Tolu Mpya wa Dunia Anatafuta Mchumba

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
</SPAN>


Tolu Mpya wa Dunia, Sultan Kosen akiwa na kaka yake
Thursday, September 17, 2009 5:42 PM
Tolu mpya wa dunia amegunduliwa nchini Uturuki, ana urefu wa mita 2.46 mbali na kuingia kwenye rekodi ya dunia ya mtu mrefu kuliko wote duniani, tolu huyo amevunja rekodi ya kuwa na miguu na mikono mikubwa kuliko watu wote duniani, tolu huyo ametangaza kuwa anatafuta mchumba baada ya kujipatia umaarufu.


Tolu mpya wa dunia toka nchini Uturuki anatafuta mchumba baada ya kujizolea umaarufu duniani na kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness akihesabika kuwa ndiye mtu mrefu kuliko watu wote waliowahi kutokea katika historia ya dunia yetu hii.

Sultan Kosen mwenye umri wa miaka 26, amemwacha kwa mbali jamaa wa China aliyekuwa akishikilia taji hilo, Bao Xishun, ambaye ana urefu mita 2.36 tu.

Kosen ana viganja vikubwa vya mikono kuliko watu wote duniani. Viganja vyake vina ukubwa wa sentimeta 27.5. Miguu yake pia imevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na ukubwa wa sentimeta 36.5.

Kosen alitambulishwa kwa dunia jana jiji London na amesema kuwa umaarufu mpya alioupata duniani utamwezesha kusafiri dunia nzima na kuweza kutengenezewa gari atakaloweza kuingia bila kujikunja kunja.

Sababu ya urefu wa Kosen ni kwamba alikuwa na tezi (uvimbe) kwenye mwili wake ambao uliharibu mfumo wa homoni zake za ukuaji na kumfanya aendelee kukua maisha yake yote, alifanyiwa operesheni na kuondolewa tezi hiyo mwaka jana na hivyo hatarefuka tena zaidi ya hapo.

Kosen alisema kuwa urefu wake ndio uliomsababishia apate tabu kupata mpenzi lakini anaamini kwa umaarufu alioupata sasa atapata mwandani wake. Wiki ijayo anaelekea Marekani kukutana na wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani.

"Ndoto yangu kubwa ni kuweza kuoa na kupata watoto - natafuta mchumba" alisema Kosen.

Chini ni video za tolu wa dunia akitambulishwa jijini London na wakati alipoamua kuingia kwenye mitaa ya jiji la London na kuwashtua watu kwa urefu wake.
 
Back
Top Bottom