Too much mabango ya matangazo ya wachawi (waganga wa kienyeji)

Hayajamani

JF-Expert Member
Jul 2, 2012
883
500
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari saa mbili usiku ndipo nikajue kumbe mauaji ya Mara hivi karibuni yalisababiswa na imani za kishirikina.

Kama tujuavyo hatuwezi kuendelea bila kuamini katika sayansi na kuacha imani za kishirikina, na nyingine za ajabu ajabu zinazopitia mlango wa nyuma kwa kuichafua dini! Ingawa jamani kwa sisi wa Tz bado, tufanye jitihada haswa kujinasua na hizi imani, manake hata maprofessa, viongozi wakubwa serikalini wana imani ya huu uchafu. Ukimfuma mtu kavua shati we mwangalie utaona machale kifuani, mikononi, shingoni kisa eti kujikinga, kutoa mikosi etc lakini ndio mabalaa hayaishi na wengi wanaopatwa ni walewale wenye machale au eti waliombewa kwa imani.... Jamani shida za nini? Mbona hatujiamini? Mbona tunaharibu sura zetu kwa kuzitoboatoa kama machujio ya nazi?

Sasa jamani haya mabango yenye matangazo ya hao wahuni mbona yame zagaa sana? Eti wanatibu magonjwa sugu, kutoa mikosi, kupandiswa cheo, kumvuta mpenzi, kuongeza maumbile, jinsi ya kujiunga na freemason etc. Je yamelipiwa na yapo kihalali? Kama sio serikali na manispaa zipo usingizini? Watu wa mazingira pia mpo wapi? Mbona miti imeshambuliwa sana na hayo mabango? Mfano ule mbuyu pale Kinondoni umejaa matangazo ya kichawi mpaka unashindwa kupumua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom