Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Mhasibu/karani wa mahakama ya mwanzo sinza anaomba rushwa waziwazi kushughulikia mirathi! Keshawatapeli watu wengi kwenye mirathi! Ofisini haonekani amekuwa kama Nguchiro!
CC:Takukuru
CC: waziri wa sheria na katiba
CC:Jaji mkuu
CC: RC Dar
CC: DC Ubungo
 
Mhasibu/karani wa mahakama ya mwanzo sinza anaomba rushwa waziwazi kushughulikia mirathi! Keshawatapeli watu wengi kwenye mirathi! Ofisini haonekani amekuwa kama Nguchiro!
CC:Takukuru
CC: waziri wa sheria na katiba
CC:Jaji mkuu
CC: RC Dar
CC: DC Ubungo
 
Nimefurahi kwa kauli yenu. Mimi naomba mnielekeze zilipo ofisi zenu nije nisimulie na niwakabidhi nakala za vielelezo ili muandike na kuwasilisha huko mnakodhani zitashughulikiwa, maana nikisema niandike mimi ni marefu na nitakumbuka machungu yaliyokwisha nipata, na Mhe. Rais kwa kushauriwa vibaya akapigilia msumari wa moto.
 
KERO AMBAYO BADO HAIJAMPATA MTU WA KUIMALIZA, NI VIBENKI (taasisi za kukopesha watumishi) HAWATOI BALLANCE ILI WALIPWE DENI LAO, KWA KUOGOPA KUPOTEZA MTEJA. HUU NI UHUNI MKOPAJI ANA MALENGO YAKE, ALAFU MTU KWA MASLAHI YAKE ANAMDIDIMIZA ZAIDI.

Mfano "MABOTO ENT" ndiyo vinara katika hili.
USHAURI:SERIKALI KUPITIA WAKURUGENZI / MAAFISA UTUMISHI WASAINI BARUA ZA KUOMBA BALANCE NA KUCHUKUA HATUA DANA DANA INAPOTOKEA. ILI KUSAIDIA WATUMISHI HATA KIDOGO CHAO WAKITUMIE KWA NATAKWA YAO WENYEWE. UKANDAMIZAJI HUU NI HATARI KWA TAIFA.
 
HALMASHAURI YA MJI KASULU.

Kipindi cha mitihani ya taifa hasa kidato cha 2 na 4 maafisa wanafanya ufisadi kwa kuwakata hela waalimu fedha zao za usimamizi. Yaani huwa wanawakatisha waalimu wasiendelee kusimamia na kumuacha msimamizi mkuu pekeake.
Sasa sijui hiyo hela wanayoikata wanairudisha Hazina/ serikalini au la!
Wanaohusika fuatilieni halmashauri hii Yaani Hawana hofu ya kutumbuliwa hawa jamaa, ni kupiga hela tu.
 
Mwanza maeneo ya Igogo Mchafukoga na Sahara kuna watu wanamiliki TANESCO zao kwa kuiba umeme wa Tanesco waliojiunganishia bila mita na wao huusambazaajumbani na kila mwezi wateja wao huwalipa shilingi 10,000 bila kujali wametumia kiasi gani maana hakuna mita. Tanesco Mwanza wanajua lakini kwa vile mgap unawafikia na wao,hakuna mtu wa kufuatilia jambo hilo maana linawaneemesha pia
 
Hongera kwa kazi, mheshimiwa Waziri wa Nishati na madini.
Kwa niaba ya wakazi wa mtaa wa ILANGAMOTO uliopo katika Kata ya LYAMKENA, Halmashauri ya Mji wa MAKAMBAKO Mkoa wa NJOMBE, naomba utusaidie kupata huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya mtaa huu.
Ni miaka mingi imepita sasa tangu tulipoanza kufuatilia umeme TANESCO.
Miaka yote tumekuwa tukiambiwa kuwa tusubiri Bajeti, Bajeti ikitoka tunaambiwa hawajapata fedha. Kutoka ilipopita Line ya umeme hadi kwenye makazi yetu kwa eneo letu hili ni umbali usiozidi Nguzo 4 tu.
NB:-Mimi nazungumzia eneo dogo ndani ya ubalozi mmoja. Eneo hili halizidi Kaya 25 zinazokaribiana sana kiasi kwamba nguzo moja inaweza kusambaza umeme hata Kaya 4.
Tunaomba utupe upendeleo wa fedha kiasi ili TANESCO waweze kutusambazia huduma hii.
Kwa ufafanuzi zaidi, wasiliana na Meneja wa TANESCO.
Ahsante sana.
 
