Ni kitabu kizuri................ila mbona muda wa kukitoa ni questionable?
Hasa karibu na uchaguzi- ukizingatia hicho hua ndio msingi wa campain
za CHADEMA?
Just an observation! :drum:
Ni kitabu kizuri................ila mbona muda wa kukitoa ni questionable?
Hasa karibu na uchaguzi- ukizingatia hicho hua ndio msingi wa campain
za CHADEMA?
Just an observation! :drum:
Mzee Mwanakijiji umekiondolea udhu Kitabu cha Nyerere
Jamani,
Nimesoma hicho kinachoitwa toleo la Kizazi kipya la Kitabu cha Nyerere cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Kwanza sijui nani amekupa ruhusa ya kukichapisha upya na kuweka maoni yako, ya hovyo! Ungefanya la busara kwa kuchapisha upya, bila ya kuchanganya na maoni yako, ili wasiokuwa na Kitabu hicho wakisome! Kwanza ni kinyume cha taratibu za uchapishaji, pili wewe huna hadhi ya kuweza kumchambua Mwalimu kwa suala alilokuwa analizungumzia, kwani wewe mawazo yako yanaanzia na kuishia kwenye Richmond na Meremeta tu, huna upana wa uchambuzi wa mambo ya Uongozi wa Nchi! Ungekuwa una uwezo huo usingeikimbia njaa ya Tanzania na kwenda kuishi kwa kubangaiza ughaibuni! Taasisi ya Mwalimu Nyerere lazima ikuchukulie hatua kwa kukiondolea tohara Kitabu hicho. Umeweka maoni yako mengi, lakini hukuweka maoni kuhusu Mwalimu Nyerere alimposema waziwazi, kwa jina, Samuel Sitta, Spika wetu wa sasa (Uk. 36 wa chapisho lako, lakini Uk. wa 26 wa Kitabu orijino cha Mwalimu, aya inayohusu Usugu wa Viongozi), wakati huo akiwa Waziri wa Sheria alipojaribu kuliyumbisha Bunge na Chama kuipigania hoja ya Serikali ya Tanganyika iliyokuwa na nia ya kutaka kuuvunja Muungano, iliyomfanya Nyerere ahamaki na kutunga Kitabu hicho! Haishangazi sasa Mhe. Sitta huyu, akiwa Spika, analivuruga Bunge, mpaka Serikali ya Awamu ya Nne inashindwa kutekeleza vizuri Ilani yake ya Uchaguzi! Yeye na wenzake wanaivuruga CCM, mpaka imeundwa Kamati ya Mzee Mwinyi. Haishangazi sasa kwa nini CCJ imeundwa, ikiwa imebana chonjo! Mpendazoe alikwishasema anamsubiri Mhe. Sitta!
Bwassa
Bwassa kama utasoma kwa makini utaelewa kwamba Sitta alikuwa na msimamo aliokuwanao Mwalimu wa kupinga madai ya kuwepo kwa Serikali tatu/kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika."Jukumu la kueleza Taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao, nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki. Mapema nilikuwa nimeambiwa kwamba alikuwa ametamka Bungeni kwamba hapo hoja ya kudai Serikali Tatu itakapoanza kujadiliwa, yeye ataipinga, maana jimbo lake la uchaguzi, Urambo, halikuwa limemtuma kwenda Bungeni kudai Serikali ya Tanganyika. Wabunge wote wakweli wangeweza kusema hivho hivyo. hata Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wangeweza kusema hivyo hivyo. Wao ni wateuliwa na Rais, ambaye alikwisha kwenda Bungeni siku chache tu zilizopita, na kupinga hoja ya Serikali tatu........"
Nakubaliana nawe.Jamani tunauana bila sababu, lazima tuwe pamoja kuweza kujenga nchi yetu. MMKJ ameona yeye mchango wake ni huo na kaufanya sisi tunapiga domo tu hapa, nina uhakika MMKJ ni msomi mzuri anajua pragriarism vizuri kuliko hata sisi wengine hapa hivyo hakuna sababu ya kumtukana na kumuuliza yeye ametoa maoni kwenye kitabu cha mwalimu kama nani. Tusipende kuhodhi hata vitu ambavyo ni kwa ajiri ya maendeleo yetu wenyewe.
Kwa ujumla kama Mwalimu angekuwa anarudi leo hata nguvu ya kutunga kitabu kama hicho asingeipata na angekufa ndani ya dakika moja baada ya kurudi
Jamani tunauana bila sababu, lazima tuwe pamoja kuweza kujenga nchi yetu. MMKJ ameona yeye mchango wake ni huo na kaufanya sisi tunapiga domo tu hapa, nina uhakika MMKJ ni msomi mzuri anajua pragriarism vizuri kuliko hata sisi wengine hapa hivyo ...
Jiongelee wewe.
Hakuna anaejua usomi wa mtu hapa, na kama Mwanakijiji amekwambia wewe kwamba kasoma kutupita mkaribishe chai mkanywe, lakini usituongelee na sisi.
Huyu mwandishi amechukua na kubadilisha maandishi ya mtu kinyume na misingi ya usambazaji vitabu, mawazo na maneno ya mtu mwingine, na akaweka alama za jina lake, ameiba.
Ukisoma "toleo la pili" huwezi jua mstari wa Nyerere unaishia wapi na chombezo za M.M.M. zinaanzia wapi maana amepanga aya upya na kufanya uhariri wake kuchanganya msomaji.
Anasema kwenye utangulizi kwamba amefanya hivyo kurahisisha maandishi ya Nyerere yaeleweke, lakini kwenye utangulizi kasema:
kukiri kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo magumu yaeleweke kwa urahisi na masuala mazito yafahamike hata kwa mtu wa kawaida kabisa. Hivyo kijitabu hiki si kigumu kukielewa na wala si cha kifalsafa sana kama vitabu vyake vingine."
Sasa kama kitabu si kigumu, kwa nini atusaidie kukielewa kwa kuchombeza chombeza chumvi zako? Huyo mwandishi mwizi ndio unamwimbia chereko kwamba amesoma kutupita?
Hivi kwani Mwanakijiji keshachapisha kitabu hicho au ni majadiliano ya kwenye JF?...
Kama Mwanakijiji kachapisha bila kufuata utaratibu unaohitajika aelezewe tu utaratibu ukoje. Sidhani kwamba hilo ni jambo ambalo haliwezi kurekebishika ili kutoa fursa ya yaliyomo kwenye kitabu hicho kujadiliwa.
"Mamlaka kwenye masuala ya uandishi haimaanishi "ruksa," madaraka, nguvu ya kuchapisha kitabu, bali karii, au utaalam ulioiva unaokubalika katika ulingo wa fani fulani. Unapoandika kitabu chochote unategemewa uwe na karii ya kuwachambulia wenzako swala fulani. Isipokuwa kama unaandika tamthilia kama za sungura, fisi na mapenzi.Mamlaka ya kuchambua mawazo ya Mwalimu maana yake nini? ... siri ambazo zinahitaji 'mamlaka' na ruksa ya kuchambua
Sawa Bibi Ntilie. Tujadili kitabu. Haya, tunajadili kipi?
Tunajadili kitabu na mawazo ya Mwanakijiji au kitabu na mawazo ya Mwalimu?
"Mamlaka kwenye masuala ya uandishi haimaanishi "ruksa," madaraka, nguvu ya kuchapisha kitabu, bali karii, au utaalam ulioiva unaokubalika katika ulingo wa fani fulani. Unapoandika kitabu chochote unategemewa uwe na karii ya kuwachambulia wenzako swala fulani. Isipokuwa kama unaandika tamthilia kama za sungura, fisi na mapenzi.
Tindikali,
Asante kwa darasa. Naamini tunachozungumzia ni kujadili kitabu na mawazo ya Mwalimu si ya Mwanakijiji na wala si kuhusu utaalamu wa karii unaouzungumzia. Mwananchi yeyote yule anao uhuru wa kujadili mawazo ya Mwalimu. Pia, naamini kwa dhati kabisa kuwa Mwalimu hakuandika kitabu kile akitaka watakaojaribu kujadili yaliyoandikwa mle lazima wawe na utaalamu unaouzingumzia au wawe wanamjua vyema Mwalimu. Mara nyingi Mwalimu alikuwa akiandika hotuba zake na vitabu kama hiki tunachokizungumzia kwa lugha nyepesi ili wananchi wote wasomi na wasio wasomi waweze kupata ujumbe aliotarajia kuufikisha.
