Serikali ina washauri inatakiwa wewe ushauri washauri wa serikali ili wao waishauri serikali.
Hii ni moja tuu ya mitizamo ya kupotosha kwa sababu inalenga kuaminisha umma kwamba kwa kiasi kikubwa kiongozi mwenye dhamana hayuko responsible kwa maamuzi anayoyafanya kwa kuwa "alishauriwa vibaya".
Dhamana na ushauri ni vitu viwili tofauti. Mtu mwenye dhamana kwa cheo chake anawajibika sii tu kwa maamuzi na matendo yake, bali na kwa walio chini yake. Yeyote anaefanya maamuzi ya hovyo regardless ya kwamba alishauriwa vibaya, anawajibika. Sasa tumekua taifa la kutumia kichaka cha "kashauriwa vibaya" na kuwalenga washauri badala ya wenye dhamana. Hatuwasaidii! Tunawa-absolve of responsibilty na accountability.
Waambieni wawe makini na ushauri wanaopewa hata kama ni kwenye masuala technical beyond uwezo wao. Wawe na personal "system" ya kuchuja ushauri. Kwa mfano kutafiti wenyewe, ku seek ushauri kwa mtu zaidi ya mmoja, kumtaka anaekushauri aje na option zaidi ya moja and atc.