SoC01 Tofauti za Kiuchumi (Kati ya walionacho na wasionacho), Nini kifanyike?

Stories of Change - 2021 Competition

minisalmin

New Member
Sep 17, 2021
1
0
Sote tunakubali uwiano usio na usawa wa kiuchumi kwa maana ya wingi wa wasionacho na uchache wa walionacho unaopelekea baadhi ya mambo ama tabia zetu na hata mahusiano yetu kuathirika kwa namna moja ama nyingine. Leo ningepende kurununa (share) nanyi baadhi ya mawazo yangu juu ya nini kifanyike kuepukaa/kubadili/kukabili hali hii inayoumiza jamii yetu kwa kiwango kikubwa mno. Umasikini kama moja ya athari /matokeo anuai ya Ombwe (Gap) hili na pia huleta changamoto nyingi sana na kutoa tafsiri halisi ya nini jamii inasumbuliwa na mabadiliko haya ya tabia za kiuchumi.

Nitatazamia katika pande zote mbili (Serikali na M(W)ananchi).

Kwa kuanzia tuanze na Wa(Mw)nanchi.

1- Kujifunza kuhusu Uchumi na tabia za Uchumi.
Tulio wengi suala la uchumi tumeliacha kama jukumu msingi la serikali, hii si sawa hata kidogo. Lazima tujifunze uchumi, tuupende uchumi na tuishi katika uchumi ili kuweza kuondokana na athari za kiuchumi tulizonazo. Elimu ya uchumi itatusaidia kudhibiti matumizi yetu, matamanio yetu na utafutaji wetu. Naomba tujiulize kitu, kama sote tunatafuta fedha/pesa hivi tumewahi kujiuliza..
Kiasi gani?
Kwanini? na
Kwa ajili gani?
Hatuoni ajabu unapata fedha nyingi na baada ya muda unakua masikini? au tunatafuta, tunapata na hatuoni kama tumepata? Tujifunze Uchumi na Tabia zake.

2-Badili Mazoea (Tabia)
Tumezoea kutumia fedha kama kitakatishi mahitaji na kusahau Akili na Afya kama msingi wa upatikanaji wa fedha. Ndugu zangu mazoea yetu ndio hujenga maisha yetu. Tumebarikiwa mitandao na simu janja kama visimbuzi taarifa na arifa lakini tumekua nyuma sana katika kupata taarifa sahihi zenye tija na faida katika maisha yetu. Ni wakati sasa kubadili mazoea na kujenga mazoea mapya.
mfano:- Kutafuta maarifa (kujifunza) pasina aibu.
Kudadisi vitu, matukio na hata mwenendo.
Kujiuliza maswali na Kujitafuta wewe mwenyewe ni nani na una uwezo gani.

3-Kubadili Fikra/Maisha/Watu/Vitu
Wajuzi wa manbo husema, ulivyo ni matokeo ya vile vinavyokuzunguka na usemacho ni matokeo ya kile ufikiriacho. Ni wakti sasa kujiuliza tunakwenda mbele ama nyuma?nTuna marafiki wenye kutosheleza kutupa hamasa ya kuvuka hapa tulipo? Je umasikini kwetu ni mazoea na haki ama changamoto na fursa ya kua bora zaidi? Badili fikra yako uione dunia katika uso wa tofauti na mengi mazuri yaliyopo, usione aibu kubadili watu ulionao, muda haukungoji anza sasa.

4-Futa aibu
Wengi tuna aibu sana katika kuziendea ndoto zetu, tunabeba amana ya fikra za watu juu yetu na kusahau malengo yetu. kwa kila tukifanyacho tumekua watu wa kutaka hiyari na salama kwa watu badala ya kutazama nini chenye manufaa kwetu na malengo yetu. Futa aibu.

Kwa machache naomba niishie hapa ili nipate fursa ya kuzungumzia Serikali kama mlezi/Mjenzi na mhimili wa watu katika nchi/Eneo husika.

Kwa upande wa SERIKALI

1- Bana Matumizi

Mara ngapi tumeliskia ama kulisoma hili neno "Matumizia ya Kawaida"? sina ubaya nalo ila nataka tujiulize ni yepi hasa? (si kwamba hayana umuhimu, la hasha) ukitazama uwiano wa matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo kuna utofauti mkubwa sana unaopelekea kuhitaji kujitathmini kulingana na mahitaji yetu. Ni muhimu serikali kubana matumizi hasa katika maeneo ya Malipo, Matumizi na Huduma (hasa zenye kulenga watu wachache)

2-Dhibiti Manunuzi
Tunajua serikali ni mdau mkubwa na mzuri sana wa maendeleo na uchumi kwa watu wake, lakini ni muhimu sana kujitazama namna/mtindo wa manunuzi. Yeye (serikali) ndio chombo pekee/Mnunuzi mkuu wa vitu/huduma kutoka kwa taasisi, watu au mataifa mengine. Ni muhimu sana kudhibiti manunuzi yetu, kupanga umuhimu wa mahitaji kulingana na kilichopo na mipango yetu, sisemi manunuzi hayana umuhimu, la hasha tujaribu kuangalia namna bora, nyepesi na nafuu ambayo haitaleta ongezeko la gharama kwenye uendeshaji ama usimamizi wa kile tunachonunua.

3-Uza Ubunifu Kidigitali (NFT)
Sanaa imekua eneo Hame (sahaulifu) katika mapana yake kama kiungo mtaji wa kiuchumi kwa jamii, wengi wetu tunatizama Muziki, Mpira, Uigizaji, Uchongaji (kidogo) na Uchoraji (pia kidogo). kama serikali ni wakati sasa wa kuendana na dunia ile inakwenda, lazima kuanzisha taasisi imara zenye kushiba wabobezi wa tafiti, chokozi, udadisi na ushawishi katika kuinua sanaa kwa ujumla wake.

Tambua aina, viwango na idadi ya sanaa ulizonazo,
Sajili na kuzipa hadhi stahiki huku ukiifunza jamii umuhimu ubora na thamani ya kile wanacho
Wezesha sanaa kukua kwa kutengeneza mazingira shawishi, wezeshi na lainishi watu kushiriki kikamilifu,
Linda kisha uza sanaa yako duniani huku ukiingizia mapato nchi Maisha yote (life time), swali (najua lipo) kivipi? kiaje? naam

Kwa sasa kuna kitu kinaitwa None Fungible Token (NFT), hii ni platform yenye kutumia crypto technology ya blockchain yenye uwezo wa kusajili sanaa, vitu ama shairi au chochote kile kwa kukipa Digital Unique ID ambapo mtanzania anauwezo wa kuuza popote duniani pasina mahitaji ya usaili wowote wa kibiashara na kuingiza fedha yake akiwa huko huko aliko bila nguvu kubwa ya matangazo. (Wataalam wa Crypto naomba msaada zaidi)

4-Wekeza zaidi Elimu Maarifa na si Elimu Taarifa
Ashakum sibezi wala kudhihaki Elimu itolewayo hapa nchini, kwanza niipongeze serikali kwa jitihada kubwa na msukumo mkubwa unaoiweka katika elimu yetu, kwa namna moja ama nyingine tumekua mfano mzuri sana kwa wengine juu ya elimu yetu tunayoitoa hapa nchini. Niiombe maboresho kidogo hasa ukizingatia mrengo wa elimu yetu upoa katika Nadharia zaidi kwa maana ya taarifa/Mapokeo, hii humnyima kijana fursa ya ubunifu.

Kasi ya mabadiliko ya tabia yakiuchumi ya kidunia haimpi nafasi kijana kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na mahitaji ya kidunia kwa kiwango na aina ya maarifa kijana anayapata, ushindani ni mkubwa na mkali sana, tunahitaji zaidi maarifa na si taarifa mana Internet imetusaidia kuzikusanya taarifa sasa ni wajibu wetu kuwekeza katika uchujaji na udahili maarifa sahihi kwa watu wetu.

Changanua elimu kikanda/kulingana na mahitaji au uwepo rasilimali kwangu mimi nadhani kuna faida zaidi kuliko mfumo mmoja unaolazimisha watoto kujifunza cha pamoja kutoka katika tamaduni na asili tofauti.

Tuna Tumbaku, Mkonge, Muwa, Pamba, Mpira, Zabibu, Ndizi, Miti, Nyama nk nk tuielekeze elimu yetu katika kufundisha watu wetu vitu walivyonavyo katika maeneo yao huku tukiruhusu uhuru wa chaguzi za kusomea kulingana na mapenzi tu ya mtu, mfano Arusha kuna Wafugaji wengi japo kuna madini lakini wengi wa watoto wa wafugaji Wanasomea Ufugaji na si Madini kwanini? Wameiona thamani ya maisha yao katika mifugo vivyo hivyo na maeneo mengine tufanye/ kuweka utaratibu utakaoakisi maisha halisi ya watu wake ili kutia wepesi na ari ya Maarifa kufika na kunufaisha jamii kwa wepesi.
Fundisha vijana ujuzi utakaowapa thamani na kukua wakiutendea kazi badala ya kuwaandaa vijana kushiriki michakato tumizi/usimamizi, tuwekeze kimkakati katika vyuo hasa vya kati na zaidi tena kwa mpango maalum kwa Vyuo Vikuu kama taasisi muhimu za kitafiti huku tukizipa nafasi kushiriki katika masuala mbalimbali kwa ujazo wake. (sisemi havishiriki, tupongeze hatua tuliopo na tuwape moyo zaidi)

