Tofauti ya Tanzania, Zambia na Kenya

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
391
kila siku tukisikia mambo ya wenzetu kenya kuhusu siasa na demokrasia yao na hivi karibuni Zambia sisi watanzania wapenda maendeleo ya kisiasa ambayo ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, tunabaki kujiuliza kwa nini hao majirani zetu na siyo sisi. Kumbuka CCM haina tofauti kubwa na vyama tawala vya muda mrefu vilivyotolewa vya KANU, UNiP, na hii MMD sasa tofauti haswa iko wapi? kwa nini sisi tunashindwa wakati CCM yenyewe imechoka kuongoza nchi? mi nafikiri nina point mbili tatu lakini ningeomba michango yenu zaidi

Kwanza, level ya elimu ya Watanzania iko chini kuliko Zambia na Kenya. Hii inaathiri mchanganuo wa kimawazona upeo wa maisha kwa ujumla wa wapiga kura wetu wengi haswa haswa wale walio vijijini. elimu ndogo ni matatizo katika ukuaji wa demokrasia yeyote ile.

Pili, vyombo vya habari hususan nchini Kenya viko imara, vinafanya kazi kwa misingi ya kweli ya kitaaluma katika kuelimisha jamii na havijawekwa katika mfuko wa wanasiasa kama hapa kwetu. Hatuwezi kudharau mchango wa wanahabari katika harakati za kiutawala na kidemokrasia kwa ujumla. Hapa Tanzania waandishi wengi ni mamluki tu wa wanasiasa wanahongwa kagari wanapotosha jamii na media house zetu hazikui kusambaa nchi nzima kutoa mwanga kwa wananchi.

Tatu, Ukubwa wa nchi na gharama za kiuendeshaji, Zambia na Kenya ni ndogo kuliko Tanzania na kuna population density kubwa katika maeneo fulani ya nchi. Hii inakua rahisi kwa vyama vya upinzani kufanya kampeni maeneo hayo kwa ufanisi zaidi tofauti na Tanzania upinzani una kazi ya kuzunguka nchi nzima kutumia gharama kubwa na ufutiliaji unakua mgumu kidogo katika kuona chama kinakua katika maeneo tofauti tofauti ya nchi.

Nne, KANu ilikufa baada ya wananchama wake kuhamia upinzani mwaka 2002, Sata alijitoa MMD 2001 na kuanzaisha chama chake ambacho kimekuja kuitoa MMD. Tanzania CCM ikimeguka itakua neema kubwa kwa upinzani kwani itaonyesha wananchi kua siyo lazima CCM ipate mustakabali wa kuongoza nchi, kwani yenyewe inakimbiwa na kwa hiyo inakufa. Hata Slaa tukumbuke alitoka CCM
 
Mbona hujaongeza sababu nyingine kwamba hata hao wapinzani hawajawafanya watanzania wawaamini kwamba wao ni vyama mbadala vyenye uwezo wa kuwapeleka mbele?
 
Mbopo ahsante sana kwa mchango nafikiri hilo nalo ni moja ya sababu. Wapinzani toka vyama vingi kuanza wametumia muda mrefu kugombania Urais badala ya kukuza vyama vyao kiitikadi na kijiografia. Ahsante
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom