Tom chilala wa redio free africa ana maslahi gani katika biashara ya dowans? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tom chilala wa redio free africa ana maslahi gani katika biashara ya dowans?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Dec 12, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi wakati wa kipindi cha udondozi wa magazeti, Tom Chilala alijitokeza ghafla na kukatiza habari aliyokuwa akisoma mfanyakazi mwenzake, kutoka kwenye gazeti la Mzalendo. Habari hiyo aliyoikatiza,ilihusu namna kesi kati ya Tanesco na Dowans ya hivi majuzi, iliyopelekea kampuni hiyo ya umma kuhukumiwa kulipa Dowans mabilioni ya fedha, ilivyoendeshwa. Kwa yeyote aliyekuwa akifuatilia kipindi hicho, atakubaliana na mimi ya kwamba, kwa namna mtangazaji huyo alivyolazimisha kusitishwa kwa habari husika, bila shaka kuna jambo lililopo kwenye habari hiyo ambalo hakutaka litoke hewani. Swali la kujiuliza ni kwanini? Na je, yeye anahusikaje katika sakata la Dowans,au kawekwa mfukoni na wahusika wenyewe! Naomba yeyote anayeweza kutoa mwanga katika maswali hayo anisaidie.
   
 2. m

  matambo JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  akili zake zitakuwa hamnazo, maana zile sio komenti za mtangazaji mwenzie ila ni taarifa iliyoandikwa gazetini na iliandikwa na gazeti la chama tawala ambayo ni chance kubwa ya kuisoma habari hiyo bila kuogopa kuwa waziri wa habari atakufuatilia, unless yalikuwa matusi

  ijapo mimi hanishangazi sana maana hata akiwa redioni anatangaza mpira huwa anachemka sana

  kama unakumbuka siku ya uchaguzi akaanza kumhoji kikwete kuwa safari iliyopita aliwapa wanawake wengi nafasi vipi safari hii?kikwete alikasirishwa na lile swali akamfokea kuwa watu ndo wametoka kupiga kura matokeo hayajatoka yeye anauliza mambo ya uwaziri na posts, yaani mi mmwenyewe niliboreka
   
Loading...