5- Futa Kodi/Tozo ZOTE zinazohusiana na mchakato mzima wa Uanzishwaji biashara.
Kodi ni LAZIMA na MUHIMU kulipwa lakini, Mpe uhuru mmiliki na mjengee imani ya mafanikio kabla hajaanza na kukua kibiashara hii itaipa nafuu jamii na wepesi katika utoaji huduma na ufanyaji biashara huku ukiboresha VIWANGO vya utoaji huduma /usimamizi wa biashara hizo. kipengele hiki ni muhimu sana katika kukuza mahusiano ya kibiashara na huduma kati ya mlipaji, mkusanyaji na mlaji. sote tunahitajiana kufikia malengo yetu lakini ni muhimu kuzingatiana katika kuyaendea malengo hayo.

6-Tumia Mifumo ya BIMA Kuinua chumi za wanachama/wananchi badala ya Kuchuma chumi zao.
Mifumo ya Bima ni muhimu na bora sana ikiratibiwa kibiashara zaidi ya huduma ingawa yaweza kua katika taswira na mienendo ya huduma. Weka mfumo utakaowawezesha wanachama kuvuna wanachowekeza pasina kusubiri kipindi fulani, hii itawezesha kukuza ushawishi na kuleta tija na wepesi wa moja kwa moja kwao na kwa serikali kupitia makato ya kodi (ambayo itakua ni ndogo) kwenye ile faida ipatikanayo na kugawiwa (dividend). Mfano NHIF yaweza kuwa ni Universal in free signup na LAZIMA kwa wote lakini ikawa na makato ama michango ya kiwango chepesi au kidogo kulingana na tathmini zitakazofanyika kumpa uhuru mwanachama kufurahia uanachama wake, labda 10K kwa mwezi kwa wakazi wa mijini na 2k /1k kwa wakazi wa vijijini, nao hawa (NHIF) wapewe ruksa ya uwekezaji katika maeneo yao ama yatafiti/viwanda/huduma kuweza kuongeza thamani ya mapato yao huku ikiweka malengo ama mikakati ya kutoa huduma bure kwa wanachama wake wote nchini, Hili linawezekana likitiliwa nia nzuri na utayari wa watu.

7-Rekebisha mifumo yote ya kibenki kutoka kwenye Biashara kwenda kwenye huduma.
Au ibaki kibiashara lakini yenye kumnufaisha mmiliki/mjenzi/mwekezaji kwa maana ya mteja. najua ni pagumu hapa lakini si mbaya kujaribu kwanini? naomba niulize swali na ntafurahi sana bankers wakinijibu,

Watu wakiacha kukopa, nini Bank itafanya? Au ni mikakati gani tuliyonayo kujiendesha pasina watu kukopa?
najua tutasema watu hawawezi acha kukopa, ni sawa lakini ikitokea hivyo what next? je ni sera zinatuzuia sisi kuwekeza maeneo mengine kama taasisi? ni kanuni zetu zinatuzuia kumpatia faida aliyetupa fedha yake kumtunzia sisi tukaitumia kuwekeza? tunasema tunabeba risk kubwa kufanya hivyo yes ndio maana kuna Bima, hata mteja kutunza fedha yake bank ni risk kubwa vile vile.

kwanini we rahisi kukopa at the interest of 10% huku tukilipa fixed interest kwa same amount kwa 3/5%? umegundua nini? ashakum siwachongei bankers na taasisi za fedha mnafanya mambo makubwa sana lakini naonelea tunaweza kwenda mbali zaidi ikiwa tutafanya kitu kustawisha mahusiano yetu na watu wetu. Leo bank kukopa mpaka uwe na Mali isiyohamishika ikiwa mteja hana hatuoni kama anakosa fursa muhimu huku na sisi tukijikosesha mapato na serikali kukosa donge nono? kwanini tusitumie njia mbadala ikiwa mteja mfano ana sanaa yake yenye thamani ikatumika kama dhamana badala ya hiyo mali isiyohamishika? (ndipo linakuja na kupata umuhimu lile suala la NFT).

kwanini wazo la mtu lenye faida na tija lisitumike kama mtaji anzia na dhamana kwa kile anahitaji kukifikia? je ni sheria zinazuia kuwekeza katika tafiti kwenye masuala ya kifedha ama ni siri za kibiashara na ni muhimu kubaki sirini?
nafkiri yaweza maoni yangu yasiwe sahihi ila tunaweza pata kitu ama kufanya jambo kufikia malengo ya usawa kiuchumi ili kuzuia athari zinazoweza kutokana na ombwe (GAP) hilo.

Kwa Muhtasari naomba niishie hapa kwa sasa.

Ahsante.
salmin
WhatsApp 0714229407
 
Back
Top Bottom