Tofauti ya Suzuki Escudo na Suzuki Grand Vitara/Vitara

Ficus

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
1,440
1,116
Wadau habari za siku? Natumai mtakuwa vyema kwa wagonjwa na wenye matatizo poleni. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, naomba kujua tofauti ya gari hizo hasa kuanzia models za kuanzia mwaka 2005 kupanda maana ukiangalia kimuonekano wa kiumbo hazina tofauti kabisa. Na model ipi ni nzuri zaidi ya nyingine in terms of performance, stability, maintenance etc
 
Attachments

  • 42BE61B4-DD06-4552-B763-057EA3F3EB53.jpeg
    42BE61B4-DD06-4552-B763-057EA3F3EB53.jpeg
    30.2 KB · Views: 206
  • A0C27DC0-A9C7-41D0-9613-25E962C8CE5A.jpeg
    A0C27DC0-A9C7-41D0-9613-25E962C8CE5A.jpeg
    40.1 KB · Views: 193
  • BCD4B7E1-3A9C-4FE5-985A-E3B2AE438386.jpeg
    BCD4B7E1-3A9C-4FE5-985A-E3B2AE438386.jpeg
    51.5 KB · Views: 179
Hiyo ya silver hapo juu ni Suzuki escudo inayofuata ni Vitara na ya chini kabisa ni Grand Vitara zote ni 2008 models.
 
Mi namiliki Escudo vitara tangu 2006 nimeipaki inafanya shughuri za nyumbani siitembelei ila iko imara sana na siwezi kumuuzia mtu.kuna rafiki yangu alinunua grand kama miaka mitano baadae, alikuwa akinipigia simu niende kumvuta. kwenye efficiency especially kama we una shughuri mbalimbali na za masafa ya kwendea nyumbani mfano kama unaishi Dar unatumia kwendea kijijini na mizigo unabebea kinoma, N.B jitahidi kufanya service.
 
Mkuu kama sijakupata vizuri una maana escudo ni nzuri zaidi ya grand vitara? Kumbuka kuwa kuna escudo, vitara na grand vitara na models za kuanzia 2005 kupanda karibia zote zinafanana sana kiumbo!
Sasa hapo ipi ni ipi ndiyo tataizo.
 
Moderators nashukuru kwa kuuleta huku huu uzi, wataalam wa hivi vyombo vya usafiri JF RugambwaYT mng'ato RRONDO Jimmie Gatsby MANI Mshana Jr na wengineo msaada wenu tafadhali.

mkuu habari.... niende kwenye mada moja kwa moja

suzuki escudo , suzuki vitara, suzuki grand vitara hiyo ni gari moja hayo majina yasikuchanganye

first generation ilitoka 1988 ikiitwa suzuki escudo kwa soko la japan Japanese domestic market (JDM) na baadhi ya masoko machache kama asia spec na south america spec

ila kwa soko la US na EUROPE hii gari ilienda kwa jina la suzuki vitara

ilipofika second generation na kuendelea (now wapo forth) jina la suzuki grand vitara likazaliwa

ila ikabaki vilevile kwa soko la japan ikaendelea kuitwa suzuki escudo ila kwa US spec na UK spec ikaitwa suzuki grand vitara

kwahyo mkuu usihofu ukiona inaitwa escudo basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la japan (JDM) then ukiona inaitwa grand vitara basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la US na UK

ni kama tu toyota corola X assista ukiinunua ya asia spec itaitwa toyota altis

na ndio maana unaona hata kuna vitu ndani pamoja na uimara zinaweza tofauti kwa sababu kila moja hapo ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya soko fulani kutokana na vigezo husika pamoja na mazingira

ushauri ukitaka kuchukua ifate inayoitwa escudo sababu hii ni japanese domestic market (JDM) na mazingira yetu tanzania gari zinazoweza kuhimili shida zetu ni hizo JDM

Nina imani maelezo yangu yatakuwa yamekusaidia kidogo
 
Mkuu nashukuru mno kwa mchango wako umeweza kunitoa tongotongo, vipi kuhusu uimara wake, perfomance, maintanance, uwezo wa kuhimili rough road n.k
Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom