Toka mtandaoni: Hivi kwanini Mungu anaruhusu mambo kama haya yatokee?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Binti yake Billy Graham alihojiwa katika kipindi cha Early Show kinachoongozwa na Jane Clayson, alimuuliza "Hivi inakuwaje Mungu anaruhusu mambo kama haya yanatokea? Akimaanisha Shambulio la Kigaidi la Sept 11, Vimbunga, Matetemeko ya Ardhi.

Anne Graham akatoa ufafanuzi na jibu ambalo limejaa umakini mkubwa, akasema "Ninaamini Mungu anasikitishwa sana na mambo haya, kama yanavyotuhunisha sisi, Lakini chakusikitisha zaidi kwa miaka mingi sana tumekuwa tukimwambia Mungu asijishughulishe na shule zetu, asijishughulishe na serikali na taifa letu, na mbaya zaidi asijishughulishe na maisha yetu. Sasa kwa kuwa Mungu wetu niwa hekima na msikivu, naamini kabisa ameamua kutuacha.

Sasa inakuwaje tunatarajia atupe baraka zake na ulinzi wake wakati tumemwacha na tumemwambia asishughulike na mambo yetu?

Kwa mfano kwa matukio yalitokea hivi punde kama mashambulio ya kigaidi, Kupigwa risasi kwa wanafunzi mashuleni na n.k. Nafikiri yameanza wakati Madeleine Murray O'Hare (ambaye ameuwawa na mwili wake umepatika siku za karibuni) alipolalamika na kudai hapendi maombi na maombezi yafanyike katika shule zetu. Na sote tulikubali kuondoa maombi mashuleni. Wengine wakasema kusiwe na masomo ya Biblia mashuleni.

Lakini Biblia ndio inafundisha ikisema "Usiue", "Usiibe" na mpende jirani yako kama nafsi yako. Na sote tulisema sawa mafundisho ya Biblia yaondolewe mashuleni.

Pia Dr. Benjamin Spock alisema tusiwaadhibu watoto wetu wanapokosa kwasababu kwa kufanya hivyo tunaathiri utu wao na kuwavunjia heshima zao (chakusikitisha mtoto wake mwenyewe Dr. Spock alijinyonga). Tulisema watalaam wanatambua nini wanachozungumza. Na wote tukaridhia tukaacha kuwaadhibu watoto.

Lakini sasa tunajiuliza maswali kwanini watoto wetu hawajitambui wala hawawezi kutofautisha jema na baya, kwanini hawana hofu ya kuua watu wengine, ama wanafunzi wenzao, au kujiua wenyewe.

Yamkini, kama tukifikiria kwa makini, tunaweza kugundua tatizo liko wapi. Ila nadhani hali hii inatokana na dhana kwamba "TUNAVUNA TULICHOPANDA"

Inasikitisha ilivyorahisi watu kudharau na kumwacha Mungu, na kushangaa kwanini dunia inaenda jehanamu. Inasikitisha kwa jinsi tunavyoamini kinachoandikwa katika magazeti, lakini tunahoji kilichoandikwa kwenye Neno la Mungu.

Inasikitisha ilivyorahisi kutuma habari za utani/ mzaha kwa kutumia mitandao ya kijamii kama barua pepe, na zinasambaa kwa haraka utadhani moto wa nyikani, lakini kutuma habari zinazomhusu Mungu unasitasita kutuma kwa wengine.

Inasikitisha kuona jumbe zenye maneno ya kashfa, matusi, kejeli, dharau, zisizo na staha zinavyoweza kutumwa katika mtandao kirahisi, wakati huo huo majadiliano ama mafundisho ya Neno la Mungu kwenye jamii yanazuiwa na kuwekewa vikwazo yasifanyike mashuleni, na maeneo ya kazi... Unacheka?

Inasikitisha kuona jinsi unavyosita na pengine kuacha kutuma ujumbe huu kwa watu wengi uwezavyo au kwa wale ambao una namba zao za simu kwasababu huna uhakika na kile wanachoamini, au watakufikiriaje unakapowatumia ujumbe huu.

Inasikitisha tunavyoweza kuwa na wasiwasi na woga juu ya watu watakavyotufikiria na sio Mungu anavyotufikiria.

Tafadhali tuma kwa watu wengine kama unafikiria ujumbe huu utawasaidia, kama huamini hivyo basi unaweza ukaacha usiwatumie, kwasababu hakuna atakayefahamu kuwa hukuwatumia.

Lakini ukiacha kutuma ujumbe huu na tafakari hii, basi usije ukaanza kulalamika jinsi dunia hii inavyoharibika.

Mungu akubariki na tafadhali watumie na rafiki zako na watu wengine.

Hakuna Taifa ama mtu yeyote anayeweza kuwa salama ama kufanikiwa bila kumshirikisha Mungu.
 
Simple, mungu hayupo alitungwa tu.

Hiyo statement 'hakuna mtu wala taifa linaloweza fanikiwa bila mungu' ni uongo mtupu.
Mataifa mengi yaliyofanikiwa ukiangalia utakuta wenye dini ni less than 50% tofauti na huku Afrika dini almost 90% tumeshika upuuzi tu tunakufa njaa. Tembea duniani uone.

Top billionaire list wote zaidi ya 1,000 angalia dini zao, utakuta 90% ni atheists, hawaamini uwepo wa mungu, sasa hiyo statement yako sijui ulifanya research wapi. Mataifa yanayohusisha mungu karibia yote yamefeli, mfano namba moja afrika, na tukija kwenye dini ya kiislamu angalia nchi za waarabu zilivyo ovyo, UAE peke yake ndiyo ina uafadhali.
 
Aseee Mshana huyo binti ya Billy Graham kwanza anaelewa kila kitu, maana baba yake mwenyewe ni mmoja wa viongozi wakubwa wa lile kundi la siri linalotengeneza na kuratibu matukio siri/secret agenda.

Na babake katika kuonyesha umma (usio jua kiundani) akawa amejivuka vazi la kuwa mtumishi wa dhehebu.

BUT: Tunaposema Mungu aoni au azuie tunaweza kusema siyo kazi yake au ikawa kazi yake kutokana na maelezo ya maandiko pale yanaposema "siku za mwisho maarifa yataongezeka.. ".

Tabia za watoto/watu kufanya uharifu na matukio hasi yenye kuogofya yanatokana na njia tuiemdeayo kuufikia ule mwisho, pia maandiko ya Bilblia yanasema "siku za mwisho Upendo kwa ndugu utapoa, mataifa yatapigana watu watakimbia huku na kule kutafuta Amani, ..."

BUT, Unapoona watu wanapenda habari za mambo ya kuchekesha, yenye mihemko, machafu nk na wanapoona maandishi yenye ujumbe wa Mungu hata kufungua hatufungui ujie ndipo pale paliponenwa 'Halitasalia jiwe hata moja, .."
 
Ni kweli kabisa na nakubaliana nawe kwa asilimia 100, mungu hayupo na kwakweli alitungwa tu na ithibati zipo.... Ila Mungu yupo... Alikuwepo yupo na atakuwepo...!!!!
We andika herufi kubwa ndogo it doesn't matter, mlilishwa matango poli toka utotoni sasa hivi ni ngumu sana kujitoa kwenye hicho kifungo cha akili.
 
We andika herufi kubwa ndogo it doesn't matter, mlilishwa matango poli toka utotoni sasa hivi ni ngumu sana kujitoa kwenye hicho kifungo cha akili.
Hapana ninachokwambia ni hakika... Nilitoka nje ya box na nikauona uhalisia... "Ninaamini kwa hakika Mungu yupo... Mimi sio blind believer.... Mungu ni sawa na akili... Unayo lakini huwezi kuionesha
 
Hapana ninachokwambia ni hakika... Nilitoka nje ya box na nikauona uhalisia... "Ninaamini kwa hakika Mungu yupo... Mimi sio blind believer.... Mungu ni sawa na akili... Unayo lakini huwezi kuionesha
Huwezi kumtoa mpumbafu ktk upumbafu wake. Unachoweza ni kumuonesha kuwa ni mpumbafu tu. Yanini kujitaabisha na mtu awaye yote ilhali hajitaabiishi?

Hakuna mtu mwenye akili kwani nani alipata kuiona? Ni tungo tu za BinAdam ili kujitaabisha na kujilisha upepo!

Bazazi
 
Huwezi kumtoa mpumbafu ktk upumbafu wake. Unachoweza ni kumuonesha kuwa ni mpumbafu tu. Yanini kujitaabisha na mtu awaye yote ilhali hajitaabiishi?

Hakuna mtu mwenye akili kwani nani alipata kuiona? Ni tungo tu za BinAdam ili kujitaabisha na kujilisha upepo!

Bazazi
Asante
 
"Inasikitisha kwa jinsi tunavyoamini kinachoandikwa katika magazeti, lakini tunahoji kilichoandikwa kwenye Neno la Mungu."
 
Back
Top Bottom