Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

kwa nini usisafishe wewe mtumiaji? Huna ubwana mkubwa wowote.
Kutumia hovyo utumie wewe akusafishie mwigine kwa hela gani uliyo nayo.

Anaenukisha ni wewe mtumiaji huduma. Huoni hata aibu?

siyo wafanyakazi wa ward kwa malipo gani manono ya huyo mfanya kazi unadhani...mnastahili hayo kwa tabia zebu chafu.

Km vipi nenda Agakhani pasafi kwa wasafi uone gharama zake.nyie wachafu mnastahili uchafu msilie.unatoka kwa mtogole unataka pawe km agakhani mweee!! Si kila mswahili ataomba kulazwa!!

Unatamani pawe km TMJ Hosp??? Ni gharama zile nenda kaonje huduma bora kwa walio barikiwa maskini wewe....
Na Kodi yangu wanakata inaeenda wapi?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama Watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.

Kwa vile huu uzi ulikuwa wa kumsifia Mwendazake na baadae akaja kuwa adui mkubwa wa Jamii Forum, na kutaka kuifunga kama angeweza..
FUTENI HUU UZI..
 
Habar za asubuh wakuu,

Kwa mda mrefu nimekua nikisubir mama atoe tamko au afanye jambo pale kwenye wizara nyeti hasa inayogusa maisha ya watanzania moja kwa moja naona mama yuko kimya tu km vile alikua aoni wakati janga linakula watu km muchwana kuna mkulu mmoja tena anajiita Musomi sijui wa Phd anajifunika na kujifukiza mara anakunywa mwarobaini saiv yuko busy anavaa barakoa 24/7 na ameshaua watu wetu kwa kushindwa kuchukua hatua sijui bado anafanya nin?

Pale yule msaanii wa Bongo fleva mama nakusihi fanya jambo kwa ajiri ya watanzania yule Dr wa miti shamba afai kuwa mkulu wa kitengo cha afya pale HQ.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mambo mazuri aliyoyafanya Hayati Magufuli yafuatuliwe kwa karibu. Narudia yake mazuri, na nitataja machache.
1. Ufisadi,uonevu ubadhirishaji. Kwa mfano matukio ya kupindisha mambo...kwa sasa imerudia wananchi wakiuza au kununua shamba au nyumba Ofisi za serikali za Mitaa kudai 10% hii naona imerudia kwa kasi..

2. Hata wenye vyeti feki wanarejea oh my God ness
 
Na Kodi yangu wanakata inaeenda wapi?
ahahahaha!! Kwa hiyo unakunya hovyo!! Na kutumia mali za sirikali hovyo kwa ajili ya kinyongo na kodi yako siyo?

Utahangaika na kusubili sana dogo.
ile kodi inaishia ulinzini huko. Kodi nyingine ni wewe kutunza mali hizo uzuri.

Hata huyo unaetaka akuhudumie anakatwa kodi tena faster hukohuko!!

Hata ivo mnunuzi ni sirikali yako.
 
NBC BANK pesa za mikopo zimeisha au hujuma? Haiwezekani MTU unaomba mikopo mwezi Mzima hela haipatikani.Kama mmeishiwa pesa si useme watu waende kwengine?
 
kwa nini usisafishe wewe mtumiaji? Huna ubwana mkubwa wowote.
Kutumia hovyo utumie wewe akusafishie mwigine kwa hela gani uliyo nayo.

Anaenukisha ni wewe mtumiaji huduma. Huoni hata aibu?

siyo wafanyakazi wa ward kwa malipo gani manono ya huyo mfanya kazi unadhani...mnastahili hayo kwa tabia zebu chafu.

Km vipi nenda Agakhani pasafi kwa wasafi uone gharama zake.nyie wachafu mnastahili uchafu msilie.unatoka kwa mtogole unataka pawe km agakhani mweee!! Si kila mswahili ataomba kulazwa!!

Unatamani pawe km TMJ Hosp??? Ni gharama zile nenda kaonje huduma bora kwa walio barikiwa maskini wewe....
Usafi ni jambo ambalo hatujaumbiwa watu weusi.watu weusi wengi ni wachafu sana.mtu anatumia choo maji yapo na bado ha flush choo au kumwagia tu.
Wafanyakazi wanasafisha,wanafua,wanafagia nje kumaintain usafi kwa hali nzuri ni ngumu maana mara nyingi wapo wachache.sasa ni vizuri watumiaji wawe wastaarabu
 
Kwa vile huu uzi ulikuwa wa kumsifia Mwendazake na baadae akaja kuwa adui mkubwa wa Jamii Forum, na kutaka kuifunga kama angeweza..
FUTENI HUU UZI..
Wacha ubaki kwa kumbukumbu ila waanzishe mpya wa awamu ya sita,tena upewe jina (mwambie Mama Samia kero zako) itapendezaa zaidi haswa ukizingatia mama amejitambulisha kuwa mpenzi wa mitandao ,na imani akijua amefunguliwa page ya kupokea kero atatendea haki kero zetu ,kwako Max ,Jf response terms as whole JamiiForum members
 
