Tohara na UKIMWI

mutisya mutambu

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
208
82
Ni muda sasa toka pale utafiti ulipofanyika kuhusu uwezo wa kupunguza ueneaji wa virusi vya ukimwi kwa kuongeza idadi ya wanaume waliotahiriwa ikiaminiwa kwamba wanaume waliotahiriwa wana hatari ndogo sana ya kupata maambukizi ukilinganisha na wale ambao hawajatahiriwa pindi wakutanapo na mwanamke mwenye virusi.

Tunaona sasa nchi nyingi zimekubaliana na utafiti huu na kweli zinachukua hatua kwa kuhamasisha utahiri kwa wanaume ambao hawakupata kutahiriwa,ilianza kenya na uganda sasa ni rwanda.

Kuhusu hili nina maswli mawili tu ndugu daktari:
1. Kuna uhusiano gani kati ya vitu hivyo viwili, kutahiriwa na virusi vya UKIMWI?
2. Kwa sasa Tz ina mpango gani kama wenzake, kwa sioni lolote likiendelea kama kwa wenzetu?

=======

KUTOKANA na utafiti wa kisayansi kuonesha kuwa kutofanya tohara kwa wanaume ni moja ya sababu zinazochangia maambukizi ya Ukimwi, wanaume katika mikoa saba nchini wanatarajiwa kufanyiwa tohara kuanzia mwakani kwa sababu inayo idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumu kwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutoka Marekani, kufanya tohara kwa wanaume hao katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Haji Mponda, jana mjini hapa, katika hotuba yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Kitaifa mjini hapa.

Dk. Mponda alisema utafiti uliofanyika na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, imeonesha kuwa mikoa hiyo inaongoza kwa maambukizi na moja ya sababu ni kuwepo kwa idadi mkubwa ya wanaume wasiofanyiwa tohara.

“Mpango wa Wizara ni kutaka kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU na utafiti umeonesha mikoa hii ina idadi ndogo ya wanaume waliofanyiwa tohara, lakini ina viwango vya juu vya maambukizi,” alisema Waziri huyo.

Hivyo alisema mpango wa Wizara ambao tayari ulianza kwa majaribio katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Kagera, itaendelezwa zaidi katika mikoa iliyoainishwa kuanzia mwakani kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia mashirika yao ya misaada sambamba na marafiki wengine wa maendeleo.

Alisema mpango huo wa kuwafanyia tohara wanaume katika mikoa hiyo umelenga kuwafikia wanaume zaidi ya milioni 2.5 na wanaume wa mikoa hiyo wameonesha kufurahishwa na uamuzi huo wa kuwatahiri.

Katika takwimu zilizotolewa na TACAIDS ya viwango vya maambukizi ya VVU ya mwaka 2003/ 2004, Mkoa wa Iringa ulikuwa na maambukizi ya asilimia 13.4 ambapo kwa mwaka 2007/2008 maambukizi ni asilimia 15.7.

Mkoa wa Mara kwa miaka hiyo, maambukizi yalikuwa ni asilimia 3.5 na kuongezeka mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 7.7 wakati Mkoa wa Shinyanga maambukizi yalikuwa ni asilimia 6.5 ambapo kwa mwaka 2007/2008 viwango vya maambukizi ni asilimia 7.4.

Naye Mwandishi Wetu, Flora Mwakasala anaripoti kuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chiku Galawa ametaka mabango yote ya waganga wa jadi yanayotangaza kuwepo kwa dawa za kuongeza nguvu za kiume, yaondolewe kwa kuwa ni kichocheo cha ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi yaliyofanyika jana kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Galawa alisema mabango hayo yamebandikwa mitaani kwa wingi.

“Huu ni utapeli mkubwa, nani kasema watu wanahitaji kuongezewa nguvu za kiume? Jambo hili ni sawa na kuwahamasisha watu waendelee kufanya uasherati na kuongeza maambukizi mapya ya VVU,” alisema.

Alisema kitendo cha watu kuongeza nguvu za kiume kinawashawishi kuendelea kufanya ngono, jambo linalosababisha kuwepo kwa ongezeko kubwa la maambukizi hasa kwa vijana ambao ni taifa la kesho.

“Tutashirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha mabango yote yaliyobandikwa mitaani na barabarani yanaondolewa,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Mafunzo Taifa wa Chama cha Waganga wa Tiba za Asili, Sadick Kalimaunga alisema kauli hiyo ya Galawa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, si sahihi kwa kuwa kazi yao ni kuwasaidia wanaume wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

“Sisi hatuchochei maambukizi ya VVU kama wanavyodai bali tunawasaidia wanaume wenye matatizo hayo kudumisha ndoa zao kwa kuwaongezea nguvu za kiume ili waweze kufanya tendo hilo kikamilifu,” alisema.

Aidha, alisema kitendo cha Serikali kuondoa mabango hayo kitasababisha baadhi ya watu wanaohitaji tiba hizo ambazo zilikuwepo tangu enzi kukosa huduma na wengine ndoa zao kuvunjika.

Kwa mujibu wa takwimu, Dar es Salaam ni mkoa unaoshika nafasi ya pili nchini kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU cha asilimia 9.3. Iringa inaongozwa kwa kuwa na asilimia 15.7.

Chanzo: Habari Leo
 
Govi huwa linafunika soft tissues za uume hivyo inabaki kuwa laini and delicate to abrassions wakati wa kujamiiana. Mtu aliyetahiriwa ngozi yake inakuwa ngumu na resistant to abrassions during sex.

Pia lile lingozi huwa linajifunua na kujifunika wakati wa sex hivyo kuongeza uwezekano wa kuchanika na kuongeza uwezekano wa kuambukizwa
 
mutisya mutambu

As Pax alivyoainisha, aliyetahiriwa ana punguza 60% ya kuambukizwa VVU tofauti na mwenye govi kutokana na michubuko inayojitokeza wakati wa tendo.

Pili kwa hapa Tz kuna mikakati mingi sana hasa katika mikoa ambayo haina mila ya tohara, kwa mfano kati ya mwaka jana na mwaka huu, wanaume wengi sana wametahiriwa (kama 10,000 hivi) na kampeni inaendelea tabora, rukwa, shinyanga etc though NGO.
 
Last edited by a moderator:
Mh condom zimeshindwa,ABC nayo imeshindwa !sasa ni kutahiri .....lakini yote kumi ngono zembe ...yaelekea tumeshindwa vita sasa.
 
Tohara ya ‘lazima' kwa wanaume yaja

KUTOKANA na utafiti wa kisayansi kuonesha kuwa kutofanya tohara kwa wanaume ni moja ya sababu zinazochangia maambukizi ya Ukimwi, wanaume katika mikoa saba nchini wanatarajiwa kufanyiwa tohara ya lazima kuanzia mwakani kwa sababu inayo idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumu kwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutoka Marekani, kufanya tohara kwa wanaume hao katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Chanzo: Habarileo
 
KUTOKANA na utafiti wa kisayansi kuonesha kuwa kutofanya tohara kwa wanaume ni moja ya sababu zinazochangia maambukizi ya Ukimwi, wanaume katika mikoa saba nchini wanatarajiwa kufanyiwa tohara kuanzia mwakani kwa sababu inayo idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumu kwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutoka Marekani, kufanya tohara kwa wanaume hao katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Haji Mponda, jana mjini hapa, katika hotuba yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Kitaifa mjini hapa.

Dk. Mponda alisema utafiti uliofanyika na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, imeonesha kuwa mikoa hiyo inaongoza kwa maambukizi na moja ya sababu ni kuwepo kwa idadi mkubwa ya wanaume wasiofanyiwa tohara.

“Mpango wa Wizara ni kutaka kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU na utafiti umeonesha mikoa hii ina idadi ndogo ya wanaume waliofanyiwa tohara, lakini ina viwango vya juu vya maambukizi,” alisema Waziri huyo.

Hivyo alisema mpango wa Wizara ambao tayari ulianza kwa majaribio katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Kagera, itaendelezwa zaidi katika mikoa iliyoainishwa kuanzia mwakani kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia mashirika yao ya misaada sambamba na marafiki wengine wa maendeleo.

Alisema mpango huo wa kuwafanyia tohara wanaume katika mikoa hiyo umelenga kuwafikia wanaume zaidi ya milioni 2.5 na wanaume wa mikoa hiyo wameonesha kufurahishwa na uamuzi huo wa kuwatahiri.

Katika takwimu zilizotolewa na TACAIDS ya viwango vya maambukizi ya VVU ya mwaka 2003/ 2004, Mkoa wa Iringa ulikuwa na maambukizi ya asilimia 13.4 ambapo kwa mwaka 2007/2008 maambukizi ni asilimia 15.7.

Mkoa wa Mara kwa miaka hiyo, maambukizi yalikuwa ni asilimia 3.5 na kuongezeka mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 7.7 wakati Mkoa wa Shinyanga maambukizi yalikuwa ni asilimia 6.5 ambapo kwa mwaka 2007/2008 viwango vya maambukizi ni asilimia 7.4.

Naye Mwandishi Wetu, Flora Mwakasala anaripoti kuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chiku Galawa ametaka mabango yote ya waganga wa jadi yanayotangaza kuwepo kwa dawa za kuongeza nguvu za kiume, yaondolewe kwa kuwa ni kichocheo cha ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi yaliyofanyika jana kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Galawa alisema mabango hayo yamebandikwa mitaani kwa wingi.

“Huu ni utapeli mkubwa, nani kasema watu wanahitaji kuongezewa nguvu za kiume? Jambo hili ni sawa na kuwahamasisha watu waendelee kufanya uasherati na kuongeza maambukizi mapya ya VVU,” alisema.

Alisema kitendo cha watu kuongeza nguvu za kiume kinawashawishi kuendelea kufanya ngono, jambo linalosababisha kuwepo kwa ongezeko kubwa la maambukizi hasa kwa vijana ambao ni taifa la kesho.

“Tutashirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha mabango yote yaliyobandikwa mitaani na barabarani yanaondolewa,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Mafunzo Taifa wa Chama cha Waganga wa Tiba za Asili, Sadick Kalimaunga alisema kauli hiyo ya Galawa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, si sahihi kwa kuwa kazi yao ni kuwasaidia wanaume wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

“Sisi hatuchochei maambukizi ya VVU kama wanavyodai bali tunawasaidia wanaume wenye matatizo hayo kudumisha ndoa zao kwa kuwaongezea nguvu za kiume ili waweze kufanya tendo hilo kikamilifu,” alisema.

Aidha, alisema kitendo cha Serikali kuondoa mabango hayo kitasababisha baadhi ya watu wanaohitaji tiba hizo ambazo zilikuwepo tangu enzi kukosa huduma na wengine ndoa zao kuvunjika.

Kwa mujibu wa takwimu, Dar es Salaam ni mkoa unaoshika nafasi ya pili nchini kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU cha asilimia 9.3. Iringa inaongozwa kwa kuwa na asilimia 15.7.

Chanzo: Habari Leo
 
Hivi hii serikali ina watu wanaofikiri kweli?? Je, huko nchi za kiislamu ambako kila mmoja amaetahiriwa hakuna wagonjwa wa ukimwi??. Badala ya kuhubiri watu wawe waadilifu kwa kutofanya ngono hovyo, eti watu watahiriwe kwa lazima. Nani tuko tayari kuharibu uumbaji wa Mungu kwa njia hiyo??. Wote walio kwenye mpango huo washindwe na walegee. Hamuwezi kusilimisha watu bila ridhaa yao.
 
Tohara kwa wanaume ni jambo la kiafa; ila sio jibu la ukimwi unless "umeutahiriwa" katika moyo na mienendo yako....plus watu lazima wawe tayari kwa hilo baada ya kuelimishwa kwa kwa wengine tohara sio mila yako so it will take time to accept it.
 
Tohara haiwezi kuwa jibu la maambukizi ya VVU!

Hii itakuwa "Nitoke Vipi" ya Dr Haji Mponda
 
Fedha ya wafadhiri kwa ajiri ya kuondoa mkono wa sweta?, amesahau kuwa katika mikoa aiyotaja kuna tatizo sugu la soko la mazao mba;imbali, si bora fedha hizo zingetumika kwenye kilimo kwanza?!, nataraji kushindwa kwa mradi huu.
 
Hii ni kuwafahamaisha wadau wa JF kwamba leo hii imeanza kampeni ya kuwafanyia tohara wanaume. Nimembiwa hii ni kwa wanaume wote wenye miaka kati ya 10 na 67. Wenye tisheti zao zimeandikwa MENYA GANDA. Hapa nipo kwenye hospitali teule ya wilaya Mbeya vijijini, eneo la Ifisi karibu na mji mdogo wa Mbalizi. Nilipofuatilia zaidi nikaambiwa, kutoa kale kangozi ni sawa na mtu anapomenya ndizi, ndizi inaliwa na ganda linatupwa. Basi wabunifu wa hako kamchezo wakasema menya ganda, ila kimsingi mie naona inayomenywa ni ndizi na sio ganda.

Kwa hiyo, watu wanamenywa ndizi zao, maganda yanatupwa. Tisheti zimendikwa pia, tohara huzuia maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 60. Kumekuwa na msururu wa vijana wadogo wenye umri wa kati ya miaka 7 na 17 wakimenywa ndizi zao. Nilipodadisi walivyopata taarifa nikaambiwa wengine waliambiwa lazima kuja, kwani baada ya kuwamaliza waliokuja kwa hiari hapa, timu ya wamenyaji hiso ndisi watapita nyumba kwa nyumba kukagua ambao bado hawajamenywa. Nikagundua kwamba kumbe si vijana wote wamekuja kwa hiari yao. Swali likanijia kichwani ikitokea madhara kwa mmoja aliyemenywa ndizi yake nani atawajibika?

Jambo lenyewe linaweza kuwa zuri kwa maana ya kusaidia kunusuru maisha ya watu wetu ambao hawasikii mawaidha wazazi, wachungaji wala mashehe. Wao wanaendekeze libeneke bila kujali maagizo ya Mungu. Lakini hiari ya mtu kuamua amenywe au asimenywe ndisi yake ni muhimu sana. Hata hivyo baadaye nilipowahoji baadhi ya vijana walisema kabla ya kumenywa walipata maelekezo kutoka kwa watoa huduma hiyo kwamba ni hiari ya kila mmoja. Hapo nikafarijika kidogo. Ila kwa asilimia 60 tu ya kujinusuru, Ina maana mpango huu bado si suluhisho la matatizo ya ufuska na mdogo wake ngono uzembe.
 
Big Dady

Ndizi ikimenywa inaleta raha sana, hao waliomenywa kwa nguvu wataona faida yake hapo baadae.
 
Last edited by a moderator:
kazi kweli kweli.iringa hiyo operation inaitwa operation ondoa vuvuzela!japo wengi wanadai eti govi linaongeza raha ya mapenzi!
 
Ndizi ikimenywa inaleta raha sana, hao waliomenywa kwa nguvu wataona faida yake hapo baadae.

wataalam wa afya wanasema tango likiliwa bila kumenywa linafaa sana kwani a lot of
vitamins vipo kwenye greenish
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom