jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Kwa political analysists wazuri watakubaliana na mimi kuwa katika uhai wake kama Chama cha Siasa kimefail kuwa na ushawishi katika upande wa pili wa muungano. Jambo hili halina afya nzuri kwa chama cha siasa Tanzania kwani kinapaswa kuwa na uwezo, wanachama na nguvu katika pande zote za muungano.
Hii inaweza kuwa ni ishara ya Chama hicho kwa makusudi kutaka kuigawa nchi vipande vipande. Kwa mwenye akili anaweza kuhoji kwa nini miaka yote CHADEMA imeacha au kushindwa kuandaa nguvu ya represantation huko Zanzibar? Hii ni ishara ya namna gani wengi wanakichukulia chama hiki kama ni cha ukanda. Kisingizio cha kuunga mkono juhudi kimekuwa kinajirudia mara kwa mara.
Nikitolea mfano wa CUF, chenyewe kimeweza na kufanikiwa kupata uungaji mkono kutokea Zanzibar hadi bara, kilichowashinda CHADEMA ni nini? Nikiiangalia ACT imeweza kujipenyeza kutoka bara hadi Zanzibar. CHADEMA ikiri kuwa ni chama chenye misingi mibovu ya kushawishi umoja wa kitaifa. Hii ni mojawapo ya sababu kwa nini kinaangukia pua katika kila uchaguzi.