Toka vita ya vietnam mpaka rais kujiuzulu kwenye mission impossible....watergate scandal

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2017
Messages
1,251
Points
2,000

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2017
1,251 2,000
Nianze kwa kusema hii ni mara yangu ya kwanza kuandika kwenye hili jukwaa la wana intelligence.Ila ningependa kushare na ninyi kuhusiana na mission impossible ya Watergate scandal.

Kutokana na sintofahamu iliyokuwa imeenea nchini Marekani kutokana na watu wengi kutokuona umuhimu wa vita ya vietnam.Katibu wa idara ya ulinzi marekani Robert .s. Mcnamara, mwaka 1967 aliagiza kufanyika uchunguzi kuangalia historia ya vita na kuangalia wapi,uhusika wa marekani na matokeo yake kwenye vita.kamati ya uchunguzi iliundwa chini ya Leslie .H. Gelb aliyekuwa kiongozi wa kitengo ya kupanga sera juu ya masuala ya ulinzi kimataifa ndani ya idara ya ulinzi.Uchunguzi huu ulitakiwa ufanyike ili kutengeneza mwongozo wa kihistoria miaka ijayo kwenye idara hiyo, hivyo haukutakiwa kutolewa mbele ya umma wa marekani ila iwe ni siri ya idara hiyo ya ulinzi.Kamati hiyo ilihusisha wanahistoria na wataalam wa mambo ya usalama na kazi hiyo ilikamilika mwaka 1969 mwezi January ikitoa ripoti yenye kurasa 7000.


Mojawapo ya watu ambao walishiriki alikuwa msomi aliyekuwa ameshiriki masuala mbalimbali ya kiusalama hasa vita ya vietnam Daniel Ellsberg lakini aligeuka kuwa mwanaharakat aliyepinga sana vita ya vietnam.Mwaka 1971 mwezi march Huyu alitoa kopi ripoti nzima nakumpa mhariri wa gazeti la Washington post aliyejulikana kama Neil Sheehan naye akaitoa kwenye kurasa za mbele ya gazeti hivyo ripoti haikuwa siri tena!.Ripoti hii ilibainisha masuala mbalimbali ambayo wamarekani walidanganywa na viongozi wa nchi yao tokea mwaka 1955 kipindi cha rais Harry Truman mpaka 1970's kipindi cha Richard Nixon.Ilionesha wazi ambavyo Marekani ilihusika kwenye chokochoko zilizoanzisha vita hivyo,Marekani kuongeza kufanya mashambulizi kwenye maeneo hadi ambayo hayakuwahi kutangazwa kwenye vyombo vikuu ya habari nk.Hii ripoti ilizua malalamiko miongoni mwa wamarekani na ilikuwa tishio kwenye ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Richard Nixon wa republican dhidi ya wapinzani wake wa democratic uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwaka 1972 hivyo kuna jambo lilitakiwa kufanyika ili kuokoa jahazi.

Miongoni mwa watu waliokuwa wanazi wa rais Richard Nixon na waliokuwa karibu nae mwaka huohuo 1971 walikutana ili kupanga jinsi ya kutatua tatizo lililoletwa na ripoti Ile ndani ya Jamii ya wamarekani.watu hao ni bwana Howard Hunt aliyewahi kuwa agent wa C.I.A aliyeshiriki oparesheni kadhaa za C.I.A ikiwemo "bay of pigs", Gordon Liddy aliyewahi kuwa agent wa F.B.I na David .R. Young Jr ambaye inasemekana alimwakilisha rais.Katika kikao hicho wote walikubaliana na ushauri wa Howard Hunt kwamba wafanye oparesheni ya siri kwa lugha ya wenzetu "covert operation".kwa ufupi covert operation ni oparesheni inayofanywa na vyombo vya usalama kwa siri, malengo yake,watu walioiandaa na watu walioidhamini hayatakiwi kujulikana.hivyo walikubaliana oparesheni hiyo ifanyike katika ofisi ya Dr Lewis Fielding ambaye alikuwa daktari wa masuala ya afya ya akili wa Daniel Ellsberg ili wapate taarifa mhimu kuhusu afya yake ya kiakili ili waweze kumpaka matope "kumpakazia" kwa wamarekani kwamba hawezi kuaminika.

