Toka Mtandaoni: Yahusuyo kuvuja kwa sauti za makada maarufu wa CCM Nape Nnauye na Mzee Abdulhaman Kinana

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,260
2,000
Nimeisikiliza clip inayodaiwa kuwa ni ya Nape na mzee Kinana wakizungumza kwenye simu. Nimeirudia zaidi ya mara 3. Bahati nzuri wote wawili nawajua in personal. Nape namfahamu na nimekutana nae kwenye matukio mbalimbali akiwa Katibu mwenezi wa CCM na baadae Waziri.

Kinana for the first time nilimuona ana kwa ana mwaka 2005 pale Kilimanjaro cranes Hotel. Tukiwa vijana wa Youth of the United Nations (YUNA) tulialikwa dinner na aliyekua mshauri wa Rais Mkapa kuhusu uchumi Dr.Cyril Chami, kutueleza azma yake ya kugombea ubunge wa Moshi vijijini mwaka huo. Kinana nae alikua sehemu ya 'congregation' hiyo. Baadae nikaja kumuona mara kadhaa akiwa Katibu mkuu wa CCM.

Kwa uzoefu wangu binafsi kuhusu watu hawa, nashawishika kuamini kwamba sauti zinazosikika ni sauti zao halisi (sio za kutengenezwa).

Lakini najiuliza wamewezaje kuongea mambo sensitive kama hayo kwenye simu? Wanasikika wakimlaumu Rais Magufuli kwamba amewasahau watu waliomnyanyua akafika hapo alipofika. Wamemuita Magufuli ni mshamba na ni mtu aliyechanganyikiwa. Wanaquestion hata IQ ya Mafufuli kuhusu mambo mbalimbali.

Wanajadili na kupanga mipango mizito ya kuonesha kutoridhishwa na namna Magufuli anavyoendesha nchi. Nape anamueleza Kinana kuwa tayari tamko lao na Makamba limeshaenda kwenye media na limepata msukumo mkubwa. Kinana anatoa maelekezo kwamba Mzee Makamba akipigiwa simu na waandishi wa habari asikubali kuongea lolote, badala yake awaambie wasome tamko.

Kinana anasema ameshaongea na Mkapa na Rais Mkapa anasikitishwa sana na namna Magufuli anavyoendesha nchi. Kinana anamuelekeza Nape aongee na Kikwete ili nae atoe tamko la "jumla jumla" ili isionekane anampinga Magufuli lakini angalau ujumbe ufike. Nape anamueleza Kinana atawasiliana na Warioba na wazee wengine nao watoe tamko. Wanasema Magufuli ameshindwa kuendesha nchi kiasi kwamba anaogopa hata kurudi Dar.

Kwa kifupi wameongea mambo mengi sana yanayolengaa mambo yafuatayo:
1. Rais Magufuli amewatupa waliomfikisha alipo
2. Rais ameshindwa kuongoza nchi
3. Kuna mpasuko mkubwa ndani ya CCM
4. Marais wastaafu na viongozi wengi wa zamani hawaridhishwi na namna nchi inavyoendeshwa lakini wanaogopa kusema
5. Nape na Kinana wana kisasi kikubwa na Rais Magufuli

Lakini swali la msingi linabaki je, clip hii imevujaje wakati waliongea kwenye simu wawili tu? Nani alirekodi kati ya Kinana na Nape? Nani alisambaza? Kwa maslahi gani?

Mhandisi mmoja wa mawasiliano anaeleza kuwa si Nape wala Kinana aliyevujisha sauti hiyo. Si Nape wala Kinana aliyerekodi. Si Nape wala Kinana aliyesambaza.

Hata ukisikiliza vizuri utagundua sauti zote mbili zinasikika clear. Ingekua mmoja kamrekodi mwenzake, yule aliyerekodi angesikika juu kuliko aliyerekodiwa. Kwahiyo hawakujirekodi.

Kuna namna mbili ambapo sauti hiyo inaweza kuwa imevuja. Namna ya kwanza ni kuvujishwa na mitandao wa simu wanayotumia (service provider). Namna ya pili ni simu zao kuingiliwa na wadukuzi.

Kuhusu mitandao ya simu kuvujisha iko hivi; watu wengi hawajui kwamba simu yoyote unayopiga inarekodiwa, na ujumbe wowote wa maandishi (sms) unaotuma unahifadhiwa. Ukimpigia mtu simu ukamtukana hata kama yule mtu hajakurekodi anaweza kukushtaki. Na mahakama ikiagiza kampuni husika ya simu ilete ushahidi wa maongezi yenu kwa siku hiyo unayoilalamikia, maongezi hayo yataletwa mahakamani kwa ushahidi.

