Tonny Ngombale Mwiru afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tonny Ngombale Mwiru afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Aug 17, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kutoka Blog ya Michuzi:

  Tonny Mwiru, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, ameburuzwa kotini kwa tuhuma za kujipatia Sh milioni 424 kwa njia za udanganyifu.

  Mtoto huyo wa kigogo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu leo.

  akisomewa mashitaka yake leo na Inspecta wa polisi, Emma Mkonyi mbele ya hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe mshitakiwa alidaiwa kughushi, kula njama na kujipatia fedha hizo kwa njia za udanganyifu.

  Hakimu Mirumbe alionekana kutia shaka na kumuuliza mshitakiwa huyo kama ni mtoto wa mwanasiasa huyo ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais ambapo mshitakiwa alikiri kuwa mzee huyo ni baba yake wa kumzaa.

  Tonny alidaiwa akiwa na wenzake wasiyofahamika katika siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam walikula njama ya kuiibia kampuni ya SCI (TZ) LTD kiasi hicho cha fedha kwa njia ya ujumbe wa kuhamisha fedha kwa haraka.

  Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kughushi fomu ya benki ya kuhamishia fedha yenye namba E17 ya Agosti 29, 2008 kwa nia ya kuonyesha kuwa fomu hiyo ni halali imesainiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ravishankar Rasiman.

  Shitaka la tatu ilidaiwa Agosti 29, 2008 katika benki ya barcley's iliyoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam aliwasilisha fomu hiyo kwa mfanyakazi wa benki,Bituni Chiza ambaye huku akijua haikuwa halali.

  Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kati ya Septemba na Octoba 2008 katika benki ya CRDB tawi la Kijitonyama, Dar es Salaam alichota Sh 424,458,799.29 kutoka katika akaunti namba 01j014293000 ya SCI (TZ) LMD akionyesha kuwa fedha hizo ni halali zimetolewa na kampuni hiyo kwenda kwenye kampuni ya Temm Power Solution akijua haikuwa kweli.

  Hata hivyo Tonny alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashalti ya dhamana.

  Ili apate dhamana alitakiwa na hakimu huyo kuwa na wadhamini watakaotoa Sh milioni 10 pamoja na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

  Kesi hiyo itatajwa Agosti 31 mwaka huu.


  --------------

  Bado tutayaona mengi mwaka huu!

  Ufisadi OYEEEE!

  HAHAHA!

  ./Mwana wa Haki

  P.S. Afadhali mimi nisiyejua kuiba, nitanusurika kuionja jela!
   
 2. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mmmmh wamempa dhamana ama?
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Michuzi kumbe aliwapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, eee?

  Siku ya kufa nyani.... HAHAHAHA
   
 4. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je, ni huyo Kinjekitile, mtoto aliyewahi kutuhumiwa kwa kufyatua risasi, sijui kwenye disko?

  na yule mtoto wa Juma Kpuya aliyetuhumiwa pia kwa kufyatua risasi, mqmbo yalienaje?
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sASA watu wa benki walimpaje fedha bila kuwa na ushahidi na hicho wanachomshitakia sasa au mzee alitiuma vimemo?
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mod, badilisha title... huyu ni Tonny Ngombale Mwiru... Victor Kinjekitile Ngombale Mwiru ni KAKA YAKE! Sorry Victor! Sikujua una KADOGO KAKO! Tehe tehe tehe! Usinshtaki mahakamani... vidole huteleza!
   
 7. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe umependa sana kutia sana chumvi. Hapa unataja Tonny na Victor na mwanzoni ulisema mtoto pekee! Tusiojua tuamini lipi?
   
 8. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Jamani, namfahamu Kinje. Nimemfahamu zaidi ya miaka 5. Katika siku zote - hata nilipokuwa nikimtembelea nyumbani kwao Kijitonyama - sikuwahi hata siku moja kusikia ana mdogo wake anaitwa Tony. Inaonekana ni wa mama mwingine. Kwa mtaji huo nilifikiria kuwa ni MTOTO WA PEKEE. Ndio maana nimesema sikujua kama alikuwa na mdogo wake.

  Umenifahamu?
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Jamani Mzee Kingunge si ndiye mshauri wa msuala ya siasa JK kule Ikulu?
  Has Kingunge fallen out with JK?Aafu haonekani tena kwenye majukwaa.
  Ukichanganya na la kuondolewa Bashe(mtu wa RA) picha fulani inajito

  keza
   
 10. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tony na Kinje ni watu wawili tofauti,Tony ni mtoto wa mama yake mdogo na Kinje,but alikuwa anakaa hapo hapo kwa mzee kigunge Makumbusho,anayekaa kijitonyama ni Kinje!
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mtoto umleavyo......
   
 12. senator

  senator JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hata maji hufwata mkondo...na kawaida mwana wa Nyoka ni nyoka tu...
   
 13. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mbona kwa Michuzi hiyo habari yenyewe kama imetolewa? au ndo wazee washapiga zengwe.....
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Sasa tunaweza kujua ni kwanini Kingunge aliita waandishi wa habari pale maelezo na kuanza kuwaongopea kuwa si kweli kama kuna mafisadi. He knew that this Tony guy was one of them, so he was trying to cover up the whole thing so as his son could be covered.
  Lakini kwa jinsi Tanzania yetu ilivyo huyo jamaa kesi yake itakuwa kama ya Mramba, Yona na Chenge, hakuna kitakachofanyika. he is not going to prison, and if he does it will be like Mrambam anakaa siku mbili then anatoka.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo utakapojua jinsi banking sector ya Tanzania ilivyooza.
   
 16. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani angalieni iyo niliyo highlight kwa red. does it make any sense to anyone?
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Swala hapa ni kujua ni mtoto wa mzee au hapana hata kama alizaliwa na mama mwingine si hilo haliusu au kukaaa hapo kijitonyama halituhusu. swali ni Mtoto wa Kingunge au hapana basi? yanini ujieleze maneno meeengiiii weeeeeee ili iweje?umelipwa? au wewe ndie muhusika(Msemaji wa Familia) wajaribu ondoa upuuzi alioufanya huyo kijana usinukishe familia???
   
 18. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mwenye Thread hii irekebishe au moderators Jaribuni kutafuta ukweli wa habari hii.Hayo majina yaliyotanjwa hapo sio waliohusika na hiyo kesi ya Udanganyifu.Kwa kuandika majina ya watu wasiohusika tunaweza kusababisha usumbufu kwa baadhi ya watu.Mpeni muda mtoa Mada...Vinginevyo ifungeni na kuiondoa hii thread!
   
 19. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyo Bituni ashawahi kuwa mhasibu wa SCI (T) kwenye miaka ya 2003/2006 sasa sijui kama ni bahati tu kwamba yeye ndo alipokea hiyo form au dili limeenda mrama kaamua kuruka..
   
 20. sister sista

  sister sista Member

  #20
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 6, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si mtoto wa kingunge ni mtoto wa shemeji yake kingunge dada wa mke wa kingunge
   
Loading...