Tohara kwa Wanawake ina faida gani?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Nimefuatilia sana wanaopinga tohara kwa Wanawake, lakini wanataja hasara tu.Faida nilizosikia kwa kuwahoji makabila yanayokeketa Wanawake ni haya yafuatayo:-

1. Kuzuia U.T.I kwa watoto wa Kike.
2. Kupunguza msuguano wa uke na hivyo kupunguza ashki ya kingono kwa Msichana.
3. Kuzuia uhuni/umalaya kwa Wasichana/Wanawake.
4. Kumuweka Msichana katika hali ya utuuzima.
5. Kumfanya mwanamke atulie katika Ndoa.

Wana JF haya niliyosikia ni ya kweli katika hali halisi ya maisha?
 
Haina faida yoyote

1.Ina punguza hamu ya kufanya mapenzi. Sasa akiolewa ndiyo ina kuaje?
2.Una haribu maumbile la eneo fulani. Mungu kaiweka kwa makusudi kwa nini muitoe?
3.Wanawake wengi hufanyiwa tihara kienyeji na husababisha afe kwa kutokwa na damu nyingi, kidonda, na hata maambukizo ya maradhi. Wengine hufa wakati wa tohara.

Ni unyanyasaji tu wanaofanyiwa wanawake wetu. Haina faida yoyote.
 
Nimefuatilia sana wanaopinga tohara kwa Wanawake, lakini wanataja hasara tu.Faida nilizosikia kwa kuwahoji makabila yanayokeketa Wanawake ni haya yafuatayo:-

1. Kuzuia U.T.I kwa watoto wa Kike.
2. Kupunguza msuguano wa uke na hivyo kupunguza ashki ya kingono kwa Msichana.
3. Kuzuia uhuni/umalaya kwa Wasichana/Wanawake.
4. Kumuweka Msichana katika hali ya utuuzima.
5. Kumfanya mwanamke atulie katika Ndoa.

Wana JF haya niliyosikia ni ya kweli katika hali halisi ya maisha?

Tohara ina faida. Ni alama wazi inayoonesha:
a. Mtu kutoka kwenye utoto na kuingia utu uzima. It is a visible sign of the rite of passage from childhood to adulthood. Bila alama hiyo ya kuonekana bado mtu haonekani kama amekua
b. Inamwonesha mtahiriwa kuwa maisha si lelemama. Ni magumu. Yabidi kuvumilia shida za maisha. Kumbe tohara ni kipimo cha ujasiri wa mtu. Ndo maana mwenye kutahiriwa hapaswi kulia kwa maumivu. Akilia daima watu wa rika lake watamcheka daima kwamba ni mwoga. Hawezi ku-face maisha
c. Tohara inapunguza hamu ya mwanamke kufanya mapenzi. It seems to be negative. Lakini kwa kweli ukavu huu ni mtihani kwa kina baba. Kumbe lengo pia ni kupima kama kina baba wanaweza kuwavuta taratibu kwa ubingwa wao katika masuala ya tendo la ndoa mpaka wakawaweka katika hali ya hamu ya kufanya mapenzi. Kumbe mwanaume anayefaulu hilo anaokena pia ni mkomavu. Tohara ni kipimo cha ujuzi wa mwanaume anayemjamii mwanamke aliye tahiriwa
d. Tohara -wanasema sina uhakika - wanasema inampunguzia mwanamke uchafu fulani katika sehemu zake. Katika jamii fulani hicho kitu kinachokatwa wanajamii wanakiita "takataka". Kumbe kinapoondolewa inaonekana ni kumweka mwanamke katika usafi kwa kiwango kikubwa
e. Tohara inamfanya mwanamke aolewe kiurahisi na wanaume wanaopenda wanawake waliotahiriwa. Bila kutahiriwa "amekula wa chuya".
 
Hakuna faida ni uonevu wa kijinsia tu. Kama kupunguza hamu ya ngono ni kitu kizuri basi wanaume tukatwe makoza(testicles), hii itasaidia kuzuia tusitafute nyumba ndogo!!
 
