni hii inaunganisha jiji la Berlin na Munich. Pia treni hii hupita kwenye handaki (channel tunnel) na kufanya safari zake kutoka Frankfurt kuelekea London.

8. Korail KTX (328 km/hr)

Hii ni train yenye mwendokasi zaidi nchini korea ya kusini. KTX ilizinduliwa mwaka 2004.

Treni hii inaunganisha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon na Gangneung hadi kufikia Seoul.

9. Eurostar e320 na TGV (320 km/hr)

Hizi ni treni ambazo waliziboresha (upgraded) na kuweza kufikia speed ya 320km/hr.

Eurostar utumia masaa 2 kusafiri kati ya Brussels, Paris na London.

10. Thalys (297.6km/hr)

Hii ni treni ya mwendokasi inayounganisha Amsterdam, Brussels, Paris na Cologne.

Hii ni treni ya muhimu zaidi kwa bara la ulaya kwani inapitia majiji mengi na Mwaka 2015 iliongeza route ya Dortmund kupitia Brussels kwenda Paris.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Duh, hizo mbili za wachina ni next level jo, afu wamewajengea wakenya geresha.
Treni zina manufaa makubwa sana kwa nchi kubwa kubwa kama Tz, congo, china, us etc.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivyokua nashuka haraka nilijua takutana na tren ambayo inafanya route mpka tanzania.🤔
 
Hii tech ilikua inashikiliwa na Japan sasa china katakeover!!
Nilijua siemens wamekufa baada ya simu zao.kua kimeo kumbe wako kwenye biashara kubwa zaidi!
Hivi ukijenga reli kama hii unaomba na tenda ya kutengenezewa treni kabisa au unaenda kununua hata treni ya kasi za mtumba?
Maana naona makampuni machache yanayotengeneza hii ndude
 
Back
Top Bottom