Toka rais wa Cuba Fidel Castro aingie madarakani kuna raia wa Cuba wengi walikimbilia Marekani kutokana na za kijamaa ambazo rais Castro alizianzisha Cuba.Hawa watu walikuwa msitari wa mbele kumpinga rais Fidel Castro.Miongoni mwao ni Eugenio Martinez ambaye alishirikiana na C.I.A katika oparesheni zaidi ya 350 nchini Cuba jamaa huyu aliishi Miami.Mojawapo ya oparesheni aliyoshiriki ilikuwa ni bay of pigs.Kipindi wakiwa wanafanya oparesheni hiyo kuna jina alikuwa akilisikia sana nalo ni Eduardo.Mtu huyu aliwahi kuwaandikia barua wacuba kupitia kwa mojawapo wa viongozi wao aliyeitwa Bernard Barker akiwapa pole kwa kushindwa kwenye oparesheni ya bay of pigs na akimulaumu rais wa Marekani aliyekuwepo madarakani kipindi cha oparesheni hiyo John Kennedy kwa kutoa support ndogo.

Siku moja Barker alimwambia akutane na Eduardo katika jumba la makumbusho ya bay of pigs tarehe 16 April 1971 katika kumbukumbu ya miaka kumi ya tukio hilo.siku ilipofika alikutana nae na akapata nafasi ya kumuona na kulijua jina halisi la huyo Eduardo ambalo ni Howard Hunt.Katika maongezi yao Howard Hunt alimshauri aache kuandaa oparesheni nyingine kupeleka Cuba badala yake atafute uraia wa Marekani ili ampatie kazi fulani ya kufanya.Baada ya siku kadhaa kupita Horward hunt alimwambia Barker kuwa yupo ikulu na ni mshauri wa rais na akamwambia kuna kazi inayohusu ulinzi kuhusu wasaliti wa taifa la Marekani ambao wametoa nyarakaza siri za nchi kwenye ubalozi wa Urusi.Hivyo Barker na Martinez walitakiwa kuwa mojawapo ya wahusika wa hiyo kazi lakini akamwambia Barker atafute mtu mwingine wakamtafuta Filipe De Diego.

Kwa upande wa martinez ilikuwa heshima kubwa kushiriki katika oparesheni hiyo baada ya wiki mbili waliambiwa na Hunt wachukue nguo za siku tatu na kazi ianze.siku iliyofuata walipanda ndege kwenda Los Angeles walipofika walifikia hoteli ya Barvely hills wakakutana katika chumba cha Hunt kwa Ajili ya utangulizi kuhusu oparesheni yenyewe.Lakini utangulizi huu haukuwa na chochote na haukupangiliwa.

Katika oparesheni nyingi za kijasusi katika utangulizi anayehusika anatakiwa apewe taarifa mhimu na anatakiwa kufanya majaribio katika mazingira yanayofanana na yaleyale ili kama utekelezaji utakuwa mgumu watafute njia nyingine.lakini utangulizi huu ulikuwa na tofauti walichoambiwa ni kuingia katika ofisi fulani na kupiga picha taarifa za afya ya akili za msaliti waliyeambiwa jina lake ni Daniel Ellsberg na Martinez alichaguliwa kupiga picha.Wote walitakiwa kuvaa kama wafanyakazi wa pale na kusubiri mda ambao Dr Fielding atatoka ofisini kisha waweke vifaa vya kuchukua picha kisha wapitie Mlango wa nyuma wamsubiri hadi mfanyakazi wa usafi amalize baada ya hapo warudi wamalizie oparesheni usiku.Walifanya kama ilivyo ila cha ajabu tangia mwanamke wa usafi aingie hawakumuona ametoka walimsubiri mda mrefu hadi wakahisi ameshatoka wakaamua kwenda kuingia lakini wakakuta milango imefungwa.lakini kuna mtu mwingine waliyekuwa nae Bwana Gordon Liddy akawaambia wavunje dirisha.baada ya kumaliza waliingia ofisini hawakukuta taarifa ya yoyote iliyohusiana na Daniel Ellsberg zaidi ya namba yake ya simu katika phonebook ya Dr Fielding.Baada ya kumaliza Martinez alichukua vidonge vya vitamin C alivyovikuta kwenye briefcase moja ili awalaghai kama waliingia waathirika ya madawa ya kulevya na walikuwa wanatafuta humo ndani madawa hayo.baada ya kumaliza waliondoka wakarudi hotelini wakidhani wamefeli kwenye oparesheni kwa kukoswa taarifa yoyote lakini Hunt aliwapongeza sana akawaambia wameanza vizuri wajiandae kwa kazi nyingine.

Kwa leo nikomee hapa nitaendelea siku nyingine kuhusiana na tukio lililofuata la Watergate lilivyotokea na lilivyopelekea rais Nixon kujiudhuru na kubadili historia ya marekani.
THANKS

**Sehemu ya pili: Toka vita ya vietnam mpaka rais kujiuzulu kwenye mission impossible....Watergate scandal(2)
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,381,479
Members 526,110
Posts 33,801,696
Top