Kama ni kuharibu maumbile mbona wanaume wanatahiriwa na watu wanatoga sehemu za mwili kuweka eleni.Halafu Bibi zetu wametulia enzi zao kwa ajili ya Tohara,ulizeni jamii zinazotairi wanawake mtasikia.Baada ya harakati za kupinga tohara kwa Wanawake sasa jamii imeharibika.
 
Nimefuatilia sana wanaopinga tohara kwa Wanawake, lakini wanataja hasara tu.Faida nilizosikia kwa kuwahoji makabila yanayokeketa Wanawake ni haya yafuatayo:-

1. Kuzuia U.T.I kwa watoto wa Kike.
2. Kupunguza msuguano wa uke na hivyo kupunguza ashki ya kingono kwa Msichana.
3. Kuzuia uhuni/umalaya kwa Wasichana/Wanawake.
4. Kumuweka Msichana katika hali ya utuuzima.
5. Kumfanya mwanamke atulie katika Ndoa.

Wana JF haya niliyosikia ni ya kweli katika hali halisi ya maisha?

Sioni ni kwa vipi tohara inaweza kuzuia UTI (Urinary Tract infection)!

Nakubaliana na wewe kwamba kampeni nyingi zimelenga kuondoa mila hizi 'potofu' bila kuangalia namna ya kuretain faida zake au kutafuta mbadala ambao utawezesha jamii zinazohusika kufikia malengo yao.

Kama lengo la tohara lilikuwa kumfanya mwanamke atulie (na kweli alikuwa 'anatulia'!), tunaposema sasa tohara marufuku, tunafanya nini kuendelea kumsaidia mwanamke atulie? Nadhani hapo ndio kwenye tatizo: mzungu akisema hii ni potofu, waafrika tunabeba 'wholesale' bila hata kuchekecha!
 
Tohara ni mbaya wakati wa kujifungua, maana ukishatahiriwa kunabaki kovu wakati wa kujifungua unaposukuma mtoto lile kovu linachanika unaweza kupoteza maisha kwa kutokwa damu nyingi.
 
. Kuzuia uhuni/umalaya kwa Wasichana/Wanawake.

Hiyo si kweli, Wanawake walio-keketwa wanapenda sana kufanya ngono (labda kwa sababu ni vigumu kufika kileleni - kwahiyo upenda KUJARIBU-JARIBU). Nawafahamu wengi tu.
 
Tohara ina faida. Ni alama wazi inayoonesha:
a. Mtu kutoka kwenye utoto na kuingia utu uzima. It is a visible sign of the rite of passage from childhood to adulthood. Bila alama hiyo ya kuonekana bado mtu haonekani kama amekua
b. Inamwonesha mtahiriwa kuwa maisha si lelemama. Ni magumu. Yabidi kuvumilia shida za maisha. Kumbe tohara ni kipimo cha ujasiri wa mtu. Ndo maana mwenye kutahiriwa hapaswi kulia kwa maumivu. Akilia daima watu wa rika lake watamcheka daima kwamba ni mwoga. Hawezi ku-face maisha
c. Tohara inapunguza hamu ya mwanamke kufanya mapenzi. It seems to be negative. Lakini kwa kweli ukavu huu ni mtihani kwa kina baba. Kumbe lengo pia ni kupima kama kina baba wanaweza kuwavuta taratibu kwa ubingwa wao katika masuala ya tendo la ndoa mpaka wakawaweka katika hali ya hamu ya kufanya mapenzi. Kumbe mwanaume anayefaulu hilo anaokena pia ni mkomavu. Tohara ni kipimo cha ujuzi wa mwanaume anayemjamii mwanamke aliye tahiriwa
d. Tohara -wanasema sina uhakika - wanasema inampunguzia mwanamke uchafu fulani katika sehemu zake. Katika jamii fulani hicho kitu kinachokatwa wanajamii wanakiita "takataka". Kumbe kinapoondolewa inaonekana ni kumweka mwanamke katika usafi kwa kiwango kikubwa
e. Tohara inamfanya mwanamke aolewe kiurahisi na wanaume wanaopenda wanawake waliotahiriwa. Bila kutahiriwa "amekula wa chuya".

duu hii kali, mana kuna mdada mrembo sana 2po nae ofcn, na kila mwanaume akija ofcn anavutiwa nae, lakini wakitoka kwa muda mkaka anakimbia mazima, kuna cku akanielezea shida yake kwamba wanamimba coz ametahiriwa na wengine ni kutoka kwnye mkoa aliotokea huyo mdada huko singida, sasa nikickia unasema wanalewa kirahic nachoka kabisa, ninavyojua mwanamke alietahiriwa hana mccmuko wowote na mwanaume anaelala nae ha enjoy lolote.
 
Tohara ni nzuri kwani inapunguza mwanamke kuwa kicheche kwa namna fulani.

Wasizuie kukeketa.
 
duu hii kali, mana kuna mdada mrembo sana 2po nae ofcn, na kila mwanaume akija ofcn anavutiwa nae, lakini wakitoka kwa muda mkaka anakimbia mazima, kuna cku akanielezea shida yake kwamba wanamimba coz ametahiriwa na wengine ni kutoka kwnye mkoa aliotokea huyo mdada huko singida, sasa nikickia unasema wanalewa kirahic nachoka kabisa, ninavyojua mwanamke alietahiriwa hana mccmuko wowote na mwanaume anaelala nae ha enjoy lolote.
Pole yao hao wanaume hawajui kitu. Mbona wenzao wanawafikisha "Kibo peak"? Mtihani mgumu, eti? Eee, ndo kukomaa huko. Unajifunza kwenda mwendo wa kobe. Mtafika tu!
 
Sioni ni kwa vipi tohara inaweza kuzuia UTI (Urinary Tract infection)!

Nakubaliana na wewe kwamba kampeni nyingi zimelenga kuondoa mila hizi 'potofu' bila kuangalia namna ya kuretain faida zake au kutafuta mbadala ambao utawezesha jamii zinazohusika kufikia malengo yao.

Kama lengo la tohara lilikuwa kumfanya mwanamke atulie (na kweli alikuwa 'anatulia'!), tunaposema sasa tohara marufuku, tunafanya nini kuendelea kumsaidia mwanamke atulie? Nadhani hapo ndio kwenye tatizo: mzungu akisema hii ni potofu, waafrika tunabeba 'wholesale' bila hata kuchekecha!
Kile kinachokatwa ni kama kidole ndicho kinachihifadhi uchafu hivyo kikikatwa kinakuwa safi kama mwanaume anapoondolewa govi.Hali kadhalika kile kidole ndicho kinachosababisha uhuni kwa wasichana.
 
Ukiona jambo linakazaniwa KUTOKOMEZWA ujue linamadhara, ukubari ukatae. Habari ndio hiyo. TOHARA INAMADHARA

Mfano: 1.Kovu la tohara HALIFUTIKI wakati wa kujifungua
linapasuka anaweza weza kupoteza maisha kama
ajakimbizwa hospital.

2. Wwanaume kutahiliwa HAKUNA MADHARA, damu sio
nyingi inadhibitiwa bila ya kupelekwa hospital.

3. Sijawahi kusikia mtu mzima au mtoto katahiliwa
katokwa damu nyingi kakimbizwa hospital, mtu mzima
au mtoto akitahiliwa akapona FOREVER NO P.
4.Mimi tulikuwepo wali 18 kijijini tulitahiliwa wote salama
FOREVER NO PROMBEM

KUHUSU WANAUME SHWARI
WANAWAKE SIO SHWARI

MBONENYAI.
 
