Tofauti ya uzito kati ya mwili hai na mwili mfu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,576
729,449
Nawasikia sana vijana ama kwa utani au kwa kupeana makavu wanapohitalifiana wakiambiana kuwa UTAJIBEBA! Ni neno rahisi kweli na pengine la kizushi hasa kwa muktadha wao...lakini katika ulimwengu wa tafakuri jadidi ni neno tofauti lenye maana pana sana
Mwili hai unajibeba wenyewe ndio maana uzito wake ni tofauti kabisa na mwili mfu...ni rahisi mno kumbeba mtu mgongoni akiwa hai kuliko akiwa mfu!!! Achana na balance uzito wake huwezi kumbeba
Dunia inaendeshwa na nguvu za uvutano unapokuwa hai ili uweze kutembea bila kuanguka kuna nguvu unakubeba....ufahamu wako kiroho unabeba karibia nusu nzima ya uzito wako wote
Ufahamu/roho(energy)ni kitu kikubwa sana na chenye kuubeba mwili wako ili uweze kujibeba na kupunguza uzito ule unaokuja kuongezeka kama roho yako ikiachana na mwili wako...hiki kinachotoweka ndio hicho kinachoongeza uzito uliofidiwa na wewe yaani roho jumlisha mwili...Ni mahesabu kinyume haya
Kwahiyo vijana wetu wakiambizana UTAJIBEBA hawajui tu kuwa wanaongea kitu kikubwa sana
Muwe na alfajiri njema
destruction_sleep_02.jpg
....!
 
Mi mjanja, nshamshirikisha Mungu aweke stop ya mwendokasi.
kuna aya moja kwenye qur'an inasema 'mcheni MWENYEZI MUNGU ukweli wa kumcha' hii sentensi ukiielewa vizuri na ukauelewa uzito wake utaacha kulitajataja jina la Mungu kimzaha mzaha hivyo.
Goodmorning
 
Hivi mtu mwenye mathalan kilo 70 akiwa hai, jee akipimwa akiwa mfu uzito wake utazidi hizo kilo 70?
 
Hivi mtu mwenye mathalan kilo 70 akiwa hai, jee akipimwa akiwa mfu uzito wake utazidi hizo kilo 70?
Itabidi tufanye kwa vitendo na jibu litakuwa ndio
Kwa usahihi wa majibu tutumie kipimo cha scalar
 
Mshana Jr hii kitu haina ukweli Tuchukulie mfano kwa mfugo kama mbuzi mpime uzito akiwa hai halaf muue (bila kumchinja) then umpime tena
Kiumbe kikiwa hai huwa uwezo wa kujibalance uzito wake na viungo vyake hivyo basi hata ukibeba inakuwa ni rahisi ila kikifa kinakuwa hakiwezi kujibalance hivyo basi ile hali ya mbebaji kubalance uzito na kubeaba ndio tunadhani uzito umeongezeka ila ukipima kwenye mzani uzito utakuta ni sawasawa na ule kabla hajafa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom