Toka ai ngie magufuli madarakani kaajiri watu 6,099 na kufukuza watumishi 12,000 huku 98.9% ya waliomba kazi serikalini wamekosa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Katibu wa Sekretarieti ya ajira, Xavier Daudi
Kwa ufupi
  • Sekretarieti ya ajira nchini Tanzania imesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, watu 6,099 wameajiriwa huku 587,746 wakikosa. Kati ya hao 140,000 ndio walioitwa katika usaili

Dar es Salaam. Watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo, Sekretarieti ya ajira imebainisha hayo leo Jumatatu Desemba 17, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kazi kwa miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katibu wa sekretarieti hiyo, Xavier Daudi amesema kuanzia Novemba 2015 hadi Desemba 2018, maombi ya kazi yalikuwa 594,300 lakini waliopata ajira ni watu 6,099.
"Tangu Serikali iingie madarakani Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi 6,554 kwa ajili ya wizara, idara, wakala, sekretarieti za mikoa, manispaa, halmashauri na taasisi mbalimbali za elimu," amesema Daudi na kuongeza:
"Jumla ya maombi 594,300 yalipokewa na kufanyiwa kazi, zaidi ya waombaji 140,000 waliitwa kwenye usaili.”
Amesema hadi Desemba 15, 2018 watu 6,099 wamepata ajira na nafasi 455 zilizotangazwa kati ya Novemba na Desemba 2018 mchakato wake unaendelea na utakamilika hivi karibuni.
Hata hivyo, Daudi alisema kuna watumishi wengine 64,814 walioajiriwa kupitia Ofisi ya Rais (Tamisemi) katika kada za afya na walimu.
 
Yaani ndani ya miaka mitatu ajira Serikalini ni 1.11% ya idadi walioomba kazi Serikalini! Halafu bado kuna watu wanadai uchumi unakuwa na kutaka huyu janga kubwa la Taifa aendelee kuwepo madarakani!
 
Mkuu na tukiweka namba ya waliofukuzwa kazi kwa madai ya kufoji vyeti (kumbuka Bashite pamoja na kufoji vyeti vyake dikteta alimkingia kifua) basi hii asilimia ya ajira Serikalini kwa miaka lita tu iliyopita itakuwa ni negative number.

Hii awamu ni mzigo kwa watanzania.
 
Katibu wa Sekretarieti ya ajira, Xavier Daudi
Kwa ufupi
  • Sekretarieti ya ajira nchini Tanzania imesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, watu 6,099 wameajiriwa huku 587,746 wakikosa. Kati ya hao 140,000 ndio walioitwa katika usaili

Dar es Salaam. Watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo, Sekretarieti ya ajira imebainisha hayo leo Jumatatu Desemba 17, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kazi kwa miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katibu wa sekretarieti hiyo, Xavier Daudi amesema kuanzia Novemba 2015 hadi Desemba 2018, maombi ya kazi yalikuwa 594,300 lakini waliopata ajira ni watu 6,099.
"Tangu Serikali iingie madarakani Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi 6,554 kwa ajili ya wizara, idara, wakala, sekretarieti za mikoa, manispaa, halmashauri na taasisi mbalimbali za elimu," amesema Daudi na kuongeza:
"Jumla ya maombi 594,300 yalipokewa na kufanyiwa kazi, zaidi ya waombaji 140,000 waliitwa kwenye usaili.”
Amesema hadi Desemba 15, 2018 watu 6,099 wamepata ajira na nafasi 455 zilizotangazwa kati ya Novemba na Desemba 2018 mchakato wake unaendelea na utakamilika hivi karibuni.
Hata hivyo, Daudi alisema kuna watumishi wengine 64,814 walioajiriwa kupitia Ofisi ya Rais (Tamisemi) katika kada za afya na walimu.
Hii itasaidia watumishi kuheshimu ofisi na kutimiza wajibu wao!
 
Yaani ndani ya miaka mitatu ajira Serikalini ni 1.11% ya idadi walioomba kazi Serikalini! Halafu bado kuna watu wanadai uchumi unakuwa na kutaka huyu janga kubwa la Taifa aendelee kuwepo madarakani!
Mkuu Bubu, naona unaumia sana mpaka umeshindwa kuvumilia!!

Indicator ya kukua kwa uchumi huwa inaendana na ukuaji wa ajira. Lakini kwa Tanzania ni tofauti. Sasa awamu hii tunaambiwa kila kitu kiko poa wakati ajira zinazidi kuadimika. Hivi ni Tanzania iko kwenye right track au kuna kikundi cha watu Tanzania ndiyo wako kwenye hiyo right track!!?
 
Inaudhi Mkuu nchi yetu iliyojaliwa ardhi kubwa tena yenye rutuba kubwa, rasilimali chungu nzima lakini ikiendelea kubaki nyuma kimaendeleo mwaka hadi mwaka kutokana na hawa majizi na mafisadi.

Inadaiwa mwanzoni mwa miaka ya 60 uchumi wetu kwa ukubwa ulikuwa unashabihiana sana na uchumi wa Malaysia, Singapore na South Korea na nchi zote hizi hazina rasilimali kama Tanzania lakini sasa hivi wametuacha mbali sana kiuchumi sisi kinachokuwa nchini ni utajiri wa kutisha wa haya majizi na mafisadi wakati idadi kubwa ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya ufukara wa kutisha.

Mkuu Bubu, naona unaumia sana mpaka umeshindwa kuvumilia!!

Indicator ya kukua kwa uchumi huwa inaendana na ukuaji wa ajira. Lakini kwa Tanzania ni tofauti. Sasa awamu hii tunaambiwa kila kitu kiko poa wakati ajira zinazidi kuadimika. Hivi ni Tanzania iko kwenye right track au kuna kikundi cha watu Tanzania ndiyo wako kwenye hiyo right track!!?
 
Mkuu Bubu, naona unaumia sana mpaka umeshindwa kuvumilia!!

Indicator ya kukua kwa uchumi huwa inaendana na ukuaji wa ajira. Lakini kwa Tanzania ni tofauti. Sasa awamu hii tunaambiwa kila kitu kiko poa wakati ajira zinazidi kuadimika. Hivi ni Tanzania iko kwenye right track au kuna kikundi cha watu Tanzania ndiyo wako kwenye hiyo right track!!?
hali mbaya sana kwa vijana
 
Back
Top Bottom