Narudia kusisitiza kwamba naamini kwa dhati kabisa kwamba Mwalimu hakuandika kitabu hicho ama maandiko yake yoyote yale akidhamiria huko mbele iwepo "mamlaka" ya aina yoyote ile itakayosababisha wananchi hata wale mbumbumbu wasiweze kujadili kuhusu aliyowahi kusema ama kuandika. Mwalimu hakuandika kitabu kile kwa ajili ya hao weledi wa siasa na historia kuja kukichambua aliandika kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania waelewe na kuzingatia kuhusu Hatma ya nchi yao.
Eti toleo la pili la kitabu cha Nyerere, Nyerere mwenyewe keshafariki, umepoteza goroli?
Mkuu Bibi Ntilie, asante sana kwa msimamo wako.
Mimi naomba niendelee kukijadili kitabu hiki. Wala sina nia sana ya kumtetea mleta hoja!
Inavyoonekana Mwalimu aliandika kitabu hiki aya moja moja akiwa na hasira kila baada ya kukutana na wakuu wa nchi kwenye mikutano yao ya aina mbali mabali ikiwemo ya faragha, wakati wa chai ya jioni na hata wakipata chui baridi,, (mtu asidakie hapa akaanza kudai nimesema Mwalimu alikuwa anapata chui tafadhali!)
Amesema wazi kwenye baadhi ya aya za kitabu hiki. Mwalimu ameandika hiki kitabu siyo kwa furaha hata kidogo, wala hakukiandika kwa ustadi sana. Inaonekana wazi alikuwa anataka aongee na wajukuu zake walioko nchi nzima. Mtanzania na mzalendo kutokijadili kitabu hiki ni kosa kubwa maana yeye ndivyo haswa alivyolenga. Nia ya mtoa hoja ni sawia na sambamba kabisa na ile ya mwalimu. Hata kama ningewekewa tindi kali kiasi gani mbele yangu nigelilitia maji mengi ili nisomapo mjadala wake ziwemo bado za kunitosha kuuelewa kuliko nig'aake ng'aake ovyo. Wallaahi ndivyo ningefanya!
Mwanakijiji hebu waandikie ule mfuko wa Mwalimu waombe kuwa tunahitaji kukichapisha na kukiuza faida inarudi kwenye mfuko huo huo! Tafadhali fanya hima Mkuu!
Asante MpendaTz,
Naomba nijihami kwa kusema kwamba utetezi wangu kwa mtoa hoja unatokana na sababu moja tu kwamba amesome kitabu/vitabu vilivyoandikwa na Mwalimu na ameona vina umuhimu wa aina yake na vinahitaji kusomwa na wengi na inapowezekana yaliyoandikwa yajadiliwe na kuzingatiwa. Simjui Mwanakijiji na hanijui zaidi ya kuwa tumo humu JF.
Nakubaliana nawe kwamba ni dhahiri yaliyojiri wakati ule yalimchefua Mwalimu kiasi cha kuamua kuandika kitabu hicho kutokana na matukio moja baada ya jingine. Moja lililowazi katika kitabu kile ni kwamba Mwalimu alijali zaidi mustakabali wa Taifa na jinsi ambavyo uongozi unahitajika kuwa makini katika kushughulikia masuala ya msingi ya kitaifa.
Pamoja na ushauri mzuri kwa Mwanakijiji, ningeongezea pia kwamba si vibaya akajaribu pia kuwatafuta viongozi wa Taasisi ili waweze kubadilishana mawazo kuhusu lolote linalomuhusu Mwalimu. Mzee Butiku alikuwa Private Secretary wa Mwalimu kwa miaka mingi tangu mara baada ya Uhuru hadi anang'atuka urais kwa hiyo yeye anamuelewa Mwalimu na mawazo yake kwa usahihi usio na shaka. Namba za Taasisi ziko kwenye Website yao www.nyererefoundation.co.tz kama sikosei.
Najua mkuu! Ila binafsi niko serious na nina sababu!