JULIUS KBARAGE NYERERE
Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa katiba tuliyo nayo ni mbaya kwa sababu inamfanya Rais kuwa Mungu mtu. Akaonya pia kuwa siku akitokea Rais mbaya, nchi itajuta kwa sababu hakuna atakayemzuia kufanya chochote kwa sababu katiba inampa Rais mamlaka yasiyo na mipaka. Miaka 30 baadaye imekuja kudhihirika.
Tafakuri: Mwalimu alijua kuwa katiba ni mbaya. Alijua kuwa katiba mbaya italitesa Taifa. Kwa nini kipindi chote cha utawala wake hakufanya jitihada za kuibadilisha hii katiba mbaya tuliyo nayo?
ALI HASSAN MWINYI
Akaja Rais Mwinyi. Mwinyi, katika kitabu cha maisha yake anasema wazi kuwa Mwalimu alitaka mgombea binafsi aruhusiwe, na vyama viruhusiwe kuungana, lakini Kamati kuu ya CCM licha ya kuona uzuri wa kuwa na mgombea binafsi, na uzuri wa kuruhusu vyama kuungana, ilikataa kwa kuhofia kuwa mambo hayo yakiruhusiwa, CCM ingeweza kupoteza madaraka kiurahisi.
Tafakuri: Mwinyi alijua hila za CCM, na umuhimu wa kuwa na demokrasia halisi kuliko hii ya kiinimacho tuliyo nayo, kwa nini katika kipindi chake cha utawala cha miaka 10, hakufanya jitihada ya kuibadilisha hii katiba mbaya tuliyo nayo?
BENJIMIN WILLIAM MKAPA
Rais Mkapa, alijua uovu mbalimbali unaolindwa na katiba. Kwenye kitabu chake cha maisha yake, Mkapa alidai kuwa angependa kuiona Tanzania yenye Tume huru ya uchaguzi. Ina maana anajua fika kuwa Tume ya uchaguzi tuliyo nayo siyo huru.
Tafakuri:
Kwa nini Rais Benjamin Mkapa hakufanya jitihada za kuwa na katiba mpya akiwa madarakani?
JAKAYA KIKWETE
Jakaya Kikwete alijua fika unafiki na siasa za hila za CCM za kutozingatia maslahi ya Taifa kwanza, alijitahidi akaanzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Lakini baadaye, hata huo mchakato ukaonekana ni kiinimacho.
Tafakuri:
Ni kweli, Kikwete aliingia kwenye mgogoro mkubwa na CCM, ambayo miaka yote imezoea kuendesha mambo kwa hila na ulaghai, lakini kwa nini hakuuvaa ujasiri ili asimame na Taifa kuliko kusimama na chama ambacho daima kimekuwa na nia ovu?
JOHN POMBE MAGUFULI
Huyu hakuwa na cha kujutia. Labda Mungu angemruhusu amalize uongozi wake, baada ya kutoka kwenye madaraka, huenda naye angeongelea ubaya wa katiba tuliyo nayo, kama walivyofanya wenzake.
Rais Magufuli, ni kama ndiye aliyetabiriwa na Mwalimu. Maana kipindi chake, mambo ya ajabu aliyatenda, hata bila ya kuzingatia sheria, kanuni, na katiba ya nchi. Alifanya alivyotaka, na aliyenyanyuka kutaka kuhoji, kama aliishi, alikiona cha mtemakuni.
Tafakuri:
Hata baada ya kuumizwa vikali na utawala wa awamu ya tano, hatujapata funzo bado?
SAMIA SULUHU HASSAN
Tangu aingie madarakani amekuwa akiongelea na kufanya mabadiliko ambayo tafsiri yake ni kuwa utawala uliopita ulionea watu, ulipora hela za watu wa nguvu, uliwadhulumu watu haki za kidemokrasia, uhuru wa maoni na kuwabagua.
Tafakuri:
Kama Rais Samia ana dhamira ya dhati, kwa nini asiende kwenye kiini cha tatizo ili matatizo tuliyoyashudia kwa muda mrefu yaondoke, na yasirudi tena?
Ukitafakari kwa umakini, kizuizi kikubwa cha ustawi wa Taifa letu ni CCM.
Polisi wanashindwa kufanya kazi kwa weledi na kwa haki kwa sababu ya CCM. CCM mara kadhaa imetumia jeshi la Polisi kuwakandamiza, kuwakomoa au hata kuwaangamiza wapinzani wao wa kisiasa.
Idara ya usalama wa Taifa inashindwa kufanya kazi kwa welwdi kwa sababu ya CCM. CCM ndio wanaoifanya taasisi hii muhimu kwa Taifa iache mambo muhimu yenye maslahi kwa Taifa, na kujishughulisha zaidi na siasa, na hasa kutumika na CCM dhidi ya wapinzani.
Mahakama nayo imepoteza weledi. Majaji una nyakati wamerumika kulinda maslahi ya CCM badala ua maslahi ya Taifa na haki za wananchi.
Bunge limekuwa kama idara ya chama. Bunge limekuwa pahali pa kupiga porojo na vijembe dhidi ya wapinzani, huku wanaofanywa hivyo wakilindwa kwa nguvu zote na spika. Marehemu Magufuli aliwahi kumwagiza spika, kwa uwazi kabisa, mbele ya umma, kuwa awafukuze wabunge ndani ya bunge ili wakitoka nje, yeye aweze kuwashugulikia. Agizo hilo spika alilitekeleza vizuri sana, na wabunge wa uoinzani walionja shubiri kwa kiwango kisichoweza kupimika.
Kwa ujumla CCM haina hata chembe ya huruma kwa wananchi wala Taifa. Kipaumbele chake ni kuhakikisha inabaki madarakani iwe kwa haki au dhuluma, iwe kwa amani au shari, iwe kwa uhai au mauaji.
CCM inaogopwa na Polisi, TISS, mahakama na Bunge. CCM inaogopwa na marais.
Wananchi wasipojitegemea wenyewe, wakasimama kwa dhati na ujasiri wa kuamua kupata katiba mpya, kwa manufaa ya Taifa, wasitegemee kama itapatikana kwa mapenzi ya CCM au Rais aliyopo madarakani. Kipingamizi kikubwa cha kuyapata maendeleo ya kweli kwa Taifa letu, ni katiba yetu mbovu. Na kipingamizi kikubwa cha kupata katiba nzuri inayoweza kulifaa Taifa letu, wakati wote, imekuwa ni CCM na Rais ambaye yupo madarakani.
Samia hata awe na dhamira njema kiasi gani kwa Taifa, bila ya katiba nzuri mpya, hawezi kufanikiwa, na hata akitaka kuwepo na katiba mpya, hatafanikiwa kuishinda CCM iliyotopea kwenye siasa ovu bila ya kujitoa mhanga wa kujitenga na uovu wa CCM, na kusimama na umma wa haki kwa manufaa ya Taifa.
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli na sasa Samia, ukitazama juu juu, unaweza kuamini kuwa wanalipenda Taifa kuliko CCM, lakini ukweli ni kuwa wanaipenda CCM kuliko Taifa. Walikuwa tayari kushiriki na kuubariki uovu wa CCM ili tu wasitengane na wenzao ambao kwao CCM ni lazima iwe madarakani hata kama itabidi kumtumia ibilisi.
Tamko: ADUI MKUBWA WA USTAWI WA KWELI WA TAIFA LETU KWA KUPITIA KATIBU ILIYO BORA, NI CCM. Adui hashangiliwi, bali anapingwa, anashambuliwa na kuondolewa. Vinginevyo, adui abadilike na kuwa rafiki na kungana na walio wema katika kutafuta na kutenda mema.