Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

HII HAPA RUSHWA KUBWA NCHI NZIMA!!

-Wakuu, maafisa elimu sekondari wamekua wakizoea kutoza rushwa kwa walimu ili wapewe nafasi yankusimamia mitihani ya taifa. Hili linafahamika. Hii imekua ikipelekea hata kuwapitisha wasimamizi wasio na sifa kisa tu wametoa hela. Iko hivi: kusimamia kwa siku 10 mfano kama kila siku ni 50000 lazima utoe laki mbili kwa afisa elimu ndo upitishwe.

-Mimi nilitoa taarifa hii kwa afisa mmoja wa takukuru akaahid kufanyia kazi mpaka leo hajafanyia kazi. Nikaamua kufuatilia kujua ni kwann suala hili halikufanyiwa kazi, nikagundua kua afisa huyu wa elimu ni rafik mkubwa na afisa huyu wa takukuru.
Me nishauri tu mamlaka ya takukuru wafuatilie kesi hizi na kuchunguza watumishi wao maana wengine ni mizigo kwa wanachi wanaojitoa kupambana na ufisadi.

-Rais wetu amejitahidi kupambana na rushwa kubwa kwenye ngazi za juu lakini ngazi za chini bado sana , kuna watumishi wa takukuru wanatukwamisha

-maafisa elimu kwa kujua au kutojua wanapokea rushwa wakifikiri kumpitisha mwalimu kusimamia mtihani ni jambo ambalo wanaamua watakavyo. Kwa kawaida kuna utaratibu maalumu ambao upo na unatakiwa ufuatwe ili kutenda haki kwa walimu wote wenye sifa za kusimamia mtihani.

Niko tayar kutoa ushirikiano kwa hili kama wahusika wa takukuru wapo hapa
 
Kero kubwa Sana Kwa wananchi ni jeshi la polisi hasa kwenye kesi za madai, wanaiwa nawanadai wakati wote wanakuwa wahanga wa polisi kutoa rushwa,jambo muhimu hapo ni mahakama Kuwa na uwakilishi kwenye eneo hilo, hilo eneo lina rushwa sana, mtu akiwekwa ndani lazima wanao weka dhamana wawe na pesa bila pesa ni ngumu Sana mtu kupata dhama kitu ambacho ni haki yake ya msingi
 
HII HAPA RUSHWA KUBWA NCHI NZIMA!!

-Wakuu, maafisa elimu sekondari wamekua wakizoea kutoza rushwa kwa walimu ili wapewe nafasi yankusimamia mitihani ya taifa. Hili linafahamika. Hii imekua ikipelekea hata kuwapitisha wasimamizi wasio na sifa kisa tu wametoa hela. Iko hivi: kusimamia kwa siku 10 mfano kama kila siku ni 50000 lazima utoe laki mbili kwa afisa elimu ndo upitishwe.

-Mimi nilitoa taarifa hii kwa afisa mmoja wa takukuru akaahid kufanyia kazi mpaka leo hajafanyia kazi. Nikaamua kufuatilia kujua ni kwann suala hili halikufanyiwa kazi, nikagundua kua afisa huyu wa elimu ni rafik mkubwa na afisa huyu wa takukuru.
Me nishauri tu mamlaka ya takukuru wafuatilie kesi hizi na kuchunguza watumishi wao maana wengine ni mizigo kwa wanachi wanaojitoa kupambana na ufisadi.

-Rais wetu amejitahidi kupambana na rushwa kubwa kwenye ngazi za juu lakini ngazi za chini bado sana , kuna watumishi wa takukuru wanatukwamisha

-maafisa elimu kwa kujua au kutojua wanapokea rushwa wakifikiri kumpitisha mwalimu kusimamia mtihani ni jambo ambalo wanaamua watakavyo. Kwa kawaida kuna utaratibu maalumu ambao upo na unatakiwa ufuatwe ili kutenda haki kwa walimu wote wenye sifa za kusimamia mtihani.

Niko tayar kutoa ushirikiano kwa hili kama wahusika wa takukuru wapo hapa
Kama kweli uko tayari kupambana na Rushwa ni jambo jema sana, shida kwenye andiko lako ni kwamba umewatuhumu maafisa Elimu wote nchini kwamba wanadai laki mbili kwa kila wanayemteua kusimamia mitihani, jambo ambalo naamini siyo kweli, ninachoweza kusema ni kwamba vitendo hivyo kweli vipi lakini siyo kwa wote, pia kwenye andiko lako umewatuhumu maafisa Takukuru wote nchini kwamba hawafuatilii na ni marafiki wa watumishi wa idara ya elimu, jambo ambalo siyo kweli, sasa naomba nikushauri na kama ni kweli ulitendewa haya naamini utafuata ushauri huu ili mamlaka zifanye kazi na kuchukua hatua stahiki;
1. Andika Namba yako ya Simu hapa
2. Andika jina la shule unayofundisha
3. Andika jina la Wilaya yako
4. Usiwe uatoa tuhumu za jumla
 
GES ltd for cheapest and affordable clearing and forwarding your cargo DAR ES SALAAM 0717267636
 
Habari wandugu, ni kero wazee jamaa wanahudumia MTU mmoja nusu SAA ,kuna folen ya watu 20 sasa wanafikiri hatuna majukumu mengine Pambafuu zao
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
We unahsi haijulikani kwamba watu wantoa na kuppokea rushwa? Na unahsi watoa rushwa na wpokea rushwa hawjulikani?
 
Kama kweli uko tayari kupambana na Rushwa ni jambo jema sana, shida kwenye andiko lako ni kwamba umewatuhumu maafisa Elimu wote nchini kwamba wanadai laki mbili kwa kila wanayemteua kusimamia mitihani, jambo ambalo naamini siyo kweli, ninachoweza kusema ni kwamba vitendo hivyo kweli vipi lakini siyo kwa wote, pia kwenye andiko lako umewatuhumu maafisa Takukuru wote nchini kwamba hawafuatilii na ni marafiki wa watumishi wa idara ya elimu, jambo ambalo siyo kweli, sasa naomba nikushauri na kama ni kweli ulitendewa haya naamini utafuata ushauri huu ili mamlaka zifanye kazi na kuchukua hatua stahiki;
1. Andika Namba yako ya Simu hapa
2. Andika jina la shule unayofundisha
3. Andika jina la Wilaya yako
4. Usiwe uatoa tuhumu za jumla
Mkuu ushauri wako ni mzuri. Lakini kuna kitu kinaitwa privacy of the informer. Hili ni la msingi hata sheria ya takukuru imeliweka. Sasa unavotaka niweke taarifa zangu hadharani kama ulivoelekeza ushaur huo ninaukataa kwa mujibu wa sheria ya takukuru ya mwaka 2009.
- aidha naweza kusahihisha kwamba sio maafisa elimu wote wanaopokea rushwa lakini ni wengi wakiwemo na wilaya kwangu mimi.
- pia sio maafisa takukuru wote wenye urafiki na maafisa elim. Lakin hili ni dhahir kua maafisa takukuru wengi ni marafik wa wakuu wa idara wengi tena sio idara ya elimu tu. Hili suala limekua ni changamoto kwa takukuru tangu siku nyingi. Hata ukifuatilia ripoti ya LHRC ya mwaka 2012 na 2013 zinaonyesha kwa namna moja au nyingine takukuru ngaz za chini walikua wanajihusisha na vitendo vya rushwa au kuminywa kwa haki za watu kutokana na kupuuza taarifa zinazotolewa za vitendo vya rushwa.
- na kwenye hili mimi nilihusisha takukuru na naongea kitu ambacho nina experience nacho. Naomba waniwie radhi sio wote ika kwa wilaya yangu nina ushahid.

