Tofauti ya tarehe, miaka, na nyakati katika jamii mbali mbali shida ni nini?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,504
30,915
Habari wana JF na poleni sana na ugonjwa huu wa corona, hakika tutavuka kwa kudra za Mola.
Kama mada inavyojieleza nimetafakari sana nimejiuliza maswali mengi kwanini tarehe, miaka na nyakati zinatofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Wachina wana mwaka wao na mwaka mpya wao, waislam wanazo nyakati zao na mwaka wao, halikadhalika wahabeshi na jamii nyingine kongwe. Hii inatokana na nini? Je kwetu Chato na sisi tuna nyakati zetu? Hii inasababishwa na nini? Naomba kujuzwa
 
Hii calender ambayo bongo na nchi nyingi inatumika inaitwa Gregorian calender imeitwa hivyo sababu mtu wa kwanza ku-introduce ni pope Gregory wa 13 mnamo mwaka 1582.

Huyu Papa alicorrect calender iliyokuwa inatumika ya julian calender... hii tunayotumia sasa hivi (Gregorian) inafuata mzunguko dunia kuzunguka jua yaani siku 365 na robo.

Kwahio hizo nchi nyingine inawezekana hazikukubaliana na calender hii au wao wana fact zao nyingine za kuhesabu siku zao.. lakini hii tunayotumia ambayo tuko 2020 ndio the most popular.
 
Kuna matukio yalitokea kwenye jamii fulani ndio yakasababisha kuanza kuhesabiwa tarehe.
 
Habari wana JF na poleni sana na ugonjwa huu wa corona, hakika tutavuka kwa kudra za Mola.
Kama mada inavyojieleza nimetafakari sana nimejiuliza maswali mengi kwanini tarehe, miaka na nyakati zinatofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Wachina wana mwaka wao na mwaka mpya wao, waislam wanazo nyakati zao na mwaka wao, halikadhalika wahabeshi na jamii nyingine kongwe. Hii inatokana na nini? Je kwetu Chato na sisi tuna nyakati zetu? Hii inasababishwa na nini? Naomba kujuzwa
Leo ni tarehe 6/4/2020 duniani kote
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom