Toka iringa: Wanafunzi wa kike wamuua mwalimu wao kwa kutaka kumbaka mwenzao..

unaleta habar za mwaka uliopita? Kama huna cha kupost ni bora uwe mchangiaji.

Naona kafanya vizuri kuileta maana wengine sisi ni walimu tunajifunza mengi sana hapa. Binafsi nimestuka na kuanza kutafakari upya jinsi ya kuishi na hivi viumbe
 
Labda alieileta hii "sread" ana lengo la kufanya utafiti juu ya kumbukumbu za wajumbe hapa ukumbini!
 
huyu dada nina mashaka naye. Kilichomfanya kupeleka ripoti nyymbani tena usiku ni nini? Naona kama hakubakwa ila ilikuwa janja tu ya kujinasua na kufukuzwa chuo. Mwalimu hakuwa na sababu ya kumbaka kwani alukuwa na uwezo wa kumpata binti.
 
Inawezekana kabisa ni mpango walipanga hao wanafunzi kumkomoa Mwalimu wa nidhamu,kwani kulikuwa na uharaka gani hadi apeleke maelezo usiku na nyumbani kwake,kwanini hakusubiri hadi asubuhi,Yaelekea marehemu alikuwa anawaban sana wasiende kutafuta ada kwa hiyo wakaona solution ni kumkomoa[ spontenous mob psychology],anyway mikono ya watanzania wengi kwa sasa ina damu,wako wanopiga suspects wa wizi na kuwaua kila siku kwa kisingizio cha hasira kali,watoto wetu wanashiriki kupiga hao wezi na akirudi anakusimulia baba au mama kuwa leo tumeua lijizi na wewe unampa hongera ,kwa kweli sio siri ukichunguza vizuri asilimia sio chini ya 30 ya watanzania hasa wa mijini wameisha shiriki hii dhambi ya mauaji,angalia hao mabinti bado wadogo lakini hawaogopi kutoa roho ya mtu,mwenyezi Mungu atuepushe na hii laana ya damu tunayomwaga kila siku kwa visingizio mbalimbali.Mwenye haki ya kukatiza maisha ya Mwanadamu ni yule tu aliyemuumba na si vinginevyo,ukiua unamkosoa Mungu aliyempa uhai.Kwa dini yetu hii ni cardinal and un pardonable offence.
 
Hii habari mbona inafanana kabisa na ile ya mwaka jana, au imejirudia kwa mara nyingine?
 
mh hilo tukio linaonekana kabisa kuwa ni mchezo wa kupangwa! hao wanafunzi inaonekana walipanga kumkomoa mwalimu wao na wakaona kabisa kwamba njia sahihi ni kumfanyia hayo yote! la kama kweli jamaa alikuwa na nia ya kubaka hilo litakuwa tatizo jengine!
 
Mkuu Skills4ever naungana na wewe kabisa,huyu dada alikuwa amejipanga na wenzake kumdhalilisha ticha maana maticha wa nidhamu sehemu yeyote huwa wanaonekana wanoko!Polisi wafanye uchunguzi makini!!
tatizo ni kwamba hawapo hao polisi makini wa kumzidi kova sasa hapo unatarajia kuna kitu.
 
Mimi nadhani hiyo walipanga tu na wanafunzi wenzake. Kwanini apeleke barua usiku? Hakuna namna ya kuprove kwamba huyu binti alitaka kubakwa,Jean na wanafunzi wengine wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Ila tu sasa naona na wanafuzi wanachoshwa na waalim kuwataka kimapenzi. Hivi mnakumbuka sakata la Mwalimu Mkuu mmoja wa Shule Sekondari Michiael Kitinya ambaye alikimbizwa na wanafunzi wakati akiwa kabisa anajiandaa kufanya ngono na mwanafunzi. Sikumbuki tena ni shule gani ila ni ya Sekondari Mkoa wa Pwani. Haya mambo yapo na ni lazima tuwafundishe watoto wetu jinsi ya kuyakomesha maana ni kesi nyingi mwalim anampa mimba mwanafunzi na hatua kali hazichukuliwi na ndiyo maana hizi kesi zao bado zinajitokeza. Let us agree ikithibitika mwalim kambaka mwanafunzi au kumpa ujauzito basi akatwe hiyo kitu yake. Naona hii itakuwa ya kutosha kuwacha watoto wetu salama. Na hii iwe kwa wanaume waote wanaobaka au kufanya mapenzi na mimba kwa watoto wote.
 
