Tofauti Za Kimaisha Kati Ya Watanzania, Je Tunahitaji Azimio Jingine?

kaisa079

Member
Nov 16, 2007
20
4
Wakati Fulani miaka kadhaa iliyopita,wakati ambao hata mimi nilikuwa sijazaliwa lilipitishwa Azimio la Arusha.Hii ilikuwa juhudi mojawapo ya Rais wa wakati huo Marehemu Baba wa Taifa kujaribu kujenga usawa wa kimaisha kati ya Watanzania kwa kuliziba pengo kubwa lililokuwepo kati ya Mabepari wachache wa wakati huo na masikini waliokuwa wengi.

Miaka kadhaa imepita tangu azimio lilivyopitishwa na mali nyingi kutaisfishwa kuwa za umma.Hata hivyo mambo yamerudi kuwa vilevile kabla ya Azimio la Arusha na pengine hali ni mbaya zaidi kuliko wakati ule!kwani kumekuwa na pengo kubwa kati ya Matajiri na Masikini wan chi hii.

Hii ndiyo hali halisi huku wa Masaki,Oysterbay na Masaki wakiishi mahekaluni wakati wa Buguruni,Manzese ,Temeke n.k wakibanana ktk vyumba finyu wa kupanga na vyoo vya passport size,laity kama wote tungekuwa sawa!

CHUO KIKUU
Wakati nikichukua shahada yangu ktk chuo kikuu kimojawapo hapa nchini,mara Ghafla serikali ikatangaza ofa kubwa tu kwa wanachuo waliokuwa wanasoma Private kwamba sasa watapewa udhamini na Serikali,hakukuwa na sababu za msingi sana zilizotolewa na serikali ya wakati huo,tukawashuhudia watoto wa wanene hao wakininufaika na udhamini wa serikali huku wengi wao wakiwa ni wa wazazi ambao wana mipesa kibao,nasema hivyo kwa sababu hakuna mtanzania mwenye kipato cha kawaida ambaye angemudu gharama za kumlipia mwanae ada ya chuo kikuu zaidi ya kusubiri neema ya kupewa udhamini wa serikali.Ikumbukwe kuwa wengi wa waliokuwa wakilipiwa ada ni wale ambao kwa aina moja au nyingine awali walishindwa kukamilisha utaratibu wa kulipiwa na serikali na wakaepuka usumbufu kwa kuamua kulipia ada wenyewe.

Hao hao wakaja kupewa tena udhamini na serikali huku watoto wa wachovu wasiohesabika wakiwa wameachwa kwa sababu ya umasikini wao.Matokeo ya zoezi hilo la serikali ni kuzalisha wanavyuo waliojua kutumbua mifedha hasa!.Wakati wengine walitegemea fedhahiyohiyo ya mkopo kuwasaidia wadogo zao na wazazi wao huko vijijini,wengine wakawa wanajiuliza wazitumie fedha hizokwa starehe zipi.Kwa wakati huo hata kipofu angeweza kumtofautisha motto wa tajiri na motto wa masikini.Ilifikia wakati motto wa kigogo mmoja alimkejeli motto wa mkulima kuwa anawezaje kuishi kwa kutegemea pesa ya mkopo pekee?

Hata hivyo maisha yaliendelea na miaka michache tu baadaye wanavyuo wakatakiwa kuchangia 40% ya ada,wengi walishindwa na kati ya walioweza kulipa wengi wao ni wale waliokuwa wamepewa fadhira na serikali na ama walikuwa ni watoto wa wenyenazo! Hapa tunaona jinsi matabaka ya kiuchumi yanavyojitokeza vyuoini.

HARARE, ZIMBABWE
Rais wa Zimbabwe kipindi Fulani aligundua kuwa bila ya kuchukua hatua za haraka tabaka la Wazungu wachache litatawala uchumi wan chi huku wazawa wengi wakiwa vibarua katika mashamba yao,akaamua kutaifisha mashamba na kuwagawia wananchi,kwa mabepari wengi huu ulionekana kama uonevu n nchi za kibepari zikamwekea vikwazo tele Rais Mugabe lakini lwa mujibu wa chombo kimoja cha habari cha nchi hiyo,hatua hiyo ilipokelewa kama ukombozi wa masikini kwa watu wengi wa hali ya chini.Tumeshuhudia Mugabe akiendelea kupewa kura na wananchi,kura ambazo ndizo zimebaki kuwa sauti pekee ya Masikini walio wengi dhidi ya Mabepari.

ELIMU YA MSINGI
Shule za st.ambazo watu hulipa ada hadi milioni kwa mtoto wa chekechea huku wanafunzi wa shule za sirikali

BARABARANI
Wenye nazo wakitembelea magari yenye vioo vya tinted na viyoyozi wakati walalahoi wakijambiana katika vidaladala ambao wengine hudiriki kugeuza vioo kuwa milango ya kupitia wakati wanagombea magari

HOSPITALI YA TAIFA
Mambo ya FAST TRACK na IPPM wakati walalahoi wakilazwa wawili wawili hadi wannewanne katika wodi za kibasila,mwaisela na sewahaji

MAHOTELINI
Tukiwa tunahudhuria Hafla Fulani katika hoteli moja ya kitalii hapa nchini utaonana watu wanavyojua kuzitumia ndugu yangu zile ambazo wa chini twajiuliza tutazipata lini wenzetu wanajiuliza wazitumieje?

KATIKA KUOA
Umefikia wakati unapomwomba rafiki au ndugu akupe mchango wa Harusi maswali kama vile mkeo anafanya kazi gani? Anasoma wapi? Au ana elimu gani?

Haki ya nani ndugu zangu nawaambieni sasa ni wakati ambao wasomi wanaoana wenyewe kwa wenyewe na kuzaa watoto wasomi zaidi,matajiri wanaoana wenyewe kwa wenyewe wanazaa watoto na wajukuu matajiri zaidi wakati masikini wanaoana wao kwa wao na kuzaa watoto ,wajukuu na hata vitukuu maisikini na fukari zaidi.Imebaki miaka michache sana tuone waziwazi kabisa mgawanyiko wa kitaifa,Taifa linageuka kuwa na matabaka ya kiuchumi japo yalikuwapo toka ukoloni ila sasa yatakuwa wazi na uchi kabisa.Unajua masikini akiolewa au akioa mtoto wa mwenye nacho anasemaje ,amepata zali! hizi ni kauli zinazoonyesha matabaka waziwazi.

Na unajua masikini asivyojua uzazi wa Mpango,kwanza hana TV ambayo ingemkalisha Sebuleni ili akifika kitandani awe amechoka hata kufanya mambo Fulani,lakini starehe pekee aliyonayo ni Ngono! Na ili aridhike kuwa amefanya mapenzi ni lazima ampe mimba mkewe kama si hawala yake.

Mimi ningeshauri tujichanganye jamani,ili wote tuwe katika level moja,sikwambie mtu mimi nikipata ka degree kangu nitajiendea kijijini kwetu nijichukulie masikini mmoja angalau nitamwendeleza japo Mti mmoja hauwezi kutengeneza msitu lakini naamini miti miwili,mitano hatimaye huwa msitu

Kwa leo naishia hapa,Nikipata nafasi nitakuletea majibu ya maswali ambayo ambayo mtu mmoja aliulizwa alipobisha geti la mbinguni.Alitamani arudi Duniani.

Nikuonjeshe Kidogo.Kuna watu hawana nafasi kabisa kule mbinguni,si ahela wala kuzimu wala peponi..kuna watu ambao kwa ubinafsi wao wanajimuvuzisha na mavitambi mbinguni wakati wengine wame slim kama njiti ya kiberitikuna watu waenda na majeneza ya midhahabu,mi silver,mi suti mizitomizito wakati kuna wengene huviringishwa tu ktk kanga au sanda iliyochoka na kusukumizwa tu katika udongo bila sanduku.. (Itaendelea)

Kwa maoni,Ushauri
Niandikie
Kaisa079@yahoo.com
 
(Itaendelea)
NAWEKA KAMBI HAPA SITI YA KWANZA KABISA NGOJA NIIFUTE VUMBI
IMG_7933.jpg
 
Back
Top Bottom