JAMANI HAPO MANISPAA YA KINONDONI IDARA YA ARDHI NA MIPANGO MIJI WAZIRI LUKUVI NJOO HUKU TUKUA BIE WATUMISHI WAKO WANATUFANYAJE WANAANCHI.. HERI MADIWANI MAANA KWA SASA HALI NI TETE
 
Salaam, kero yangu ni kuhusu kutopewa wa Umeme wa REA kwenye kitongoji cha KIJUKA kijiji cha Mabuye wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera. Kitongoji hiki kina kila sifa ya kupatiwa Huduma hii lakini imeshindikana na baadala yake Huduma hii imepelekwa kwenye vijiji vilivyo kizunguka na kwenye baadhi ya vitongoji vilivyobaki lakini chenyewe hakina. Aidha hali hii imetokana na uwepo wa Mtendaji wa kijiji cha Mabuye ambaye hawajibiki vizuri pia. Mwanzoni tuliambiwa kuwa kitongoji hiki kimepewa transfoma moja hivyo kitapata umeme lakini la kushangaza ni kwamba sasa hivi hiyo transfoma haipo tena imepelekwa kwingine. Tumepeleka malalamiko yetu sehemu mbalimbali juu ya hili na tunahaidiwa kusaidiwa lakini hakuna msaada wowote hadi leo.Vilevile tuliwahi kuambiwa kuwa mkandarasi anyeshughulika na maeneo haya kusambaza umeme wa REA anasubiri kupewa ramani ya Kitongoji hiki ili aanze kazi lakini mwaka umepinduka sasa hakuna kinacho endelea. Pia haya yote yanachagizwa na michezo michafu inayochezwa na baadhi ya viongozi akiwemo Mtendaji wa kijiji Mabuye. Suala hili natamani limfikie kiongozi mwenye dhamana juu ya hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna mtu alishajibiwa kero yake hapa? Ama tunajifurahisha tu kutoa hoja?
 
Anayeiongoza taasisi ya "URAIS" analitia hasara taifa.
Ashauriwe ajiuzulu kwa maslahi ya taifa.
 
Jibu kubwa ni ulaji wa pesa za Elimu Bure. 1. Kuna manunuzi hewa na 2. Bei zilizoongezwa. Tangia 2016 luzuku ya elimu Bure ianze kwa shule za sekondari na msingi, Hakuna ukaguzi wa maana kuhusu matumizi ya fedha hizo. Kemikali hewa, bei za wino, karatasi na chaki
 
Namhurumia sana MAGUFULI, kwa jinsi anavyohangaika kutuletea maendeleo harafu majitu mengine yapo ofisi nyeti za wakuu wa wilaya, takukuru, usalama wa taifa, polisi na ofisi nyingine ndo wanaongoza kufanya ufisadi na kuleta umaskini kwenye wilaya hizo. Rais Magufuli weka hata email hadharani yako tuwe tunakutumia madudu yanayofanywa na hawa viongozi unaowaamini.

Hatuwezi kuja kukuletea maovu haya kwenye ofisi za ikulu process ni ndefu Sana. Mzee Magufuli amini tu kuna wananchi wazalendo wanashindwa kukuwasilishia maovu ya wateule na maafisa wako wapiga dili....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habarini,

Uzi huu uwe spesho kwa wale wenye maoni, maendeleo,hata mapovu na changamoto mbalimbali tunazokutana nazo sisi kama watanzania katika Jamii zetu kila siku.

mimi naanza na Pongezi Kubwa kwa maendeleo nnayoyaona katika nchi yetu na katika jamii inayonizunguka kwani mambo yanaenda na yanaenda vizuri.. maoni yangu kwa jamii tuzidi kuchapa kazi ili tupate maendeleo yetu binafsi na nchi kwa ujumla..
 
Rushwa uteuzi wa maafisa Elimu. Ni kati ya mil 5 hadi 10 ili uteuliwe Afisa Elimu Tanzania. Matokeo yake maafisa Elimu wengi hawawezi kusimamia Elimu, huonekana mashuleni kusindikiza mitihani tu. Hakuna mipango wala mikakati kuinua Elimu. Nao wanauza ukuu wa shule ili kurejesha mtaji wao. Mfumo wa uteuzi ubadilishwe. Nafasi zitangazwe, washindanishwe kisha watakaofuzu ndio wateuliwe
Namhurumia sana MAGUFULI, kwa jinsi anavyohangaika kutuletea maendeleo harafu majitu mengine yapo ofisi nyeti za wakuu wa wilaya, takukuru, usalama wa taifa, polisi na ofisi nyingine ndo wanaongoza kufanya ufisadi na kuleta umaskini kwenye wilaya hizo. Rais Magufuli weka hata email hadharani yako tuwe tunakutumia madudu yanayofanywa na hawa viongozi unaowaamini.

Hatuwezi kuja kukuletea maovu haya kwenye ofisi za ikulu process ni ndefu Sana. Mzee Magufuli amini tu kuna wananchi wazalendo wanashindwa kukuwasilishia maovu ya wateule na maafisa wako wapiga dili....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habarini,

Uzi huu uwe spesho kwa wale wenye maoni, maendeleo,hata mapovu na changamoto mbalimbali tunazokutana nazo sisi kama watanzania katika Jamii zetu kila siku.

mimi naanza na Pongezi Kubwa kwa maendeleo nnayoyaona katika nchi yetu na katika jamii inayonizunguka kwani mambo yanaenda na yanaenda vizuri.. maoni yangu kwa jamii tuzidi kuchapa kazi ili tupate maendeleo yetu binafsi na nchi kwa ujumla..
Elimu elimu elimu ....lowasa alisema hii kauli ina Maana kubwa sana,..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia. Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100. Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.

Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.
sasa bosi iyo kampuni jina lake inauitwaje mbona taarifa fupi fupi
watajie ao mamlaka husika watusaidie maana hili nalo ni jipu tena ni balaa
 
Back
Top Bottom