Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Amekuuliza wewe mkuu, Rais anavyombo vingi mtandao mkubwa, kuliko hata huyo anayeongoza..Hii KERO barabarani raia wanainyamazia tu
Pumbavu kweli.

Mnataka hata suala la uongozaji wa magari liongelewe na rais.

Wapuuzi nyie.
 
Nasikia Magufuli atakuwa Mbeya Meimosi mwaka huu, tunaomba shughulikia chuo cha utumishi Mbeya ili wanafunzi na waalimu waishi kwa haki. kwa ufupi, matatizo yafuatayo ndio uozo katika chuo hicho, hili lipo wazi kwa watu wote waliowahi kupitia chuo hicho.

1. Waalimu wanavujisha mitihani sana kwa wanafunzi, hasa wa kike. Kuna wanafunzi tunawajua kabisa hawana akili, wanafaulu kwasababu wanafanya ngono na waalimu, waziwazi. Mwanafunzi yeyote akiulizwa hili anajua, kwa wale wasio na mahusiano na waalimu ambao hawataki kupewa matokeo ya chupi, waende wapi sasa? wapigania haki za binadamu pia ingilieni hili.

2. Waalimu wanafanya ngono na wanafunzi wa kike hadi wanagombaniana. Hakuna maadili

3. Futilia mbali waalimu wabovu na wa kuazima, hawakisaidii chuo.

4. Mkuu wa chuo hana nguvu wala maamuzi dhidi ya waalimu au wanafunzi. hadi wanafunzi tunajua ugumvi wa kimapenzi kati ya waalimu kugombania mabinti wa kike na kuvujisha mitihani lakini hakuna hatua zinachukuliwa.
 
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri anayehusika. TANESCO ni moja kati ya MAJANGA makubwa kabisa ya kitaifa. Jambo dogo tu la kutumia dakika chache tu kulitatua unaweza ukafuatilia TANESCO hata zaidi ya majuma kadhaa.
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuwasaidia watanznia wa kipato cha chini katika eneo hili, naomba nchi yetu iwe na Mashirika ya usambazaji umeme zaidi ya mawili.
Hiyo itakuwa ni dawa pekee itakayowakomboa watanzania wengi kutoka katika Janga kuu hili la TANESCO.
Kutoka Makambako, Njombe.
 
Kuna wafanyakazi wa TANROADS wanakuwa na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya Msata - Bagamoyo mida ya usiku, wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.

Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.

Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi.

utaifakwanza
Wanatutesa sana hao na tipper zetu za mchanga ndio mtaji wao mkubwa
Asante sana sana mkuu.hii ni taarifa muhimu sana. Hatua zitachukuliwa haraka sana. Na je mkuu Huwezi kupata namba za hiyo hardbody? Ili kurahisishia mamlaka husika kutumbua.

Mkuu hao jamaa ni maarufu sana hio njia ya Bagamoyo nadhani hawatumii gari moja kwa kuogopa kujulikana, mimi nina magari yangu ya mchanga njia hio madereva wangu wananambia hawawezi kuniletea hesabu bila kuwatoa wao kwanza, hawakamati gari zote ujue kuna baadhi ya gari wanazokusanya hesabu hizo huwa haziguswagi.Hawa jamaa ni cancer kwenye jipu walishavukaga kitambo tu,watumbuliwe tu hamna namna.
Mkuu
 
Daisam kwa mawazo yangu mkoa wa Njombe kuna Mkuu wa Mkoa, Meneja Tanesco wa Mkoa, kuna Mbunge, Kuna Diwani, hivi hakika matatizo hayo ni ya kupelekwa kwa Rais, una maana hao viongozi hawapo, tunatumia nafasi ya Rais vibaya mno, au tuseme mtiririko wa uongozi ki Mkoa hufahamu, nafikiri ndiyo sababu umeshindwa kutatuliwa tatizo lako hilo, hebu jipange.
 
Wana JF; naomba ukiamua kuchangia hapa uwe na constructive criticism (atakaependa na anaetaka kusifia nae anakaribishwa) kwa sharti moja: UJE NA USHAHIDI WENYE TAKWIMU.

Kwenu viongozi wa serikali na CCM mliomo humu nanyi naomba mtupe maelezo sahihi (ukileta maelezo kuwa mbuzi ni sawa na kondoo kwa kuwa huchungwa pamoja mimi binafsi sitasita kukupa my honest opinion however you hate it).

Naanza na suala la elimu:
Professor Ndalichako na wenzio; logic ya kuzuia waalimu kutoka nje ya nchi kufundisha hapa nchini kwetu ni nini? Tuzingatie facts zifuatazo:
1. Hao waalimu kutoka nje mara nyingi wanahitajika na shule binafsi, hawalipwi na serikali na wanalipiwa work permits na kulipa kodi (PAYE).
2. Shule binafsi hazisaidiwi kwa namna yeyote na serikali, kwa mantiki hiyo wenye shule hizo wanabeba mzigo wote kabisa (100%) ikiwemo gharama za utashi wao wa kutaka kuajiri waalimu wa nje (na hakuna mtu binafsi alie tayari kulipa Shilingi 10 badala ya Shilingi 2 kupata kitu chenye ubora ule ule). Kuna logic gani kuwazuia kutumia resources wazitakazo?

Niishie hapa kwa sasa.
 
Back
Top Bottom