Tonny Ngombale Mwiru afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Hii ni siasa au uhalifu? Ingepelekwa kwenye jukwaa stahiki kwani kwa maoni yangu hii siyo mada ya siasa.
 
.....Wenzake wasiojulikana....siku isiyofahamika na mahali pasipojulikana. Halafu mtu anapelekwa mahakamani na anaswekwa rumande kwa maelezo haya. Baada ya wiki mbili analetwa mahakamani Polisi wanasema upelelezi bado haujakamilika. Sasa grounds za kumweka ndani au ni zipi? Wahanga wa mifumo hii ni wengi. NDO MAANA TUNAHITAJI CHANGES
 
Kutoka Blog ya Michuzi:

Tonny Mwiru, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, ameburuzwa kotini kwa tuhuma za kujipatia Sh milioni 424 kwa njia za udanganyifu.

Mtoto huyo wa kigogo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu leo.

akisomewa mashitaka yake leo na Inspecta wa polisi, Emma Mkonyi mbele ya hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe mshitakiwa alidaiwa kughushi, kula njama na kujipatia fedha hizo kwa njia za udanganyifu.

Hakimu Mirumbe alionekana kutia shaka na kumuuliza mshitakiwa huyo kama ni mtoto wa mwanasiasa huyo ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais ambapo mshitakiwa alikiri kuwa mzee huyo ni baba yake wa kumzaa.

Tonny alidaiwa akiwa na wenzake wasiyofahamika katika siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam walikula njama ya kuiibia kampuni ya SCI (TZ) LTD kiasi hicho cha fedha kwa njia ya ujumbe wa kuhamisha fedha kwa haraka.

Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kughushi fomu ya benki ya kuhamishia fedha yenye namba E17 ya Agosti 29, 2008 kwa nia ya kuonyesha kuwa fomu hiyo ni halali imesainiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ravishankar Rasiman.

Shitaka la tatu ilidaiwa Agosti 29, 2008 katika benki ya barcley’s iliyoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam aliwasilisha fomu hiyo kwa mfanyakazi wa benki,Bituni Chiza ambaye huku akijua haikuwa halali.

Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kati ya Septemba na Octoba 2008 katika benki ya CRDB tawi la Kijitonyama, Dar es Salaam alichota Sh 424,458,799.29 kutoka katika akaunti namba 01j014293000 ya SCI (TZ) LMD akionyesha kuwa fedha hizo ni halali zimetolewa na kampuni hiyo kwenda kwenye kampuni ya Temm Power Solution akijua haikuwa kweli.

Hata hivyo Tonny alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashalti ya dhamana.

Ili apate dhamana alitakiwa na hakimu huyo kuwa na wadhamini watakaotoa Sh milioni 10 pamoja na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 31 mwaka huu.


--------------

Bado tutayaona mengi mwaka huu!

Ufisadi OYEEEE!

HAHAHA!

./Mwana wa Haki

P.S. Afadhali mimi nisiyejua kuiba, nitanusurika kuionja jela!
Hahaha why kingunge?au alihisi Tanzania ni nchi ya Ukoo wake?!!maana baba,mtoto na wajukuu wote mafisadi....
 
Hahaha why kingunge?au alihisi Tanzania ni nchi ya Ukoo wake?!!maana baba,mtoto na wajukuu wote mafisadi....

Mbona haya mambo ni ya 2010 august ? Kuyaleta leo bila kuonyesha kesi iliishaje ni ushambenga mtupu. Wekeni wazi kama aliiba na kuhukumiwa ni sawa kabisa. Na mkumbuke alikamatwa wakati Baba yake akiwa mtu muhimu sana ndani ya CCM wakati huo.
 
Jf bwana, uzi umekaa hapa miaka mitano lakini leo unaibuliwa!
Huu uzi ni wa siku nyingi na kama ikitokea mtu amecomment kwa uzi wa miaka ya nyuma unakuwa activated na kuwa kama mpya hivyo comment #36 na kisha ikafuatia comment yako ndo imeufanya uonekane kwenye list kama ni mpya na wewe ndo ukawa wa pili ku-comment, mie mwenyewe nimeshituka kuja kucheck tarehe nikaona ya siku nyingi (ikilog in kwa computer kidogo inakuwa rahisi kugundua ila kwa simu kunakuwa mara kwa mara comment mpya zinakuwa zinajitokeza hivyo kama usivyoangalia vizuri unajua mpya na kuanza ku-comment na ndio unakuwa tena kama renewed)
 
Mmenikumbusha mbali sana ,uyo hakimu ni marehemu kwa ss RIP ..mmenikumbusha machungu waungwana
 
Back
Top Bottom