Tokeni kati yao mkajitenge nao nayo nuru yenu ipate kuangaza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tokeni kati yao mkajitenge nao nayo nuru yenu ipate kuangaza!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ame, Sep 13, 2012.

 1. A

  Ame JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwa muda wa zaidi ya Muongo mmoja sasa tumekuwa tukisikia watanzania takribani wote wakilia kwa sauti moja na ya uchungu kuwa adui yao mkubwa ni ufisadi. Nami natoa wito kwa wote wenye kuelewa na kujitambua kwamba ufisadi ndiyo common adui yetu mkubwa watoke katika nchi hii ya baba zao (Uongozi ulio zaa ufisadi) ambamo ufisadi ni order of the day. M4C inatupatia hii platform yasafari ya kuiendea nchi ya ahadi kwani wale wenzetu wa upande wapili naonamagamba yamekataa kuvuka.

  Kwa wale wanaomini uumbaji basi ni kanuni ya asili ama kiingereza nature (ki-ungu) baraka na laana haziwezi kukaa nyumba moja ni either uamue kukaa na laana ku suffer the consequences ama uamue kuvunja laanauweze kufurahia baraka. Pia mwanga na giza haviwezi ku-co-exist. Kwa maana hiyo ukiamua kuwa mwanga lazima gizauliondoe ama ukiwa hutaki mwanga basi unazima taa ili giza litamalaki (Ndivyowalivyo fanya ndugu zetu kwa kuruhusu magamba kubaki katika nyumba yao).

  Hivi Ndivyo ilivyo kwa wote wenye kupenda mabadiliko chanya kwa maana ya kuuondoa ufisadi ambao mwasisi wa wake ni chama na serikali iliyopo madarakani hasa kwakua haijakaa kutokea kuwepo chama ama serikali nyingine iliyoitawala hii nchi kuacha ile ya kikoloni tangu kuumbwa kwa dunia.Hii inaonyesha dhahiri kuwa kama ufisadi ulizaliwa katika nchi hii basi baba namama yake ni serikali inayoongozwa na chama ambacho ndicho kiko madarakani tangu enzi za uhuru ambao ndiyo mwanzo wa maisha ya nchii hii baaada ya wakatiwa ukoloni.

  Maisha yetu wanadamu yana ongozwa na utashi nakila aliye mwanadamu tofauti na mnyama anautashi na huo umempatia bure uwezo wakuchagua maisha anayotaka kuishi ya giza ama mwanga. Kwa sababu hiyo kama ufisaditunaufananisha na giza ama laana basi ni hakika kabisa mbuzi hawezi zaa ng'ombena hivyo basi kama ufisadi ni mtoto au tunda la uongozi wetu tangu uhuru basi ni hakika kabisa asiliya mtoto inafanana na wazazi wake. Tutategemea muujiza kama baba ataamua kumuamtoto wake na hii ndiyo tuliyoishuhudia baada ya magamba kushindwa kuvuka kudhihirisha ufisadi ni mtoto halali wa chama na serikali iliyopo madarakanikwa miaka 50. Nasi tunao uchaguzi wa ama kuishi katika laana na giza ama kuwasha taa na kufanya giza litokomee.

  Ni kwa sababu hiyo mimi nimeamua kuwasha taa nakuwa muumini wa M4C nakukaribisha na wewe ndugu ambaye hupendi kukaa gizani.

  Welcome to the world of light....M4C!
   
 2. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Bado mda wangu wa kazi haujaisha ntarudi baadae
   
 3. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Amen mtumishi!
   
 4. K

  KINUKAMORI Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm ianze kutafutiwa sanda
   
Loading...