Tofauti za kisiasa kati ya kizazi cha Dotcom na kile cha SLP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti za kisiasa kati ya kizazi cha Dotcom na kile cha SLP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Jul 16, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima mbele kama kawaida,
  Walau hadi sasa tunaweza kuandika tofauti za kisiasa kati ya kizazi cha Dotcom na hiki cha SLP. Tofauti hizi ni kama ifuatavyo:-
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]No
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Kizazi cha Dotcom
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Kizazi cha S.L.P
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](i)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wengi ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wengi ni wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](ii)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wengi wanaamini CCM itaanguka katika uchaguzi ujao
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wanaamini CCM itatawala milele
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](iii)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Siku zote wanasifia CHADEMA na kuiponda CCM
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Kuna wakati wanakiponda sana chama chao na kuisifia CHADEMA na kinyume chake
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](iv)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wanaamini kwamba kuchokwa kwa CCM kunatokana na kutawala kwa muda mrefu. Tuhuma za ufisadi ni nyongeza tu ya hiyo sababu kuu.
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wanaamini kuchokwa kwa CCM kunatokana na kuwakumbatia watuhumiwa wa ufisadi. Wanadai wakifukuzwa watuhumiwa wote Chama chao kitaimarika
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](iii)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wanasema mgombea wao wa Urais mwaka 2015 ni Dk Willbrod Peter Slaa
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Hawajui ni nani atakuwa mgombea wao wa Urais hadi sasa. Wengine wanasema Edward Lowassa, wengine Benard Membe, Samwel Sitta, Steven Wassira nk.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](iv)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wanapenda maandamano kushinikiza serikali kutatua kero zao
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Ni waoga wa kuandamana kudai haki zao. Kwao maandamano yanaleta fujo na uvunjifu wa amani, hivyo wanaogopa kukamatwa na Polisi. Na wanaamini waandamanaji ni wahuni wa mitaani wasio na kazi za kufanya
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](v)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wanaamini uongozi wa serikali za CCM tangu tupate uhuru hazijafanya lolote nchini
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wanaamini Serikali za CCM zimefanya mengi mazuri. Wanataja Shule za kata, Barabara za lami, amani na utulivu, Uwanja wa Taifa wa kisasa nk
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](vi)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wengi wanafahamu Mabalozi wa Nyumba kumi kumi si Viongozi wa kiserikali.
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wengi wanaamini Mabalozi wa Nyumba kumi kumi ni Viongozi wa kiserikali.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](vii)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Wengi ni wahitimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Kwa kifupi ni kundi la vijana wenye damu inayochemka
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Wachache sana ni wahitimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Wengi wao ni kizazi cha miaka ya 1960 kurudi nyuma. Ni wazee wenye damu iliyopoa
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](viii)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Ni wasomaji wazuri wa habari kwenye mitandao ya kompyuta
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Si wasomaji wa habari kwenye mitandao kutokana na kutokuwa na ujuzi (utundu) wa kutumia kompyuta
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](ix)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Si wafuatiliaji wazuri wa habari kwenye magazeti. Wananunua gazeti pale anaona kuna habari imemvutia au kuna Makala ya Mwandishi flani anaifuatilia.
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Ni wafuatiliaji wazuri habari kwenye magazeti na ni wasikilizaji wa vipindi vya Redio nyakati za asubuhi vinavyosoma vichwa vya magazeti. Wananua magazeti kama utamaduni tu lakini hawayasomi zaidi ya 35% ya gazeti zima. Wengi si wasomaji wa Makala za kisiasa
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 43, bgcolor: transparent"](x)
  [/TD]
  [TD="width: 309, bgcolor: transparent"]Mifano ya kizazi cha Dotcom ni watu kama Mnyika, Zitto, Wenje, nk
  [/TD]
  [TD="width: 287, bgcolor: transparent"]Mifano ya kizazi cha SLP ni Pius Msekwa, William Malecela, Anna Abdallah, Steven Wassira nk
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  TUMBIRI (PhD, University of HULL - Hull City, UK),

  tumbiri@jamiiforums.com
   
Loading...