What are you talkin about BABU YAO for GOD SAKE,
a) hiyo visible sign ya kutoka utotoni kwenda ukubwani MUNGU alishaiweka jamani si ndio wanaume kubalehe na wasichana kuvunja ungo(a girl start to Menstruate)
b) hivi kwenye hiii nchi yetu ya kimaskini kwasababu ya ufisadi hivi inahitaji ukeketwe ndio usione ugumu wa maisha ? na hao wasiokeketwa ndo kwamba hawawezi kuvumilia huo ugumu wa maisha? si ni kutesana tuuuu...
c) from that point of view kwamba kupima kama kina baba wanaweza kuwavuta taratibu kwa ubingwa wao katika masuala ya tendo la ndoa mpaka wakawaweka katika hali ya hamu ya kufanya mapenzi. WANGAPI WANAFAULU KWENYE HILO ???????? do you know over 70% of women they dont reach orgasm? that means most men they do not succeed on satisfying their partners. hiyo inajumuisha na wasiokeketwa ,sasa kwa mtindo huuuu huoni kwamba waanawake wengi waliokeketwa wanateseka? wanakuwa kama chombo cha mwanaume kujistarehesha badala ya kuwa mwenza katika kustarehe na tendo hilo.
d)Nani aliyesema uchafu wa mwanamke uko kwenye Clitoris? wewe kama mwanaume unakubali hilo? that means humjui mkeo/patner wako vizuri.
e)na hilo la kwamba Tohara inamfanya mwanamke aolewe kiurahisi na wanaume wanaopenda wanawake waliotahiriwa. Bila kutahiriwa "amekula wa chuya". Hivi kweli jamani upendo unaaanzia kwenye kukaguana kama umetahiriwa au laaah? au mwenzetu unaanza kufanya mapenzi na mwanamke ukiona ana tohara ndo uamue kumpenda? utasex na wangapi? is this means muonekano na tabia ya mtu kwako havina thamani zaidi ya tohara?then wee unafall kwenye kauli Men fall inlove through sex en women through love nha?

nyongeza kwa wale wanaosema tohara inapunguza mwanamke kuwa kicheche? na hao wanaume waliotahiriwa ambao ndio wanaongoza kwa ukicheche inakuwaje? ukicheche ni tabia ya mtu utahiriwe usitahiriwwe ukiwa kicheche ni kicheche tuu,tena aliyetahiriwa ndio yuko mashakani zaidi kwasabbu atakuwa hatoshelezwi atakuwa anajaribu kila mwanaume mwanaume nyie mnasema kicheche kumbe mwenzenu anatafuta kutosheka.

N:B najua wapo ambao mapatner zao au wake zao wamekeketwa , ndio ishatokea tuchukulie hiii kama changamoto ya kumjali zaidi mwenzio kuona kwamba ana mapungufu flani kwa hiyo unahitaji mbinu na jitihada ili umtosheleze, lakini isiwe ndio kisingizo cha kumbbwaga mwenzio kisa kakeketwa au kisingizio cha kutetea huuuu unyanyasaji wa kijinsia kisa mkeo kakeketwa
 
Nimefuatilia sana wanaopinga tohara kwa Wanawake, lakini wanataja hasara tu.Faida nilizosikia kwa kuwahoji makabila yanayokeketa Wanawake ni haya yafuatayo:-

1. Kuzuia U.T.I kwa watoto wa Kike.
2. Kupunguza msuguano wa uke na hivyo kupunguza ashki ya kingono kwa Msichana.
3. Kuzuia uhuni/umalaya kwa Wasichana/Wanawake.
4. Kumuweka Msichana katika hali ya utuuzima.
5. Kumfanya mwanamke atulie katika Ndoa.

Wana JF haya niliyosikia ni ya kweli katika hali halisi ya maisha?

Haina Faida yoyote!!! Ni unyama tu.
 
Haina faida yoyote..................

honestly it cuts down on the fun the man and his wife will have together.
 
Faida kwa nani?
Hasara kwa nani?
Tohara ni desturi yenye kuleta madhara kwa mwanamke mwenyewe, na hata kama kuna faida haizidi hasara.
Wanaume wenye kuoa wanawake waliofanyiwa tohara hula hasara, Ndiyo maana wengi hutoka nje kufuata wale wasiofanyiwa tohara hiyo!
 
Kile kinachokatwa ni kama kidole ndicho kinachihifadhi uchafu hivyo kikikatwa kinakuwa safi kama mwanaume anapoondolewa govi.Hali kadhalika kile kidole ndicho kinachosababisha uhuni kwa wasichana.

Are you sure Mkuu?
  • Kidole? do u have a clue re:female anatomy?
  • Kidole kuweka uchafu na kusababisha uhuni??? wonders will never ceaze!
Kwa taarifa yako, wivu wa wanaume kuhusu wanawake wao haujaanza tu huku Africa au hata nchi za kiarabu na Somalia kunakofanywa ukeketaji kupunguza "ashki"( excuse for this language maana there is no better way to explain) kwa wanawake.

Kwani Mungu alipomuumba mwanamke na kumwekea hisia na kila kitu kama mwanaume hakujua vyote hadi binadamu aje agundue na kutafuta njia ya kikatili ya kumpunguzia?

Ingeeleweka kama ukeketaji ungekuwa ni njia reversible ambapo muda ukifika basi huyo mwanamke angeweza kurudishiwa kilichofungwa kwa muda.

Wazungu wao walianzisha utaratibu wa kuwavalisha wanawake zao Chastity belts ambapo mume alifunga na ufungo na kuondoka nao...huu mkanda au chupi ya chuma mnaweza kuona ilivyokuwa pia ukatili maana mtu utalalaje na kushinda umevaa chuma?

Anyway the bottomline is.... binadamu huwezi kumchunga kama mbuzi au kumdhibiti.Binadamu/mwanamke atajidhibiti mwenyewe pale atakapoona mumewe au mtu wake anampa heshima stahili.
 
Kusema kwamba kutahiri wanawake ni "female genital mutilation (FGM)" ni sawsawa na kusema "breast implant ni female breast mutilation (FBM)". Tatizo sio kutahiri wanawake au kutahiri wanaume. Tatizo ni Mwafrika kujiamini na yale anayofanya. Mimi naamini wale walioanzisha hiyo tabia ya kutahiri akina mama na akina baba hawakuwa wapumbavu kama sisi leo tunavyoongea kirahisi sababu mzungu fulani kasema hii ni tabia mbaya. Ajali ziko hata hospitalini, lakini hatufunga hospitali. Magari na ndege zinaanguka na kuua watu kila siku lakini hawajafuta kusafiri, fikiri!

Kabla ya kupiga marufuku kutahiri akina mama tufanye utafiti wa kisayansi jamii na tuthibiti nini maana yake kutahiri akina mama. Mwalimu Nyerere alisema shida yetu Waafrika ni kutoa majibu rahisi rahisi kwa matatizo magumu sana. Mimi naongezea kwamba matatizo ya Kiafrika tusiyape kirahisi majibu ya Kizungu, ni kudumisha wendawazimu wa Mwafrika na huo ndio unafanya hadi kesho aonekane nyani tu mbele ya binadamu wengine.

Kutahiri si kukeketwa na wala tafsiri yake kwa kiingereza si 'mutilation'. Wanaotudanganya kwa maneno hayo wao wana vitu vinaitwa 'tatoo' wana 'body piercing' na plastic surgery hata organ transplants. Mambo hayo wanayafanya sehemu mbovu na ngumu! Wakati mwingine wanatatoo na kupierce hata watoto wadogo wasio na uamuzi wa hiari. Je hawa wanakeketa na ku-mutilate?

Leo kuna utafiti unaobaini kwa kiasi cha kutosha kwamba wanaume wanaotahiri ni vigumu kidogo kuambukizwa virusi vya Ukimwi na tayari kuna mbiu ya kutahiri watu ili wajinusuru na Ukimwi. Wabongo muna habari? Si muda itakuwa sheria Tanzania wanaume wote lazima kutahiri! Bottoms up!!!!!??? Hey!

Tufanye utafiti kabla ya kuiga vitu kama madodoki yasiyo na vichwa. Mungu hajaleta duniani wali wala ugali. Mbona tunaswaga pilau bila kusema huo ni uchafuzi wa mchele? Mungu katupa akili na yafaa tuitumie!

Tuache kuiga, kutoa majibu rahisi rahisi kwa matatizo magumu na kuyapa maswali ya Kiafrika majibu ya kizungu! Matatizo yanayotokea wakati wa kutahiri akina mama tuyatafutie ufumbuzi, hatuwezi kutupa jongoo na mti wake tukawa kweli wasomi wa karne ya ishirini na moja. Tusiwe kasuku! Tufikiri kabla ya kulaani mila na desturi ambazo mababu zetu walizijenga kama wanafalsafa.

Denyutali,

Makanjaula
 
Last edited:
Back
Top Bottom