Tokea lini Kikwete kuomba kura za wapemba ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tokea lini Kikwete kuomba kura za wapemba ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Oct 17, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  MAKAMO Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Bw. Machano Khamis Ali, amesema kuwa ameshangazwa na kauli ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya ya Mrisho Kikwete ya kuwaomba wananchi wa Kisiwa cha Pemba wawape kura ili kuijaribu CCM.
  Hayo ameyaeleza jana katika uzinduzi wa Kadi za Uwanachama wa Vijana wa CUF uliofanyika katika Ukumbi wa Jamatkhan mjini hapa.
  Rais Kikwete juzi alikuwa katika mkutano wa Kampeni Kisiwani Pemba, ambapo aliwataka wananchi wa kisiwa hicho kuipigia kura CCM kwa kuijaribu ili iweze kuwaletea maendeleo zaidi ndani ya kisiwa hicho.
  Bw. Machano alisema kwamba hakusudii kumjibu Rais Kikwete lakini inaonekana dhahiri kwamba hajui anachokizungumza katika mikutano yake ya kampeni na kusahau kuwa chama chake kimeshaongoza kwa takriban miaka 33 sasa bila ya kuwanufaisha wananchi.
  “Sikusudii kumjibu rais bali nawaambia vijana ili muweze kulifahamiu hilo”, alisema.
  Ailfahamisha kwamba kutokana na hali hiyo ameifananisha CCM sawa na kikwete kutokana na kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake tangu kukaa madarakani.
  “Kama kweli CCM inatimiza miaka 33 bado unataka kujaribiwa haiwezekani, vijana kuweni macho”, alieleza na kuongeza kuwa imekuwa ni sawa na kiwete kw akushindwa kutembea.
  Hivyo aliwataka vijana hao kujaribu kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, na kuhakikisha kwamba wanakipatia ushindi chama cha CUF ili kiwaletee maendeleo ya kweli.
  Alisema kwamba kama wanavyojuwa kwmba chama chao kinawtegemea wao katika kufanikisha suala hilo, hivyo ni wajibu wao kufanya utundu ili kuiendeleza Jumuiya yao kwa lengo la kukiendeleza chama chao.
  Nae Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Taifa Bw. Khalifa Abdallah Ali, amewaahidi viongozi wa chama hicho kwamba vijana watafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha chama hicho wanakiingiza madarakani.
  “Tutatumia muda wetu wote, hakuna kulala mpaka tukiingize chama chetu madarakani, ili kuwakomboa vijana wetu pamoja na watanzania kwa ujumla”, alisema.
  Alisema kwamba vijana hivi sasa wamekuwa hawana tofauti na wazee, kutokana na madhila wanayoyapata kutoka kwa CCM.
  “Hivi sasa vijana sote tuemkonga hatujuulikani wazee wala vijana sote tupo rika moja kwa shida za CCM, tumechoka tunataka mabadiliko”, alisema.
  ALUTA KONTINUA..Viva CUF :yield:
   
Loading...