Toka Singida: Dr. Kitila Mkumbo apandishwa mahakamani rasmi...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo na madiwani wawili, wametiwa mbaroni wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Wakati Dk Mkumbo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, akituhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigullu Nchemba, Diwani wa Kata ya Mabogini Wilaya ya Moshi, Albert Msando na Alex Umbella wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, wamehojiwa na polisi kwa makosa ya jinai.

Dk Mkumbo amepandishwa kizimbani jana akiunganishwa katika kesi inayomkabili Ofisa wa Sera na Utafiti wa chama hicho kikuu cha upinzani, Mwita Waitara Mwikwabe (37).

Mwanasheria wa Serikali, Maria Mudulugu alidai mbele ya Hakimu Ruth Massamu kuwa, Julai 14 mwaka huu saa 10.00 jioni, mshtakiwa Dk Mkumbo alitoa lugha ya matusi dhidi ya mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Mwanasheria aliiambia mahakama kuwa, Dk Mkumbo alitamka kuwa mbunge huyo ni malaya, mzinzi na ni 'the comedy' (msanii), huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mwansheria Mudulugu alisema kuwa mshtakiwa alitoa lugha hiyo ya matusi kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika katika viwanja vya kituo cha mabasi cha Kijiji cha Nguvumali Kata ya Ndago, Jimbo la Iramba Magharibi.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na yupo nje baada ya kudhaminiwa wa watu wawili. Kesi hiyo itatajwa tena Julai 30 mwaka huu.

Wakati huo huo, vijana wawili wakazi wa Kata ya Ndago, Paulo Nashakigwa (27) na Emmanuel Shilla (24) wamepandishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakituhumiwa kushiriki kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Yohana Mpinga (30).

Mudulugu alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa Julai 14 mwaka huu, majira ya alasiri wakiwa katika Kijiji cha Nguvumali Kata ya Ndago wote kwa pamoja wakitumia fimbo na mawe, walimpiga Yohana na kusababisha afariki dunia.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Washtakiwa hao wameunganishwa na wenzao 12 ambao wamesomewa shtaka hilo la mauaji Julai 16 mwaka huu. Kesi hiyo itatajwa tena Julai 30 mwaka huu.
 
Walirekodi hayo matusi?ndo politics hizo za bongo,nadhani atapigwa faini,(kama ni kweli),hakuna la ziada.
 
Namkubali sana Dr Kitila Mkumbo ila akianza kujiingiza kwenye siasa tu.
Hatokuwa tofauti na Lyatingo Mremu.Just wait and see.
 
Hivi ndugu yetu lusinde alipandishwa mahakamani kwa kusema maneno makali zaidi ya hayo??

Hivi mwigulu sio malaya??? kusema ukweli ni kosa?? mbona tunamwita Komba msanii kuna kosa gani

Vipi chi hii?
 
Hivi ndugu yetu lusinde alipandishwa mahakamani kwa kusema maneno makali zaidi ya hayo??

Hivi mwigulu sio malaya??? kusema ukweli ni kosa?? mbona tunamwita Komba msanii kuna kosa gani

Vipi chi hii?

Mkuu TIMING Polisi magamba na mahakama magamba wanaweza kufanya lolote lile katika juhudi zao za kupunguza au kusimamisha kabisa speed ya CHADEMA katika kuiteka nchi katika uchaguzi ujao wa 2015.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu TIMING Polisi magamba na mahakama magamba wanaweza kufanya lolote lile katika juhudi zao za kupunguza au kusimamisha kabisa speed ya CHADEMA katika kuiteka nchi katika uchaguzi ujao wa 2015.
it is too late my brother.... wanchofanya ni kuongeza chuki tu na wananchi
 
it is too late my brother.... wanchofanya ni kuongeza chuki tu na wananchi

Ni kweli kabisa, mfa maji haishi kutapatapa. Chuki wanayojaribu kuijenga miongoni mwa Watanzania inaweza kabisa kuongeza kwa kiwango kikubwa umwagaji mkubwa wa damu nchini.
 
Walirekodi hayo matusi?ndo politics hizo za bongo,nadhani atapigwa faini,(kama ni kweli),hakuna la ziada.

ndio mnavyojidanganya, hapo ni jela inamuita ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kuropoka kama huyu
 
Mkuu TIMING Polisi magamba na mahakama magamba wanaweza kufanya lolote lile katika juhudi zao za kupunguza au kusimamisha kabisa speed ya CHADEMA katika kuiteka nchi katika uchaguzi ujao wa 2015.

sasa muiache mahakama ifanye kazi yake
 
Last edited by a moderator:
ndio mnavyojidanganya, hapo ni jela inamuita ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kuropoka kama huyu

naona vipuri vimeshweka nanihino ready

india.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
it is too late my brother.... wanchofanya ni kuongeza chuki tu na wananchi

Unayosema mkuu ni sahihikabisa, watu sasa hivi wameicho CCM na wanafatilia mambo huwezi kuamini...leo nikuwa nimekaa sehemu kuna wamama waka wanaongea kuhusu barabara za Arusha kujengwa kwa kiwango cha rami....kauli niliyoisikia kutoka kwa kina mama hao ilinifanya niamini kuwa watu kweli wame ichoka CCM walisema..." wameona Chadema inalichukua jiji ndiyo wanaanza kutujengea rami, hata watujengee rami mpaka choo chdema itachukua nchi tu..."
 
ndio mnavyojidanganya, hapo ni jela inamuita ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kuropoka kama huyu

Kwani atakuwa mfungwa wa kwanza, magereza hatuiongopi ndiyo maana kuna watu wengine walienda kuwathibitishia hilo...CCM wapumbavu sana mnatutishea mahakama na polisi siku sinyingi watakuwa wana tulinda sisi...
 
Kazi ipi, kuna mwanasiasa alie wahi kutukana kama huyu pumbavu.

je serikali ilimshitaki au polisi sikuhiyo hawa kuwepo...

kuna kati ya hawa waliotukanwa aliyeenda kushtaki na hakutendewa haki?... Acheni kulalamika tu bila kuchukua hatua
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom