MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Yaliyotokea katika chaguzi kuu za nchi za Togo, Burundi na Malawi yameonyesha kuwa nchi za Afrika zinaweza kufanya Uchaguzi Mkuu ulio huru kwa amani na utulivu lakini kikubwa zaidi, zikapata viongozi wake bila kutegemea jicho la waangalizi wa kimataifa walioko nje ya Afrika.
Janga la COVID-19 limetoa funzo muhimu kwa nchi za Afrika kuhusu uwezo wa kuendesha chaguzi zake kuu bila kutegemea ''kiranja'' anayetoka nje ya Afrika (Ulaya na Marekani).
Walianza wananchi wa Togo ambao mwezi wa pili (February) walipiga kura za kuwachagua viongozi wao bila ya uwepo wa wasimamizi kutoka nje ya Afrika. Uchaguzi ulimalizika kwa amani na utulivu ambapo asilimia 76 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura .
Zoezi hili lilifuatiwa na nchi ya Burundi ambayo nayo mwezi wa tano (Mei), walifanya Uchaguzi wa amani na utulivu bila ya uwepo wa waangalizi kutoka nje ya Afrika. Uchaguzi ulimalizika kwa amani na utulivu ambapo asilimia 88 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura.
Nchi ya Malawi imekuwa ya tatu kufanya Uchaguzi Mkuu bila uwepo wa waangalizi wa nje ya Afrika. Uchaguzi wake umefanyika kwa amani na utulivu ambapo asilimia 64 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura.
Nchi ya Ethiopia ambayo ilikuwa pia inategemea kufanya Uchaguzi Mkuu mwezi wa nane (Augosti) bila waangalizi wa kutoka nje ya Afrika lakini Waziri Mkuu, Abiy Ahmed ameahirisha Uchaguzi huo bila kupanga tarehe nyingine. Maamuzi haya yamemfanya Spika wa Bunge kujiuzuru akimtuhumu Waziri Mkuu kwa kuvunja katiba kwa kuendelea kuwa madarakani baada ya muda wake wa kikatiba.
Mwezi wa tisa (Septemba) tutashuhudia pia wananchi wa Jamhuri ya Shelisheli wakipiga kura ya kumchagua Rais wa nchi bila uwepo wa waangalizi wa nje ya Afrika.
Baada ya Jamhuri ya Shelisheli, Tanzania tutafuatia mwezi wa kumi (Oktoba).
Chaguzi hizi zote zimedhihirisha na kutoa angalizo kuwa chaguzi nyingi katika nchi za Afrika huwa zinakuwa sio za amani na utulivu kutokana na waangalizi kutoka nje ya Afrika (Ulaya na Marekani) kuwa na ajenda zao zinazosababisha kuvunjika kwa amani na utulivu katika nchi za Afrika.
Nchi za Afrika zimekuwa zikiaminishwa kuwa bila kuwa na waangalizi kutoka nje ya Afrika (Ulaya na Marekani), basi Uchaguzi hauwezi kuwa huru nawa amani na utulivu. Janga la COVID-19 limeondoa hii mithiologia.
Nchi za afrika kwa sasa zimeonyesha uwezo mkubwa katika kuendesha chaguzi zake huru na zikamalizika kwa amani na utulivu chini ya waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika na asasi za kiraia za ndani ya nchi zake.
Huu ni ushindi mkubwa kwa nchi za Afrika.