Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Kuna magari kama 50 hivi ya kenya ya beba udongo kila siku kupita hapa Monduli, sijui kutoka wapi na kupeleka Kenya.

Niliambiwa ni madini na wanayahamisha yote Kenya, Tanzania itakapo amka hawana kitu. Kumbukni tanzanite, na hasa Almasi ya Mwadui wakati wa De bear ile kampuni ya Afrika Kusini ili hamisha na kuchimba kila sehemu ambapo ina patikana, enzi za baba wa ufisadi ze kapa.

Mwenye taarifa kamili atujuze
 
Jipu uchungu lingine lipo pale wilaya ya Chamwino tena hili nimpelekee moja kwa moja kamanda wa Usalama barabarani, Kamanda Mpinga.

Kuna kamanda wa barabarani pale wa Wilaya ya Chamwino yeye ndiye kinara wa kuvunja sheria za barabarani baada ya kunikamata swala motor vehicle license nikagundua kumbe yeye gari yake aina ya Suzuki Swift ya kijivu T 613 CRG hajalipia motor vehicle tangu tar18/11/2014 mpaka leo hii.

Kwahiyo anadaiwa na serikali takribani 425,000/- nikagundua kumbe mkuki kwa raia kwa trafiki mchungu.

Naamini DTO Chamwino ni jipu tu kama majipu mengine juzi kati vijana wake walikamatwa na kashfa fulani ya barabarani lakini tuseme ukweli DTO ndiye master mwenyewe wa michezo ile tukushuru kamanda Misime kwa umakini ila ondoa huyu DTO methew anakuchafua.
 
jipu lingine ni matumizi yasiyo wazi ya fedha za elimu bure namwomba magu aweke ahakikishe watendaji wa elimu wanatumia hiyo pesa kwa uwazi ili umma ujue kinachoendelea.

Pia serikali iache kutumia wazabuni kwa vitu vidogo vinginevyo ni kuendeleza wizi na upotevu wa mali za umma....
 
kadendu

Cha ajabu kuna eneo ambalo trafiki pale Chamwino(Buigiri) wansimama(point) na Mathew ndipo anaposimama kuanzia Dec mpaka leo wamekwishakufa kwa kugongwa raia zaidi ya 7 na kupelekea ugomvi mkubwa na wanakijiji hapo mpaka vijana kupelekwa mahakamani.

Ni eneo la kwenda speed 50 sababu ni eneo la makazi ya watu lakini madereva wanapita na speed watakazo bora uwe na mshiko hivyo imepelekea vifo vya watu wengi kwa muda mfupi katika eneo hili najiridhisha DTO wa eneo la chamwino pamoja na kushinda barabarani muda wote ni jipu linalostahili kutumbuliwa maana limeiva muuda.
 
bodi ya mikopo kwa elimu ya juu jamani hawa jamaa ni wezi vibaya sana, nina mkopo mwaka wa pili sasa but sijapewa bumu tatu, na kila ukiwafuata wanakwambia rudi chuo muhasibu (loan officer)wako ndio alete taarifa zako, tusaidieni jaman tunateseka na hatujui wapi pakukimbilia.
 
Kuna hawa jamaa wanajiita DMI(DAUGHTER OF MARRY IMMACULATE AND COLLABORATOR) wanamiliki shule nyingi za St. Joseph University pamoja na vyuo vyake vikuu.

Kimtazamo wangu hawa jamaa wamekuja kuchuma pesa and we must watch out,kwasababu janga watakalo tuacha nalo ni kubwa na sidhani kama nchi inafuatilia,hawa jamaa wamejikita kwenye elimu kuanzia shule za upili mpaka vyuo vikuu lakini kitu kinachofanyika huko mashuleni na vyuoni sijui hata nielezee vipi.

Ninachoomba ni kwamba nchi iliangalie hili suala kwa jicho la tatu, hawa jamaa watatuachia matatizo makubwa sana,mfano sakata kubwa juzi lilitokea miongoni mwa vyuo vyao kuhusiana na wahadhiri wa vyuo wasio na vigezo, suala ambalo ni kweli nimelifanyia research ni kweli.

Yaani, chuo kinatoa degree za ualimu katika masomo yote ya sayansi pamoja na hisabati lakini hakina mhadhiri hata mmoja aliye na vigezo, watu wanafundishwa na wahadhiri wenye Diploma na Degree, mtu ambae kidogo alikuwa amesoma alikuwa ni Mr JOSEPHAT ambae kwa sasa hayupo wameshashindwa na na wahindi na alikuwa na master katika hesabu.

Kwa ufupi, tunaomba mtusaidie sana nchi itaangamia.
 
Any university is said to be the source of interlectuals but kulingana na mfumo wa elimu unaoendeshwa na hawa jamaa,wanafanya mambo kinyume yake.

Kuna kitu nakiona japo upeo wangu ni mdogo sana, AUTHORITATIVE EDUCATION SYSTEM. Huu ni mfumo wa elimu usioruhusu demokrasia katika upatikanaji wake unapokea kama unavyopewa hakuna kuhoji.

Kwa ufupi wahindi wanawakaririsha wanafunzi majibu ya maswali na endapo tu utafanya vile unavyojua wewe utafeli sana, usipohudhuria darasani hata kama unajua yaliyofundishwa kuliko waliokuwepo kwenye kipindi utafeli tu.

Liangalieni hili suala jamani kizazi kijacho kitaangamia.
 
Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
Hili sio jipu baya ni jipu faida linawasaidia kupata kipato cha hapa na pale. Walimu wanamaisha duni sana.
 
Jipu mishahara ya wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma wenye level moja ya elimu kutokulingana ni jipu uchungu sana.

Mfano, Mwl. wa degree serikalini mshahara wake haulingani na wa mfanyakazi wa NSSF au TRA mwenye degree moja.

Hili jipu, kwanini halitumbuliwi?
 
Nadhani ipo haja kuwa na mfumo rasmi kwa kila wizara ambao utatumika kupokea kero za wananchi na majibu kutolewa kupitia mfumo huohuo.

Kwa utaratibu huohuo, tovuti ya serikali na JF viwe vitovu vya kuifikia mifumo ya Wizara hizo, hii itasaidia kubaini mapungufu na mafanikio katika utendaji wa watumishi wa serikali
 
Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia
Aisee umegusa penyewe. Jamaa wanaisaliti nchi kwa tamaa ya 'peanut money' afu wangejua sasa wageni wakwepa vibali wanavyowadharau.... wakipewa buku 20 tu wanatulia, njaa kama nini sijui.

Wanaboa kichizi, ukiwa unakwenda kwa Magufuli aisee nistue twende wote maana nina list ya wengi sana wanaoiba kazi zetu.
 
Kuna jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi halijakamilika kwa miaka mitano lina ghorofa takriban sita, cha kushangaza wameanza kujenga kaofisi kengine pembeni.

Huyu Waziri aanze kwake na sio anasumbua watu wengine kwenye idara yake bado kuna madudu!

NB: Jengo hili limejificha mkabala na jengo la Posta
 
Kuna uwanja uko Mwananyama unaitwa Garden, ni uwanja wa wazi ila kuna watu wamejenga nyumba na kuna hall la sherehe.

Serikali ilitaka kupavunja muda mrefu lakini wameshindwa kisa kuna ndugu yake Sumaye ndo kikwazo na kuna watu wamejimilikisha kama kwa baba zao wanakataza hadi watoto kucheza kisa wao wachimbe mchanga na kujaza takataka.

Nawasilisha mkuu
 
Napendekeza JF pawe na permanent thread au jukwaa maalumu ambalo wananchi au members wa JF wenye taarifa za jambo lolote ambazo tunadhani kwamba zinaweza ama kufichua uovu fulani au kuisaidia serikali yetu kuondoa majipu basi ziwe zinawekwa hapo ili iwe rahisi kwa serikali na wahusika kuzisoma na hata ikibidi kuzitendea kazi na ikibidi waje kuzitolea feedback hapa JF na kama sio basi walao kwenye reliable media outlets.

Jambo hili litasaidia wengi kwani kuna watu wana taarifa nyeti nyingi tu, lakini kila mtu hawajui pa kuzipeleka au anazitupa tu kokote kule. Lakini tukiwa na kitu kama hicho hapa JF kwanza kitaiongezea JF heshima yake kwa jamii na serikali yetu pia zaidi ya hayo jambo hili litakuwa faida yetu sote wasomaji kufumbuana macho.

Maana hayo masanduku ya maoni kwenye ofisi za serikali hata sijui nani huwa anafungua na kama yanasomwa sijui hata kama wanayatendea kazi. Lakini hapa wanaopita ni wengi lazima wataingiwa na soni tu. Boss kama kaficha, wako wengine wataona na lazima huko kwenye ofisi zao watajadili na watasema tu kwamba jamani eeh huko JF mmeona tumelipuliwa?

Huu ni mtizamo wangu tu, kila mtu anaweza changia apendavyo kwa namna ya kujenga na si kubomoa tafadhali!
 
Majipu yangu ni urasimu kwenye ofisi za watendaji na serikali za mtaa.

Kumekuwa na ucheleweshaji wa huduma kwa wananchi pasipo sababu za msingi. Hawa watu waajiriwe na wasiwe watu madalali na matapeli.

Kwanini serikali za mtaa zote zina watu matapelitapeli na ma broker?
 
Mimi naomba ufatilie kesi ya madai no 31 ya mwaka 2001 - Joyce John vs Maguzu Masanja....

Yaani kesi ya mwaka 2001 hadi leo haijaisha..... kibaya zaidi Maguzu anamtumia Mkuu wa Wilaya kuzuia utekelezaji wa shauri hilo. Utekelezwaji wa hukumu hiyo ulitakiwa kufanyika mwaka 2003 baada ya Mahakama Kuu kuamuru Joyce apewe haki zake lakini mpaka sasa umekwama.

Kwa kweli hapa kuna mazingira ya rushwa kabisa....
 
TANESCO Mwanza ni jipu kubwa wanakata mno umeme kinachoendelea ni hujuma kwa Serikali ionekane haifanyi kazi.

Nafasi za kazi serikalini zilizohamishiwa Halmashauli ni shidaaa, wamagawiana tu.

Naiomba serikali izirudishe utumishi wa umma watoto wa maskini tupate ajira
 
Kwenye Kampuni za MOHAMED INTERPRISES Kuna Wahindi Hawana Vibali wanajificha kwenye MAGODOWN VYOONI lakini usiku wanatembea kama kawaida
 
TRA mko wapi na hii mimashine yenu? Wafanyabiashara Kariakoo hasa wahindi ukienda kununua vitu kwa mfano ukitoa laki kununua vitu utaandikiwa risti ya elfu ishirini
 
Back
Top Bottom