Toka mwaka 2015 kuna matukio makubwa ya Kihalifu ambayo yameitetemesha Tanzania na hayajapata ufumbuzi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
3,914
2,000
Toka mwaka 2015 kumekuwa na matukio makubwa nchini ambayo yaliyumbisha nchi hasa upande wa Idara ya Usalama. Na ambayo waliyoyapanga walifanikiwa kwa Asilimia 100 kuvishinda vyombo vya dora.

1. Tukio la kutekwa na kupotezwa Ben Saanane mwanaharakati ambaye alikuwa akiandika sana suala la Elimu ya Mh Rais. Huyu bwana mwanaharakati mkosoaji mkuu wa Utawala wa Magufuli pamoja na Magufuli mwenyewe. Alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka leo hajaonekana. Polisi imeshindwa kufahamu lolote kuhusu huyu bwana.

2. Mwandishi wa habari Azory N. Huyu alikuwa akiandika habari kuhusiana na matukio yaliyokuwa yanatokea Kibiti. Kipindi hicho kuna mkanganyiko ,fujo na vurugu. Alitekwa na watu ambao kwake hawakujulikana. Mpaka leo hajarudi na Polisi hawajafanikiwa kwa lolote ktk hili.

3. Shambulio la Tundu A. Lissu huyu alishambuliwa katikati ya jiji la Dodoma na kumiminiwa risasi nyingi sana. Waliofanya tendo hilo mpaka leo haijawezekana kukamatwa wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Serikali pamoja na kuwa na mkono mrefu inaonekana hawa wameiweza sana. Serikali imenyoosha mikono juu.

4. Nadhani wahalifu waliona kuwa kuna shida upande wa ulinzi wa ndani ya nchi kwa kipindi hicho.wakatumia nafasi hiyo kuja mteka Mo Dewji mfanyabiashara Tajiri Kijana.hawa walitoka nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo flan flan. Wakafanikiwa kwa asilimia 100 kumteka, kuwa naye na baadaye kumwachia. Hawa hawajapatikana mpaka leo na hamna anayehangaika nao.maisha yanaendelea kama kama.

Kwa maono yangu nadhani haya matukio yalikuwa na lengo baya la kutaka kuifanua serikali ionekane haipo stable hasa katika suala la usalama wa Raia wake.ni matukio ya kuipaka taka nchi na Serikali yake.

Pia kuonesha kuwa jeshi letu ni dhaifu katika upande wa Intelejensia.kitu ambacho si sahihi.maana mara nyingi jeshi limekuwa liking'amua mapema mbinu zinazotaka kufanywa na wapinzani hasa kwnye maandamano na mikutano kabla ya matukio hayo kufanyika.
 
Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
668
1,000
Na bado hizo tano nyingine ndio tutaona mambo makuu na ajabu kuwahi kutokea as long as Hana tena cha kupoteza.
 
batmanwafez

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
612
1,000
Mtu mmoja utoe pesa kwenye mfuko wa shati utunze kwenye mfuko wa suruali, je utasema hio pesa sio yako?!
 
omoghambi

JF-Expert Member
Apr 24, 2016
298
500
Toka mwaka 2015 kumekuwa na matukio makubwa nchini ambayo yaliyumbisha nchi hasa upande wa Idara ya Usalama. Na ambayo waliyoyapanga walifanikiwa kwa Asilimia 100 kuvishinda vyombo vya dora.

1. Tukio la kutekwa na kupotezwa Ben Saanane mwanaharakati ambaye alikuwa akiandika sana suala la Elimu ya Mh Rais. Huyu bwana mwanaharakati mkosoaji mkuu wa Utawala wa Magufuli pamoja na Magufuli mwenyewe. Alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka leo hajaonekana. Polisi imeshindwa kufahamu lolote kuhusu huyu bwana.

2. Mwandishi wa habari Azory N. Huyu alikuwa akiandika habari kuhusiana na matukio yaliyokuwa yanatokea Kibiti. Kipindi hicho kuna mkanganyiko ,fujo na vurugu. Alitekwa na watu ambao kwake hawakujulikana. Mpaka leo hajarudi na Polisi hawajafanikiwa kwa lolote ktk hili.

3. Shambulio la Tundu A. Lissu huyu alishambuliwa katikati ya jiji la Dodoma na kumiminiwa risasi nyingi sana. Waliofanya tendo hilo mpaka leo haijawezekana kukamatwa wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Serikali pamoja na kuwa na mkono mrefu inaonekana hawa wameiweza sana. Serikali imenyoosha mikono juu.

4. Nadhani wahalifu waliona kuwa kuna shida upande wa ulinzi wa ndani ya nchi kwa kipindi hicho.wakatumia nafasi hiyo kuja mteka Mo Dewji mfanyabiashara Tajiri Kijana.hawa walitoka nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo flan flan. Wakafanikiwa kwa asilimia 100 kumteka, kuwa naye na baadaye kumwachia. Hawa hawajapatikana mpaka leo na hamna anayehangaika nao.maisha yanaendelea kama kama.

Kwa maono yangu nadhani haya matukio yalikuwa na lengo baya la kutaka kuifanua serikali ionekane haipo stable hasa katika suala la usalama wa Raia wake.ni matukio ya kuipaka taka nchi na Serikali yake.

Pia kuonesha kuwa jeshi letu ni dhaifu katika upande wa Intelejensia.kitu ambacho si sahihi.maana mara nyingi jeshi limekuwa liking'amua mapema mbinu zinazotaka kufanywa na wapinzani hasa kwnye maandamano na mikutano kabla ya matukio hayo kufanyika.
kuna mambo mengi sana ambayo hayatangazwi kwa ajili ya usalama, hata waliohusika na kumteka mo unaezakuta wameshashughulikiwa kitambo ila tu sio mambo ya kutangazwa itv na tbc ndio mana unaona hayajashughulikiwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom