Toka mtandaoni: Dodoso la kumpokea mfanyakazi wa nyumbani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
*Dodoso la kumpokea dada au kijana, msaidizi wa kazi za nyumbani*

1. Majina kamili
2. Umri
3. Historia ya familia
4. Historia ya elimu
5. Historia ya Afya
6. Historia ya kazi na kwanini aliacha.
7. Ratiba yake ya siku
8. Kazi anazoweza kufanya
9. Kazi asizoweza kufanya na kwanini.
10. Aina ya vyakula asivyoweza kula na kwanini
11. Tambua Dini yake na imani zake.

*Zingatia*

●Baada ya kumdodosa dada, andika majibu yake na utumie hayo kumpangia majukumu yake na kanuni za kazi hapo kwako.

●Ni muhimu dada kupima afya yake pindi anapoingia kwako.

●Ni muhimu dada kuwa na barua ya utambulisho kutoka kijiji alipotoka iliyosainiwa na yenye muhuri na saini ya mwenyekiti wake

●Ni muhimu dada kuja na kithibitisho cha wazazi au walezi wake kuridhia kufanya kazi hapo na uwe na mawasiliano nao.

●Ni muhimu kuweka wazi ratiba za likizo

●Ni muhimu kuweka wazi matumizi yatakayokua juu yako na atakayojitegemea

●Ni muhimu kumuandalia ratiba ya kazi itakayomuongoza kwa siku nzima.

●Ikiwezekana binti akaguliwe vitu alivyokuja navyo wakati anapofika.

●Msisitize binti kuhusu usafi wa mwili wake na wa mazingira pamoja na chakula wakati anandaa

●Muajiri jitahidi kuishi na binti kwa upendo mpe motisha na kumpongeza anapofanya vizuri na kumuelekeza vizuri pale anapokosea ili ajifunze na si kumkaripia kila mara au hata kumpiga.

Angalizo: Iwapo utamnunulia binti zawadi mf. Nguo fanya kwa kiasi ili azoee, wengi hufurahi kupitiliza na kutaka kurudi kwao kuringishia nguo zao na hii sio nzuri kwa muajiri

●Binti aelekezwe kupokea wageni na ndugu kwa ukarimu, lakini pia muajiri usiseme siri za familia au kumsema mtu wa familia mbele ya binti.

●kama una watoto waelekeze kujitegemea na kushiriki baadhi ya kazi, usijisahau ukaharibu watoto sababu wanafanyiwa kila kitu.

●Binti asaini mkataba unaoelekeza majukumu yake na kanuni za kazi na malipo yake.

●Binti asaini kila anapopokea mshahara

```Lengo ni kujenga mipaka,heshima na usalama wa kazi na familia nzima
 
Duh mambo kibao utadhani analipwa milioni. Kupima afya ni sawa na pia kujua tabia zake ila kitu muhimu kwa wafanyakazi ni kuwa treat right mfano kuwalaza katika vyumba vizuri, kula chakula mnachokula familia na kufanya kazi kwa upamoja mfano unamwagilia maua na ww siku moja moja kuonyesha hata na ww unaweza fanya kazi zake. Wawe wasafi hapa waajiri tunachangia sana utakuta unamfanyisha kazi kama kufyeka na kutompa sabuni za kufulia au kuogea pia kumnunulia nguo za kutosha mashuka na mataulo ili aweze kuwa msafi. Usafi ni uwekezaji.

Mie nina wafanyakazi wawili kwa sasa wana miaka 5 na pia nimeshakaa na dada wa kazi toka ana miaka 18 mpk akaja kuolewa akiwa 23 na jamaa aliyemuoa alijua ni mdogo wangu na kwa sasa ana drive ki-passo wako njema kabisa. Pia kuna mdada alipata mimba nikamwondoa yaani alilia sana mpk ikabidi alipojifungua nimfungulie sehemu ya kushona na kwa sasa amepanga anajitegemea

Pia tusiwanyime vyakula kama matunda wacha wale hata mayai mfanye ajisikie yuko nyumbani. Mahausi boy wangu wote waliopitia niliwafundisha kuendesha gari na kuwakatia leseni na uwa nawatumia kwenda shambani na safari nyingine ndogondogo za nyumbani hivyo wakisepa wanakuwa masuka wazuri tu
 
kama una watoto waelekeze kujitegemea na kushiriki baadhi ya kazi, usijisahau ukaharibu watoto sababu wanafanyiwa kila kitu."

Hili ni la msingi sana.

Jamii inaelekea pabaya kwa sasa kutokana na watoto kutofundishwa kazi.

Wafanyakazi wa ndani wanafanya kila kitu.
 
Duh mambo kibao utadhani analipwa milioni. Kupima afya ni sawa na pia kujua tabia zake ila kitu muhimu kwa wafanyakazi ni kuwa treat right mfano kuwalaza katika vyumba vizuri, kula chakula mnachokula familia na kufanya kazi kwa upamoja mfano unamwagilia maua na ww siku moja moja kuonyesha hata na ww unaweza fanya kazi zake. Wawe wasafi hapa waajiri tunachangia sana utakuta unamfanyisha kazi kama kufyeka na kutompa sabuni za kufulia au kuogea pia kumnunulia nguo za kutosha mashuka na mataulo ili aweze kuwa msafi. Usafi ni uwekezaji.

Mie nina wafanyakazi wawili kwa sasa wana miaka 5 na pia nimeshakaa na dada wa kazi toka ana miaka 18 mpk akaja kuolewa akiwa 23 na jamaa aliyemuoa alijua ni mdogo wangu na kwa sasa ana drive ki-passo wako njema kabisa. Pia kuna mdada alipata mimba nikamwondoa yaani alilia sana mpk ikabidi alipojifungua nimfungulie sehemu ya kushona na kwa sasa amepanga anajitegemea

Pia tusiwanyime vyakula kama matunda wacha wale hata mayai mfanye ajisikie yuko nyumbani. Mahausi boy wangu wote waliopitia niliwafundisha kuendesha gari na kuwakatia leseni na uwa nawatumia kwenda shambani na safari nyingine ndogondogo za nyumbani hivyo wakisepa wanakuwa masuka wazuri tu
Aisee Mungu akubariki
 
Sasa wewe na matendo yako mema yote hayo bado unajiita FUNZA?
 
Back
Top Bottom