Maongezi yote ya kwenye simu hurekodiwa automatically na hutunzwa kwa miezi mitatu kabla ya kufutwa kwenye database ili kuruhusu space kwa watumiaji wengine. Na 'sms' yoyote unayotuma hutunzwa kwa miezi 6 au zaidi.

Kwa kawaida mitandao ya simu hairuhusiwi kuvujisha taarifa za mteja katika hali yoyote isipokuwa kwa amri ya mahakama tu. Hii ni katika kulinda faragha (privacy) ya watumiaji.

Lakini sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970 (National Security Act), sheria ya ujasusi na usalama ya mwaka 1996 (Intelligence and Security Service Act), na Sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2006 (Prevention of Terrorism act), zinaruhusu mitandao ya simu kutoa taarifa zako bila hata ruhusa ya mahakama, ikiwa tu mawasiliano yako yatashukiwa kwamba yanahatarisha usalama wa nchi.

Kwahiyo mitandao ya simu inaweza kutoa taarifa zako ikiwa ni pamoja na simu ulizopiga na 'sms' ulizotuma kama zitashukiwa kwamba zihatarisha usalama wa nchi. Pia sheria hizo zinaruhusu makachero wa TISS kudukua mawasiliano yako (kusikiliza simu zako na kusoma sms zako) kama watahisi mawasiliano yako yanahatarisha usalama wa nchi.

Kwahiyo mitandao ya simu si mahali salama sana pa kuongea mambo sensitive na kupanga dili kama hizi za Nape na Kinana. Mitandao ya simu ni ya kutumia kwa tahadhari sana.

Mahali pekee unapoweza kuwa na angalau uhuru kidogo wa kuongea kwa kujiachia ni kupitia whatsapp call, kwa sababu domain yake haitunzi conversation na huwezi kurekodi simu ya whatsapp. Lakini hizi simu za kawaida na meseji za kawaida ni "unoko" mtupu. Ukitaka kupiga simu ya kawaida, piga kuwajulia hali ndugu zako na kudiscuss viazi vyako ulivyolima kule Njombe. Sio mambo mazito kama haya ya kina Nape.

Je nani alaumiwe kwenye hii issue?
Wa kulaumiwa si mitandao wa simu (assuming wamelazimishwa kutoa hizo rekodi). wala wa kulaumiwa sio TISS (kama walihack simu za kina Nape na Kinana).

Wa kulaumiwa ni Nape na Kinana wenyewe, kwa sababu kwa uzoefu wao walipaswa kujua yote haya. Kwa sababu wao ni wanasiasa ambao ni 'high profile' walipaswa kujua simu zao zinaweza kuwa hacked wakati wowote, au mitandao ya simu inaweza kuvujisha mawasiliano yao itakapohitajika kufanya hivyo.

Kwahiyo kitendo cha wao kujiachia na 'kubwabwaja' kila kitu hadharani ni kosa lao wenyewe. Mambo kama haya walitakiwa kuongea wakiwa ana kwa ana. Na kama walishindwa kuonana wangepigiana hata whatsapp call, ambazo haziwezi kuwa hacked na third party.

Lakini kwa kuongea waziwazi kwenye simu means wameamua kujirisk wenyewe. Sasa wasubiri 'Bwana mkubwa' atawafurahisha.!

Acknowledgement to Malisa J. The author of this post
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,260
2,000
.
IMG-20190718-WA0030.jpeg
 

madindigwa

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,643
2,000
Inasikitisha sana wao walitaka kukumbukwa vipi wakati tayar mmoja ni mstaafu na mwingine sio kiongozi wa chama walitakaje? Kwa kiasi chao walikitumikia chama kama wafanyakazi wa chama kwa sababu walikua wanalipwa mishahara yao na mzee Kinana kama bado alikua anatamani uongozi kwa nn alilazimika kustaafu wakati Mwenyekit wa chama alikua anamuhitaji

Wanapenda sana kulambwa miguu hawa wastaafu watu wakae pemmbeni ss hivi vijana tunataka fikra mpya waache kuwashwa washwa hawa wazee tunawaheahimu wamuache rais wetu afanye majukumu yake wao tayari ni zilipendwa tunacho hitaji kutoka kwao ni fikra zao na hekma tu
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,610
2,000
Kuhusu sakata! Mi ni Chadema kindakindaki! lakini kiukweli nimeumizwa sana na mashambulizi dhidi ya kinana & co, yanayofanywa na cyprian & co, alipambana sana kuijenga sisiemu lakini kichaa & co wanachukulia poa daaa noma sana!
Unadhani Kinana hua anaionea huruma Chadema wkt wakina Mbowe&wabunge wanawekwa ndani hovyo hovyo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom