Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Mwambieni huyo a atoe ajira, aruhusu kuhama , apandishe madaraja na alipe stahiki za wafanyakazi
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious
Nitaamini kwa kuwa viongozi wote aina ya makonda watashika adabu , hatutaki kuona tunaonewa au kunyanyaswa kwenye nchi yetu na kikundi Cha watu wachache. Kumbuka furaha na Amani ni zaidi ya Pesa.
 
ali
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu

!Alichaguliwa na nani kwanza! nisije jibu swali lisilo nihusu
 
Aache kudili na wapinzani na kupiga piga simu zisizo na mpango kwenye vituo vya redio na kudharirisha watu mbere za alaiki za watu na aache sifa za kijinga na pia asiwe na upendereo .ajenge nchi .Mjomba wallahi ukiwa huku nje ya nchi ndio utajuwa kwamba Tanzania bado sana na tupo usingizini .wallahi Mjomba inauma sana nchi yetu tajiri lakini bado na kama sasa tunaye raisi asiyejierewa kazi kudharirisha watu OK umemtumbua lakini nchi yetu umeifanyia nn
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Kumpeleka mahakaman RC Wa DSM kwa tuhuma zinazo mkabili.
 
... Let's be honest, yaani wewe unaona ni sawa kuwa na kiongozi ambaye amefanya udanganyifu kuhusu elimu yake? Huyu atakuwaje na moral authority Kukemea wenzake kama alivyosema mukulu??
Alafu ndio watunga SHERIA!say no to criminal
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
kuangalia shilawadu
 
Aruhusu ajira kwa kundi ambalo ni kubwa sana la walimu na madaktar japo nusu ili watakao baki wapate huko private
 
Naomba Mheshimiwa Rais Magufuli au waziri wa nishati Bwana Muhongo atakapokuja huku Makambako atusaidie suala la UMEME hasa katika mtaa wa Ilangamoto na mitaa mingine. Tangu mwaka 2014 tuliandikisha kwa ajili ya kupata UMEME wa REA lakini mpaka sasa hakuna konachoendelea. Juhudi za ufuatiliaji zimefanyika lakini mpaka sasa hazijazaa matunda. TUNAOMBA KUSAIDIWA KATIKA HILO. Ahsante.
 
Sikatai kuongezewa mishahara kwa watumishivwengine lakini swala hili limebase ni kwa kiasi gani hiyo sector au sehemu directly inachangiaje katika uchumi wa nchi na unyeti wa kazi zake.sasa leo hii na hadle trilions za wananchi na serekali unilipe lak5 au6 kama mwalimu.haitakaa iwezekane mkuu
Mkuu kila kazi inauzito wake, fikiria watu wanao handle miradi ya mabilion, hawa unawaweka sehemu gan,? wao sio muhimu? mfano Mainjinia, Ma Afisa Manunuzi,Madaktari.
Kiukweli kila mtu sehemu alipo ana majukumu muhimu kumfanya pia mwenzake awepo pale.
Mfano TRA Akulipwa Mshahara mkubwa Afu Dokta analipwa Mshahara wa Kawaida unaona kunausawa hapo?
Nadhani dhana ya kuwa mtumishi wa umma iangaliwe hata katika usawa wa ngazi za Elimu na Sio kazi flani flan kuwa muhimu zaidi ya nyingine.
 
Habari zenu watanzania wenzangu na poleni katika kulijenga taifa letu pendwa. Ambalo bado lipo miongoni mwa mataifa yanayoendelea. Pia pole na pongezi kubwa zimuendee raisi wangu mpendwa Dk JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI kwa majukumu mazito ya kuilea familia yetu Tanzania kwa ukubwa wake na watu wake wengi tunaokadiriwa kufikia 54m. Watanzania wenye dini,kabila,itikadi,tabia,upendo,wapenda wizi,maovu,mema,wakwepa kodi,wajanja,wapiga dili,wauzao wanyama wetu,wanaohongwa na kuikubali miktaba isyo na maslahi ya taifa,wala rushwa,wasiopenda nchi yetu ikipga hatua,chuki,wacha Mungu na wacha shetani.
Naomba nisiwachoshe niende kwenye maada husika kabisa.

Mimi sio mwanauchumi ila ni mhandisi ujenzi, katika suala/sera yako ya Tanzania ya viwanda ni nzuri mtukufu raisi wetu mpendwa. Kuna kitu ningependa nikushauri kuwa ingekuwa bora na jambo la busara wazo kuu/kwanza/kipaumbele kuweka elimu mbele kwanza kwa vijana wetu wa kitanzania kwani wapo wenye uwezo mkubwa ila watu wa kuwatengeneza ndo hawapo mkuu. mfano mdogo kiukweli namshukuru Mungu nimesomea hizo shule wanazoziita za watoto wenye vipaji maalumu. Huko kuna vijana wenye uwezo mkubwa sana jamani darasani tusikatae wala kubisha, sasa hawa vijana wanakuwa wana ndoto kubwa sana maisha na zinakuja kuyeyukia vyuoni.
kitu cha kufanya ili tutimize ndoto yetu ya tanzania ya viwanda ni haya yafuatayo.

1--Wale vijana wanaofaulu vizuri sana kwa kupata daraja la 1 aidha kidato cha 4 au cha 6 wawe wanachukuliwa wanapewa mchujo/mtihani hata mara 3 wakiwa kama 500 wanachujwa mpaka tunawapata vijana 100 ambao wametokea mara mbili katika 100 bora. Sasa vijana hawa watachukuliwa na kupelekwa katika kambi maalumu wafunzwe uzalendo na wazalendo wetu watiifu walio tayari kuifia nchi yetu wapandikizwe chembechembe za kulipenda Taifa letu na wajue kuwa kuijenga Tanzania ni wajibu wao. pia kidogo wanapata na mafunzo ya kijeshi.

Nakuomba uiongeze hii kambi mana nakuona umepanua makambi ya jkt yamekuwa mengi. Kambi kama hii Russia, Usa Israel wanazo na tena hao vijana wanasikilizwa na kufanyiwa chochote wanachotaka kutoka katika Taifa lao. Baadaye vijana hawa wanachukuliwa na kupelekwa katika nchi wahisani,marafiki na sisi ili wasome na kujifunza mbinu mbalimbali za uhandisi wa iviwanda,namna ya kutengeneza bidhaa fulani ambayo tuna mpango wa kuizalisha hapa nchini, wajifunze namna ya kuyachimba hayo madini rejea jinsi Gadafi alivyowafanya mabeberu na wanyonyaji,wezi wa ulaya magharibi na marekani ambao huibia mataifa machanga na miktaba laghai ili siku tukiwafukuza tayari tuwe na watalaamu wetu pia na viwanda hatutahitaji utegemezi toka kwao.
Vijana hawa watakuwa wanasoma kwa vitendo zaidi ikiwezekana waingie katika viwanda huko uchina na kwingineko na wajifunze teknolojia tayari kuipandikiza hapa kwetu.

2--Nimeshuhudia vijana wenye uwezo mkubwa sana ambao wakiwezeshwa wanaweza kuisaidia nchi yetu na kufika mbali sana. Wazalendo wa kuwawandaa hawa vijana hawapo watu wanaangalia matumbo yao badala ya taifa mbele. Naomba uweke sera ya Tanzania kwanza na somo la uzalendo lifundishwe tokea shule za awali mpaka chuo kikuu.Lazima na vijana waipende nchi yao mana inauma kuona kijana ambaye angeweza kuijenga nchi yake anafurahia kupanda ndege kwenda nchi ulaya. Ulaya mababu wao walizijenga kwa jasho la damu na maji usiku na mchana na leo hii vizazi vyao wanaishi vizuri.
Hapa naomba pia hata walimu wawe na moyo wa ualimu maana wao ndo wanaweka mbegu na matunda na madhara yao yanatokea kwa wanafunzi wote (watanzania) sio wa kupuuzwa hata kidogo na ndo taifa letu ni matokeo ya walimu wetu.

3-- Ningeomba sekta ya elimu isidharauliwe na isiachwe nyuma na nguvu kubwa ielekee hapa maana ndo kila kitu. Watalaamu k.v madaktari,WAZALENDO,walimu,wahandisi,wanasheria nguli,wanauchumi,wapanga sera na mahusiano za kimataifa n.k wanatengenezwa hivyo Taifa letu ni matokeo ya walimu waliowafundisha na kuweka mbegu kwa wanafunzi watakaokuja kulitumikia baadaye.

Mwalimu asiwe yule aliyepata daraja la mwisho au makapi,mtu akafaulu kwa kubangaiza unadhani ataenda kuwafundisha nini Tanzania ya kesho. Ifanye sekta hii iwe nyeti kama TISS mana ndo Taifa lenyewe. Kusomea ualimu lazima mtahiniwa awe na daraja la 1/2. Motisha,mishahara,mazingira yao ya kazi,kuishi yawe mazuri ya kuwafanya wapende kazi yao pia lazima mwlimu apitie jkt kama zamani ilivyokuwa,kwanza sheria iwepo kuwa lazima kila akishafikisha umri wa miaka 18 apite jeshini huko ndo hata anapewa ID ya Taifa.

