Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,531
- 22,473
Kamusi ya kiingereza inayotolewa na Oxford University Press ya nchini Uingereza iitwayo Oxford English Dictionary, mwezi huu wa June imeingiza neno "Tweet" ambalo linamaanisha kutuma ujumbe kwenda twitter.
Kwenye kamusi hiyo neno Tweet linasemwa kwa kiingereza -"to send message on twitter". Ingawa neno tweet lipo katika kamusi hiyo likimaanisha wimbo wa ndege mdogo aina ya mbayuwayu, sasa limeingizwa rasmi katika kamusi hiyo iliyoanza kuuzwa mapema mwezi huu.
Mtandao wa twitter umekuwa ni maarufu duniani ukivutia watu wa rika zote na kufanya lugha ya kiingereza kukubali neno la twitter kama NOMINO na tweet kama KIARIFU hivyo kufanya maneno hayo kutambulika katika lugha ya kiingereza. Pia neno retweet limo katika kamusi hiyo likimaanisha kubadilishana ujumbe au kwa kiingereza -"sharing anothers tweet".
Katika kile kinachoonekana kwenda na wakati na teknolojia, kamusi hiyo pia imeingiza maneno mengine yanayohusiana na teknolojia ambayo ni "big data", crowdsourcing, e-reader, mouseover, redirect (the noun) au NOMINO na stream the VERB au KITENZI.
Neno "crowdsourcing" ni neno linalomaanisha kitendo cha kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa watu tofauti kwa njia ya mahojiano ya simu au ana kwa ana lakini kwa minajili ya kutengeneza habari kamili. Njia hii inatumika sana kwenye mataifa yaliyoendelea kwa kuwepo ajira kamili ambapo mtafutaji anaitwa telephone researcher au marketer na kitendo chenyewe -"telephone marketing".
Mbayuwayu
Pia kuna neno moja la mtaani au misimu au kwa kiingereza "Slang", linalosemwa huko nchini Marekani kwa kiingereza "to have a cow" ambalo linamaanisha kwa kiingereza "to have a fit" likimaanisha kwa kiswahili kwamba mtu amekasirika au amekasirishwa na jambo fulani kiasi cha kutaka kuchukua hatua fulani na neo hili anatumia sana yule jamaa aitwae Bart kwenye tamthiria za Simpsons.
Twitter ni huduma itolewayo kwenye mtandao wa internet inayowawezeha watumiaji wa jamii mbalimbali kwasiliana kwa kutumiana na kusoma ujumbe mfupi au tweets mpaka maneno yafikiayo 140 kwa wakati mmoja.
Alama maalum ya Twitter
Nimeona si mbaya kuweka habari hii hapa baada ya kupita katika duka moja kubwa la vitabu hapa ughaibuni ambalo linauza vitabu vya aina zote. Duka hilo liitwalo Waterstones ndilo duka kubwa kabisa la vitabu nchini Uingereza na lina matawi katika karibu miji yote mikubwa nchini humo.
Je kuna maneno yapi mapya ambayo yamejitokeza katika kipindi cha miezi sita iliyopita nchini mwetu Tanzania ningependa kuyapata hapa.