Toka jimboni Arumeru: UVCCM Arusha wagomea posho toka kwa mbunge... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toka jimboni Arumeru: UVCCM Arusha wagomea posho toka kwa mbunge...

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by only83, Feb 20, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Arumeru, juzi waligoma kupokea posho ya Sh 5,000 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige kwa madai kuwa ni ndogo na za kuwadhalilisha.

  Magige alitoa posho hiyo mwishoni mwa wiki kama asante kwa vijana waliomsindikiza katika ziara yake wilayani Arumeru mkoani Arusha kutoa msaada wa baiskeli kwa walemavu katika eneo la Oldonyo Sambu.

  Vyanzo vya habari vilieleza kuwa ziara hiyo ilianza saa 5 asubuhi na kumalizikia majira ya saa moja jioni na baada ya hapo Magige alitoa fedha hizo kwa mmoja wa wapambe wake ili awagawie vijana waliokwenda katika ziara hiyo iliyoonekana zaidi kuwa ya Jumuiya ya Wanawake ya chama hicho (UWT).

  Baada ya mgawo huo, inadaiwa vijana hao walizisusa wakidai ni kidogo na zinalenga kuwadhalilisha.

  “Umefika wakati wa sisi vijana kugoma kutumiwa kwa ujira mdogo kwa manufaa ya watu, tumekwenda ziara siku nzima halafu anatupa Sh 5,000, hii dharau kubwa.

  “Huu ni udhalilishaji wa kutufanya kama watoto wadogo wa kubembelezewa pipi, sasa udhalilishaji wa aina hii umefika mwisho kwa wabunge wa namna hii turudishe hizi fedha mara moja,” alisikika akishawishi wenzake kijana mmoja aliyekuwepo katika msafara huo.

  Mbunge Magige alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema hana taarifa ya UVCCM kukataa kupokea posho hiyo na kutaka kugombana kwani wenye kujua hilo ni wao wenyewe na wao ndio wanaopaswa kuulizwa.

  “Mimi sina taarifa ya hilo la kukataa posho ya ziara wala vijana kugombana, lakini ingekuwa vizuri zaidi ungewauliza hao hao vijana juu ya sakata hilo,’’ alisema Magige.

  Mmoja wa wanachama wa UVCCM Arusha, Philimini Amo alipoulizwa, alidai kweli vijana hao walikataa posho hiyo na kudai kuwa hali hiyo ilijitokeza kutokana na Magige kupewa taarifa potofu na wapambe.

  Source : Habari leo
  [/FONT]
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Umefika wakati sasa kwa TRA kutupia macho 'posho'. Aina hii ya kulipana imetapakaa kila mahali na huku ndiko wangevuna mapato mengi kwa kutoza kodi.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  i seee....
  napita tu pande hizi...
  kumbe uchaguzi deal eeeh?
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hao TRA wenye ndiyo ufisadi umetanda huko.
  Mi naona hawa magamba wataparanganyana siku si nyingi mpk na waache maofisi zikiwa wazi.
   
 5. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Posho posho posho! UVCCM posho hazitoshi!UWT posho,wabunge wa CCMposho hazitoshi!kazi kweli kweli!
   
 6. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli! Hii nayo habari ama kuchafuana tu?
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Posho ndiyo style ya CCM, utaendelea kusikia na zingine nyingi!!
   
 8. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwako habari ni ipi?
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Posho zinaipeleka CCM kuzimu.
   
 10. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Catherine Magige si ndo kale kabunge kadogo dogo na kazuri kuliko wote?!
   
 11. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mh Kigwangwalla angalia heshima ile uliyojijengea kwetu watanzania wakati ule wa mgomo wa madaktari isije ikapotea kwa kushindwa kuelewa vitu vidogo kama maana ya neno ''habari''. By the way kwa nini kwenye chama chenu kila tukio lazima mgawe posho, usafiri, au misosi. Mmeiharibu kabisa ile dhana ya kujitolea aliyotuachia baba wa Taifa. Kwa ushiriki wa hao vijana kugawa msaada kwa walemavu hawakustahili kulipwa hela, labda lunch kwa kuwa wamespend kutwa nzima. Zamani watu tuliamka asubuhi kuchimba barabara, kubeba matofari ya ujenzi wa viwanja (Ambavyo chama chenu kimevipora) bila kulipwa hata shilingi na viongozi wahamasishaji walipewa chakula na kijiji bila kulipa, posho hazikuwepo wakati huo. Lakini leo hata miaka 35 ya chama inabidi zichinjwe ng'ombe 70 na NYUMBU 20, je tutafika kweli? Hii si ndio chachu ya kufanya ufisadi kwani bila hela hapendwi mtu ndani ya CCM
   
 12. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazuri kuliko wote!!!! wote akina nani?
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  CCM kiboko -- misaada sasa hivi upepo ni Arumeru tu; pelekeni na mahindi ya njaa fasta mjipatie jimbo.
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kigwangalla bwana,haya tupe defination ya Habari msomi wetu...
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ha huyu jamaa hana ujasiri kabisa na wala sikuona mchango wake kwenye doctors movement...CCM walimuweka kiti moto kuwa anachochea mgomo,akalalamika kule Facebook kuwa atatoa tamko zito,baadae akakumbuka kitumbua chake,akanywea kama kuku aliyenyeshewa na mvua...
   
 16. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,049
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Hamis Kingwangwalla, USITURUSHIE HOJA! Unashangaa nini wakati weye wajua kuwa huo ni UTAMADUNI wa CCM? Huyu Magige anachotoa ni RUSHWA siyo posho? Mie sishangai kuwa MNADAI MAPATO yenu yaongezeke MNAPOKAA Bungeni! Matumizi yake ndo haya! Sofia Simba naye anawabana Wabunge wanawake wa CCM. Hapa Magige atatoa hesabu ya Matumizi ya POSHO zake kwa Mwenyekiti wake! Je, kwa staili hii CCM mna intergrity ya kuendelea kuongoza nchi?
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Lini mlikuwa wasafi.
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nawapongeza sana vijana wa CCM waliogoma kupokea posho kidogo kweli wameonyesha kipaji cha hali ya juu cha uelewa wa itikadi ya chama chetu, wamefuzu mafunzo ya viongozi wao, mbona wao bungeni wanataka kumpigia kura ya kutokuwa na imani rais wetu mpendwa kwa kugoma kuwaongeza posho? Big up totoz mtoto wa kenge ni kenge tu hawezi kuwa mpole kama mjusi.
   
 19. H

  HByabatto jr Senior Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msisahau kugawa chumvi,gongo,bange na tumbaku ili mshinde kirahisi
   
 20. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kuchafuana kwa vipi kwani wewe unajifanya hujui kuwa chama chenu bila kuhonga hakifanyiki kitu? Mlianza kusema ni takrima na sasa mmeitia maji mnaiita POSHO; zote hizo ni rushwa tu hata mkizibadilisha majina nyie magamba.Huyu mama si ndio mbeba hela za kuhonga za Lowassa huko Arusha, sasa wanamchafua vipi na hizo ndio zake?!!
   
Loading...