4--- Shule za ufundi ziongezwe karibu zote zigeuzwe polepole. Tutenge shule zetu watoto wanaopenda fani fulani au wenye kipaji fulani mfano Dodoma kuwe ni uhandisi magari, mtwara iwe kilimo,lindi iwe ujasiriamali,morogoro michezo,kigoma uhandisi majengo,kagera ufugaji,mwanza siasa,singida siasa,manyara umeme wa aina zote.

Sasa kutokea hizi shule ndo tunachukua vijana na kuwapeleka huko kwa wenzetu wajifunze mbinu ili baadaye waje kuwafundisha wengine ili tusitumie gharama kuwapeleka wengine nje. mfano umeme wa upepo Netherland wapo vizuri, umeme wa jua germany wapo, kilimo Israel wapo vizuri na viwanda china wapo vizuri.

Kama gharama inakuwa kubwa basi tunamchukua mtalaamu toka huko tunamlipa afundishe vijana wetu hapahapa.

5---Hawa vijana nina imani wakipikwa vizuri na wazalendo waliotukuka watakuwa na uwezo wa kusimamia kiwanda cha kusindika nyama,kutengeneza bidhaa za ngozi za ng'ombe,mbogamboga,juice, na kusafirisha matunda ya kiwango cha juu,asali safi na kuuza na bidhaa zetu zilizozalishwa hapa nchini na watanzania wenyewe.

6--- ukienda AIST-NM/ chuo cha Mandela naumia kuwaona vijana wa kikenya na wa kighana,kinigeria ndo wanaofundisha pale na chuo kipo kwetu. Eti watanzania hawapo wenye sifa ingawa vijana wapo ila wazalendo wa kuwaandaa ndo shida. Nakipongeza chuo hichi wameanza kuchukua vijana wanaofanya vizuri kidato cha 6 na kuwaandaa ili badaye wawe wahadhiri hapo chuoni. Hapa nakuomba uige mfano huu wa kuwandaa hawa vijana kuna mbinu nyingi zinaweza kutumika kuwapata hawa vijana watiifu walio tayari kulifia Taifa lao.

7-- Yaani ardhi tunayo nzuri sana tena sana jamani kwa watu ambao mmetembea mkaona wengine wanavyoishi katika ardhi zao mbaya ila bado wanalima mazao mazuri na wanauza nje ya nchi na kuongeza pato lao.

Hapa vijana wachukuliwe hata wawende Italy wajifunze kilimo cha matunda na namna ya kuyasindik/kuyafadhi ili yasafirishwe kwenda nje. Hivyo wakulima watalima kitalaamu hata kilimo cha umwagiliaji mana tutakuwa na umeme wa jua kama singida, tunajenga viwanda na watalaamu tunao watalaamu wa kusindika. Kwa mtindo huu tutatua mpaka tatizo la ajira linalokabili Taifa letu. Inatakiwa ifikie sehemu tujivunie vyetu ila la sivyo tutakuwa tegemezi milele.

8--Kwa kumalizia wewe mtanzania mwenzangu tujaribu kupendana na kutakiana mazuri pia na kutoa maoni na ushauri wa kulijenga Taifa letu. Tanzania ni yetu sote na sio kuwa ni ya raisi Magufuli pekee. Kumbuka sio kuwa ni Magufuli pekee mwenye kuipenda Tanzania/mzalendo na mtiifu ila hata wewe pia. Unakaribishwa utoe mchango wako ili kuinenepesha nchi yetu kiuchumi jamani na sio kwa kukosoa ila ukikosoa toa way forward tafadhali sana.

toeni maada za kulijenga taifa letu jamani sio kuwa jukumu la kulijenga taifa ni la raisi pekee hata wewe hapo una mchango mkubwa kwa Tanzania. Huyo raisi ni muwakilishi wetu anategemea michango toka kwetu watanzania ila sio ndo tumpangie cha kufanya.

I LOVE TANZANIA ,TANZANIA IS MY MAMALAND, AM PROUD OF BEING TANZANIAN,AM PROUD OF MY LOVELY PRESIDENT JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.

LIVE LONGER TANZANIA,VIVA TANZANIA,VIVA PRESIDENT MAGUFULI
 
Back
Top Bottom