Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Keri kubwa ni hivi vibali vya ujenzi. Mtu unaongeza chumba chako kimoja . Mtendaji anakuja anataka rushes ukikataa anakupiga faini na barua limetoka manispaa na muhuri ameligonga. Huu ni utapeli maeneo yetu hayajapimwa iweje ulazimishe kibali na hizi hela wanakuja mgambo wa kata na Mtendaji.

Ikiwezekana futa kabisa Mambo ya watendaji wa kata hawana Cha maana wanachofanya zaidi ya fitina na kukamua wananachi pesa. Misharahara yenyewe haipandi bado Kila mtu anageuka zakayo mtoza ushuru
 
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.
Na imekuwa kama utaratibu wa hawa wagombea kufanya haya mambo hakika ni mambo yasiyovumilika kwa namna moja au nyingine
 
Barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha SIMU 2000 ( mawasiliano) iwekwe lamiharaka ni kero kubwa.
2. Kitua chamabasi yaendyomikoani Ubungo kijengwe haraka.
Hiyo ya barabara, tayari mkuu lami imewekwa
 
Nakumbuka kuna dogo alikuwa amepimwa siku moja nyuma ila anaonekana kuzidiwa sana...ila wao hawajali kama ni mda wa kazi wanapga stori za michepuko yao na siasa waliniuzi kweli aisee na umati wa watu upo nje unasubiri majibu na vipimo ila wao hawaanzi kazi ni stori mbele mx player apk

Regards, mx player pro
 
Kuna huyu Msomali anaitwa Hussen, nadhani ndio mmiliki wa Sanitas Hospital Mikocheni. Huyu jamaa alijenga ukuta wa Hospital chini ya Viwango. Ukuta umeanguka umeharibu Mali za Watu. Jamaa ana jehuri sana na amegoma halipi na hakuna wanaloweza kumfanya. Hili jengo la Hospital litakuja kuuwa watu wengi sana. Tunaomba mamlaka husika waingilie kati. Maana huyu msomali inasemekana hagusiki
 
Kero yangu ni pale jengo la RITA. Rafiki yangu umri miaka 80 alitaka nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwaka 1976 cha mwanawe. Alizungushwa zaidi ya miezi sita akipandisha ngazi ya gorofa la kifahari. Kila mara aliambiwa ETI rekodi haionekani rudi baada ya wiki mbili. Alifika ofisi ya malalamiko mara kadha lakini hakukuta mtu ofisini. Meza tu na kiti. Akaacha barua lakini hakuna majibu. Mwishowe jamaa mmoja msamaria alimwambia atamsaidia. Baada ya wiki moja alimletea cheti rasmi chenye mhuri na saini. Ofisi ya RITA makao makuu inanuka rushwa. Utakuta foleni kibao wazee wakisumbuka. TAKUKURU angalieni hapa
 
Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
Pamoja na wizara husika kupiga marufuku tuition, mimi sioni ubaya wa tuition. Tuition inawasaidia watoto wa wenye kipato cha chini na kati kuwapa watoto wao elimu ya kuwavusha. Kwa wenyenazo hupeleka watoto wao kwenye supper/premium schools ambapo ushindi kwa kawaida ni 100%. Kama wanapiga marifuku tuition shule za serkali je, watadhtu kupiga marufuku shule za binafsi, ambazo mtoto analipia tuitio kama sehemu ya karo?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Pale Dodoma nashukuru Waziri wa Maji, Ndugu Aweso amefanya jambo. Dodoma maji yalikua yashida sana na hakuna sababu za maana zinazotolewa hakuna. Ila tangu Mkurugenzi wa DUWASA ahamishwe maji yanatoka kila siku na hata usiku ambao ulikua maji yanakatika sasa yanatoka.

Ila kiukweli ni kua Mkurugenzi alikua akihujumiwa na watendaji wa chini. Hivyo ipo haja hata wao wakamulikwa maana Mkurugenzi pekee bila waliochini yake waliokua wakikwamisha haiwezekani. Na kuna kauli kua mtu huyo alikua mkali na wakaamua kumhujumu.
 
Mhuuu
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Jipu linaanzia kwake yeye mwenyewe kuvuruga uchaguzi 2020 na kufuta mfumo wa vyama vingi sasa on athari yake viboko vya mkoloni kwa wakosaji vimezaliwa bila kufuata utaratibu,sheria na mwongozo wa nchi.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
kero yangu kupanda kwa bei za vitu mfano wiki mbilizilizo pita mafuta ya kula lita ili kua 3800 ila hadi leo mafita lita ni 5000 tuna elekea wapi
 
Back
Top Bottom