Ni wajibu wa kila Mtanzania kuwa mzalendo na kupaza sauti pamoja na kuonesha kwa vitendo kuwa tunaichukia rushwa na tumekusudia kuitokomeza. Shukrani za pekee kwa Mhe. Raisi John Joseph Pombe Magufuli kwa kuonyesha wazi wazi kuwa ni raisi aliyekusudia kuungana na watanzania wote kutokomeza rushwa na kuleta maendeleo ya taifa. hivyo yatupasa watu wote hasa vijana wenzangu tumuunge mkono raisi wetu kwenye vita hii ya rushwa naimani kubwa kwa uongozi wake tutaweza kuidhibiti rushwa na kuleta maendeleo makubwa kwenye taifa letu.