Hapa Namtumbo-Ruvuma kuna jipu idara ya maji,Maji yanatoka mara moja kwa wiki tena usiku ila pesa inakusanywa elfu kumi/10000/= per month.
Wananchi wanaona ni aina ya ufisadi na kufanya maisha ya watu kuwa magumu,maana kungekuwa na mita uhalali ungekuja elfu 3 au 4 per month.
Kijana wangu Juma Awesso tunakuomba uje utuokoe kama utapita na kuisoma hii kero
 
Tulitegemea huyu rais aje na utatuzi wa mitanziko mikubwa iliyojitokeza ktk awamu ya 5 baada ya mwendazake kutumia katiba yetu mbovu na sheria zetu mbaya kuliyumbisha taifa. Hivyo tulitarajia yafuatayo:-

1. Abatilishe na kubadilisha sheria zinazowaweka watuhumiwa rumande kimabavu, mfano;- mashekhe, Harbinder Seth, Papaa Msofe, n.k

2. Aibadilishe katiba ili isitoe mwanya kwa mtu mmoja (rais) ama chama tawala kuharibu uchaguzi kama ilivyokuwa 2020.

3. Atoe tamko hata la kulaani tu kama sheria haimpi uwezo wa kuwatumbua kabisa Covid-19 waliopo bungeni. Lkn anaonekana kudemka ngoma ya mtangulizi wake. Nimeona alipokuwa Mwanza amemtambua Nusrat kama mbunge anayewakilisha vijana mkoa wa Singida na akapewa nafasi ya kutoa neno.

4. Ajitenge na makada wa chadema walionunuliwa na akina Bashiru na Polepole. Lkn naona bado anawapa uwaziri, uDC, n.k. Nadhani atawatumia huko mbeleni kwa staili zile zile za awamu ya 5.

5. Afanye teuzi kwa misingi ya weledi. Lkn naona anaangalia zaidi wale wanaoweza kumsogeza mbele kisiasa.

Ndiyo maana anaondoa wasiyo wake na anapachika walio wakwake. Akina Bashiru, Polepole, Heri James pamoja na katibu wa UVCCM amewatoa na anatia chachandu yake.

My take.
Kwa jinsi tunavyoenda, huyu rais wetu hana nia ya kubadilisha katiba na sheria kandamizi.
 
Du! Huyu mwanamke mtamuua.
Ama kweli kuwa Rais ni mtiti.
Leo ni lawama tu toka asubuhi

Rais Samia nakukumbusha tena usijaribu kumridhisha kila unayemwongoza ova.
 
Tulitegemea huyu rais aje na utatuzi wa mitanziko mikubwa iliyojitokeza ktk awamu ya 5 baada ya mwendazake kutumia katiba yetu mbovu na sheria zetu mbaya kuliyumbisha taifa. Hivyo tulitarajia yafuatayo:-

1. Abatilishe na kubadilisha sheria zinazowaweka watuhumiwa rumande kimabavu, mfano;- mashekhe, Harbinder Seth, Papaa Msofe, n.k

2. Aibadilishe katiba ili isitoe mwanya kwa mtu mmoja (rais) ama chama tawala kuharibu uchaguzi kama ilivyokuwa 2020.

3. Atoe tamko hata la kulaani tu kama sheria haimpi uwezo wa kuwatumbua kabisa Covid-19 waliopo bungeni. Lkn anaonekana kudemka ngoma ya mtangulizi wake. Nimeona alipokuwa Mwanza amemtambua Nusrat kama mbunge anayewakilisha vijana mkoa wa Singida na akapewa nafasi ya kutoa neno.

4. Ajitenge na makada wa chadema walionunuliwa na akina Bashiru na Polepole. Lkn naona bado anawapa uwaziri, uDC, n.k. Nadhani atawatumia huko mbeleni kwa staili zile zile za awamu ya 5.

5. Afanye teuzi kwa misingi ya weledi. Lkn naona anaangalia zaidi wale wanaoweza kumsogeza mbele kisiasa.

Ndiyo maana anaondoa wasiyo wake na anapachika walio wakwake. Akina Bashiru, Polepole, Heri James pamoja na katibu wa UVCCM amewatoa na anatia chachandu yake.

My take.
Kwa jinsi tunavyoenda, huyu rais wetu hana nia ya kubadilisha katiba na sheria kandamizi.
Katiba haiombwi ni sharti na haki ya raia kudai katiba .....ukiona kimya ingia baeabarani ni haki yako kama huna subira usiombe ingia kati
 
Tulitegemea huyu rais aje na utatuzi wa mitanziko mikubwa iliyojitokeza ktk awamu ya 5 baada ya mwendazake kutumia katiba yetu mbovu na sheria zetu mbaya kuliyumbisha taifa. Hivyo tulitarajia yafuatayo...
Duuh! Yote hayo within 3 months
 
Back
Top Bottom