Huyo mwanafunzi inaonesha dhahiri alikua amepanga kum'ulimboka ticha sababu hayo maelezo ni ya kiofisi sasa kwanini apeleke nyumbani na ni usiku???
 
Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Bulongwa kilichoko Wilaya ya Makete mkoani Iringa, wamemuua kwa kumshambulia kichwani mkufunzi wa chuo hicho, Dk. Jumbe Mafingo, kwa madai ya kupinga jaribio lake la kutaka kumbaka mwanafunzi mwenzao.


Taarifa za awali za makachero wa polisi zilieleza kuwa mkufunzi huyo aliuawa baada ya kutuhumiwa kwamba alitaka kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike, Jean Laison Mwakabuta kwa kutaka kumbaka.Tukio hilo la kuuawa kinyama kwa mkufunzi huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, lilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini hapa.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, Dk. Mafingo alifikwa na umauti baada ya mwanafunzi huyo kuamua kwenda nyumbani kwake usiku ili kumkabidhi maelezo yake ya kimaandishi kuhusu sababu zilizomfanya alale nje ya chuo.Ilielezwa kuwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye nyumba ya mwalimu huyo, mwanafunzi huyo alianza kupiga kelele kuwa anabakwa.


Alisema kufuatia kelele hizo, wanachuo wengine waliamka katika vyumba vyao na kwenda hadi eneo la tukio na kuanza kumshambulia kichwani mkufunzi huyo hadi kumuua.


Kamanda Mangalla alisema Dk. Mafingo aliuawa kwa kushambuliwa na kitu kizito kichwani.

“Huyu Jean Laison Mwakabuta, aliambiwa na Dk. Mafingo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, aandike maelezo ya maandishi kwa sababu gani alilala nje ya chuo,...baada ya kuandika maelezo hayo, aliamua kuyapeleka nyumbani kwa mkufunzi huyo usiku, sasa baada ya kugonga mlango na hatimaye akaruhusiwa kuingia, alianza kupiga kelele kwamba anabakwa…na ndipo wanafunzi wenzake waliposikia kelele wakaamka na kukimbilia eneo hilo na kumshambulia mkufunzi huyo hadi kufa,” alisema Kamanda Mangalla.


Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, uongozi wa chuo hicho cha Bulongwa ulitoa ridhaa kwa wanachuo wote kwenda kutembea nje ya chuo kwa lengo la kuwapunguzia msongo wa mawazo ya masomo na Jean Laison Mwakabuta hakurejea chuoni hadi siku iliyofuata.Kamanda Mangalla, alisema wanachuo wanne akiwamo mwanafunzi Jean, wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji hayo.

Hawa bwana wahuni 2 walikuwa na bifu na mwalim wao wakamtegea then wakapiga hadi wakaua, hili swala we have 2 be serious.
 
Tukio hili lina mwaka mmoja au zaidi tangu litokee! Au ni ganda la muwa la jana ...?
 
Tukio hili lina mwaka mmoja au zaidi tangu litokee! Au ni ganda la muwa la jana ...?

em niambie kesi iliendeleaje maana inaonekana wanafunzi walikuwa na bifu na mwalimu wao wakataka wamkomeshe bahati mbaya akafariki
 
Mh Spika naomba MWONGOZO, Kifungu cha 48 ibara ndogo ya 3 inasema nanukuu Ikiwa jambo lolote lipo mahakamani au kwenye Vyombo vya sheria lisizungumziwe hapa .................. hivyo Mh mlata Mada kaileta Hoja ya mwaka jana na hukumu yake b.....
 
wanafunzi kama ndo njia ya kutatua matitizo yenu jueni mmekosea,ona sasa mnataka kwenda jela kwa jambo dogo tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom