Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Ni wajibu wa kila Mtanzania kuwa mzalendo na kupaza sauti pamoja na kuonesha kwa vitendo kuwa tunaichukia rushwa na tumekusudia kuitokomeza. Shukrani za pekee kwa Mhe. Raisi John Joseph Pombe Magufuli kwa kuonyesha wazi wazi kuwa ni raisi aliyekusudia kuungana na watanzania wote kutokomeza rushwa na kuleta maendeleo ya taifa. hivyo yatupasa watu wote hasa vijana wenzangu tumuunge mkono raisi wetu kwenye vita hii ya rushwa naimani kubwa kwa uongozi wake tutaweza kuidhibiti rushwa na kuleta maendeleo makubwa kwenye taifa letu.
 
Wewe kama amekutuma mwambie afanye yote anayofanya lakini ahakikishe mzunguko wa fedha aliouua ameurekebisha na hela zipatikane mtaani, vinginevyo hamna anayemuelewa.
 
Wewe kama amekutuma mwambie afanye yote anayofanya lakini ahakikishe mzunguko wa fedha aliouua ameurekebisha na hela zipatikane mtaani, vinginevyo hamna anayemuelewa.
katika kujenga nyumba ni vema uanze na msingi wa mawe then waweza kumalizia na matofali ya tope na nyumba yaweza kudumu mda mrefu sana, hivyo huwezi ukaanza na tope na kumalizia na mawe.
Mh jpm anajenga msingi mzuri wa uchumi katika nchi, miradi mingi alio ianzisha yawezekana hata watoto wake wasiifaidi bali wajukuu wetu watakuja kuelewa kazi kubwa anayo ifanya, so kuwa mpole mkuu!
 
(i). Barabara ya Nyakanazi (Biharamulo) - Kabingo (Kakonko) takribani 54Km imejengwa kwa muda usiopungua miaka 8 bila kukamilika Mkandarasi akiwa Nyanza Road

(ii). Kutokuwepo kwa Meli ya abiria kutoka Mwanza, Kemondo - Bukoba mbadala wa Mv Bukoba iliyozama miaka ya 1990s. Kutokuwepo kwa meli kumesababisha usafiri na usafirishaji kuwa mgumu na ghari sana
 
Wananchi tunaotumia Barabara ya Zakhem-Kijichi, kupitia Mbagala Kuu tuna kero ya kipande cha Barabara toka "Kibonde maji- Kichemchem" ambacho kimeachwa bila kuweka lami kwa muda sasa..
 
Serikali inaibiwa !!!!!!
Sana tena sana wakati wa ukusanyaji ushuru magetini wafanyabiashara hawalipi ushuru sitahiki magetini ,
Wanatoa rushwa private mazao yanapita free kama mzigo ni millioni kumi mfanyabiashara analipa millioni tatu then mzigo unapita free
Simu zinapigwa kabla gari kupita mtu anatanguliza rushwa baadae gari haisimamishwi inapita free ko mfanyabiashara anaweza kutoa kila geti laki tano tano nakupita kwa faida kubwa....!!!
 
Wakuu safi?
Kwa umri mdogo nilionao sijabahatika kushuhudia mashirika mengi ya umma yakifanya kazi effectively. Nimebahatika kukutana na magofu na machuma chakavu tu sehemu mbalimbali za nchi hii ambayo yanasemekana ni magofu ya umma.
Tanzania bara nimefika mikoa 16 kama sitakosea na kila mkoa nimedadisi na kuambiwa kuwa kulikuwa na hiki na kile ambavyo sasa vimekufa au kubinasfishwa kiholela.
Kama walioyahujumu haya mashirika wako hai na documents zinawatambua basi wapandishwe kizimbani haraka. Hii italeta adabu kwa watumishi wanaohudumu katika mashirika na taasisi mbalimbali za serikali.
Note: Serikali isikwepe wajibu wake kwa watumishi wa umma, iwapatie watumishi stahiki zote muhimu.
 
Kwanza nipongeze Serikali ya Mpendwa rais wetu Dr JPM kwa kuwezesha ujenzi wa barabara nzuri sana ya SINZA - TANDALE - UZURI.
Tatizo ni Sub Contractor aliyejenga mitaro! Mitaro imejengwa in such away that mvua ikinyesha maji yanatiririkia kwenye baadhi ya nyumba za watu hasa kipande cha sinza E.
Hii ni kero kubwa kwa wakazi wa sinza E.Tunaomba wahusika waje sinza kujiona hali halisi ili waweze kuchukua hatua stahiki kabla mheshimiwa Rais hajaizindua hii Barabara.

CC: W/ Ujenzi
CC: RC DAR
CC: Tanroads
 
Hivi sisi wananchi wa Maeneo tunaotumia Barabara itokayo Mgeni, Kata ya Mbagala Kuu sio wapiga kura, Mbona na sisi tulimchagua Mh. Rais lakini tumesahailika kabisa Barabara hiyo ina Mashimo sana Magari yanaharibika jamani, Daladala nzuri haziletwi huku sababu kubwa ni ubovu wa barabara:
1. Je, ni watendaji wanaomwakilisha Rais ndo wanaotufanyia figisu
2. Je, taarifa za ubovu huu wabarabara hazifiki kwa wahusika
3. Ama hatuthaminiwi?
 
Kwako Rais wetu Mpendwa Rais wa wanyonge John Pombe Magufuli tupia jicho wilaya ya kigamboni kata ya Mwasonga kuna Madini yamegundulika kwenye maeneo yetu mwekezaji yupo tayari muda wowote kuwalipa wananchi wenye maeneo yao lakini bado anazungushwa na wasaidizi wako hatujui tatizo ni nn?
 
Acha tamaa ya pesa kwani si muda mtaanza kumpigia magoti JPM mkidanganya kuwa hamjalipwa au mmelipwa kidogo
 
Kwako Rais wetu Mpendwa Rais wa wanyonge John Pombe Magufuli tupia jicho wilaya ya kigamboni kata ya Mwasonga kuna Madini yamegundulika kwenye maeneo yetu mwekezaji yupo tayari muda wowote kuwalipa wananchi wenye maeneo yao lakini bado anazungushwa na wasaidizi wako hatujui tatizo ni nn?

Mbaya zaidi hata hatuwezi tena kuyaendeleza maeneo hayo baada ya kuja kupimwa na watumishi kutoka wizara ya ardhi na makazi na kutuambia tusiyaendeleze tena...

Tulipoishia ni hapo hapo na mwekezaji mpaka kibali kashapata kutoka Wizara ya Nishati na Madini lakini kuna watendaji hawa wa chini wanamkwamisha huyu mwekezaji sisi huku wananchi bado tukiendelea kusubilia hatima yetu tangu mwaka wa jana.
 
Madini yoyote ni mali ya serikali, kama yamegundulika sidhani kama huyo mzungu anaweza yachimba pasipo vibali vya serikali..
 
Madini yoyote ni mali ya serikali, kama yamegundulika sidhani kama huyo mzungu anaweza yachimba pasipo vibali vya serikali..

Soma vizuri hapo juu thread yangu nimeeleza...

Mwekezaji hadi kibali kashapewa kutoka Wizara ya Nishati na Madini!
 
Soma vizuri hapo juu thread yangu nimeeleza...

Mwekezaji hadi kibali kashapewa kutoka Wizara ya Nishati na Madini!

NB; mpaka pesa kashakopa benki kwa ajili ya kutulipa wananchi lakini serikali wilaya ya kigamboni ndio wanaoleta mizengwe
 
Soma vizuri hapo juu thread yangu nimeeleza...

Mwekezaji hadi kibali kashapewa kutoka Wizara ya Nishati na Madini!
Mkuu thread yako inasomeka hivi, hakuna neno kibali...

Anyway bila shaka JPM atasoma mambo uliyomuandikia hapa

Kwako Rais wetu Mpendwa Rais wa wanyonge John Pombe Magufuli tupia jicho wilaya ya kigamboni kata ya Mwasonga kuna Madini yamegundulika kwenye maeneo yetu mwekezaji yupo tayari muda wowote kuwalipa wananchi wenye maeneo yao lakini bado anazungushwa na wasaidizi wako hatujui tatizo ni nn?
 
Mkuu thread yako inasomeka hivi, hakuna neno kibali...

Anyway bila shaka JPM atasoma mambo uliyomuandikia hapa

Sisi wote tupo kwa ajiri ya kujenga nyumba moja hakuna sababu ya kugombania fito...

Karibu tena mpwa
 
58 Reactions
Reply
Back
Top Bottom