- wenye mamlaka ya kufuatilia suala hili wanitafute inbox sio kunishaur niweke contact hapa. Anayenishaur hivo atakua sio mwenye mamlaka hayo au sheria hata ya takukuru haijui na mimi nitampuuza
 
Nimefuatilia kwa kina tuhuma ulizozitoa na nimekufuatia wewe binafsi, nimejiridha pasipo shaka kwamba wewe mpenda majungu, hakuna taarifa kama hizo, Takukuru ngazi ya Wilaya siyo kweli kabisa kwamba wanavuruga ushahidi wa kesi ndani ya Wilaya, au hata kujihusisha na rushwa, kwani huna ushahidi hata mmoja ambao unaonesha kutoka Wilaya yako wa kesi zinazowahusisha Takukuru kushitakiwa kwa kupokea na kuomba rushwa, hivyo wewe binafsi ni mpenda majungu, madai kwamba unaheshimu usiri wa mtoa taarifa, hauna msingi, sasa mbona Mimi nimekufuatilia na kujua historia yako wewe, umesoma wapi, Wazazi wako, na unafanya nini. Nakushauri kwamba usipende kuchafua watu na Taasisi nyeti za Serikali. Kuna siku utasaidia kutoa ushahidi. Hakuna haja ya kufuatwa inbox, bali humu humu kama wewe ulivyofanya.
 
Kitendo cha police kusherekea na Makonda kimedhihirisha kuwa Police wote ni CCM na ni vibaraka wa CCM na wanatumiwa na ccm
 
Naichukia sana CCM kwa kuwekeza pesa nyingi kwenye kununua watu Huku wakiacha watu wanaangamia kwa uzembe wa viongozi tena kwa kukosa huduma muhimu na kitendo kunyang'anya kura za wananchi
 
nashauri serikali ifanye namba ya 911 iwe ndo ya kutoa taarifa, za uhalifu, kupotea watu na mambo mengi ya kusaidia upelelezi.
 
serikali ya nchi hii imeshapoteza uaminifu kwa raia wake mkuu ... wala usihangaike
 
Namba ya dharura ipo ila ni watanzania wachache wanayoijua!Hata mimi mwenyewe siijui!
Sasa nimeijua,ni 112!
 
Tanesco Kisarawe ni jipu hasa idara ya upimaji mimi mkaz wa buyuni kwa masister tangubmwezi wa sita nahangaika kupata umeme nimeleta form zangu wakaja wakapima na mimi wakanipimia mwez wa tisa mpaka leo form hazipo nashindwa kulipia jambo baya wanashirikiana na mtu kule buyuni kutuzungusha nimeandika lalamiko langu tangu mwez wa tisa hakuna majibu nifanyeje? Mh waziri nisaidie mimi sina rushwa yakutoa umeme uwake pale kwangu.
 
Jaffo aende Kilolo,pale pana uchaf mkubwa sana,wafanyakaz hawalipwi staik zao kwa wkt,walimu wanahamishwa,wanaenda likizo lkn pia n halmashaur yenye kibur sana kwa watumish wa chn,watu hawapandishwi madaraja kwa wkt ukidai hak zako wanakuwekea visas mara ooh hutapata special duty! nenda kilolo uone mafail ya wafanyakaz jins ambavyo hayana kumbukumbu zao! wanajilipa wao 2 pale posho za naul za likizo hasa walimu wanapata tabu sana!
 
Habar wana wanajamvi?

Kwa kuwa Jf ni platform kubwa nchini na imechangia kwa kiasi kikubwa sanaa serikali kupata Taarifa mbali mbali sasa binafsi nmeona ni vyema sasa wanajf tuwe na uzi special kabsa wa kumtajia wateule wake wanavyo mwaangusha!

Kupia eneo ili endapo mwana jf utaenda kwenye ofisi ya umma na ukakosa huduma kwa sababu ya ngiriba za viongozi wetu tafadhali kupitia hapa mtaje aliyekufanyia ngiriba hizo mpk ukakosa huduma!

Umeenda kwa mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya?mkurigenzi au mtendaji yoyote ukakosa huduma kisa ni rushwa au ngiriba mshenzi tafadhali aliyekufanyia hivyo wewe kazi yako n ndogo tu mfyekeleee mbali humu ndani

Mimi naanza na aliyekuwa Waziri wa kilimo Charles Tizeba kiukweli sikuwah kumwelewa maana alipewa wizara ambayo hakuwa na uelewa nayo nashukuru katumbuliwa.

Je nani mwingine???????

Tililika hapa chini mtaje mtu weka na ushaidi.
 
58 Reactions
Reply
Back
Top Bottom