Tofauti ya Siasa za Mrengo wa Kushoto, Mrengo wa Kati na Mrengo wa Kulia

Konya

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
921
118
Hivi chama cha siasa kuwa cha mrengo wa kushoto au kulia tafsiri yake ni nini hasa?

Vipi, mrengo wa Kati ndo upi?

Kuna uhusiano gani sasa na mifumo hii ubeberu, ubepari na kijamii(na hiyo mirengo tajwa)?

Na nini hasa nia na malengo ya kuwa kushoto au kulia na maendeleo ya nchi husika kwa ujumla, hasa kwa zile nchi ambazo zina vyama vya namna hii?

Wa wale wataalam wa siasa naomba kufahamishwa...
 
Kushoto ni ma socialist na kulia ni macapitalist.Huko kushoto na kulia pia kuna ma extrems,ma radical
 
Mimi ninavyojua, siasa za mrengo wa kusho huwa zinafanywa na Chama pinzani ambacho kinakuwa kinapingana kisera kwa 100% na chama tawala, na zile za mrengo wa kati(wakati mwingine, mrengo wa wastani) zinafanywa na chama ambacho kinakuwa tati kati ya sera cha chama tawala na zile za chama chenye mrengo wa kushoto.
 
Siasa za mrengo wa kushoto =Socialism
Siasa za mrengo wa kulia = Capitalism e.g. USA, Germany sometimes, UK and many other european countries
Siasa za mrengo wa kati =Social democrat e.g. scandinavian countries
Siasa za majitaka = Siasa chafu, fitina, uzandiku, wizi, e.g. malizia mwenyewe
 
In politics, the Left, left-wing, and leftists are people or views which generally support social change to create a more egalitarian society.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP][SUP][3][/SUP][SUP][4][/SUP] They usually involve a concern for those in society who are disadvantaged relative to others and an assumption that there are unjustified inequalities (which right-wing politics views as natural or traditional) that should be reduced or abolished


In politics, the Right, right-wing, and rightist have been defined as acceptance or support of social hierarchy.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP][SUP][3][/SUP] Inequality is viewed by the Right as either inevitable, natural, normal, or desirable,[SUP][1][/SUP] whether it arises through traditional social differences[SUP][4][/SUP] or from competition in market economies
 
  • Thanks
Reactions: len
siasa za mlengo wa kushoto ni siasa za kijamaa,wanaamini katika umoja,kushirikiana,kusaidiana na mengineyo (socialism)
siasa za kulia ni za kibepari liberals/liberalism wanaamini katika liberty,economic freedom,na mengineyo
siasa za mlengo wa kati hawa hawapo kijamaa wala kibepari
 
kwa uelewa wangu mlengo wa kulia means CAPITALIST ORIENTED POLITICS na kushoto ni SOCIALIST ORIENTED POLITICS. Mlengo wa kati siasa ambazo si za kulia wala kushoto yaani inakopa mambo furani kutoka capitalism na mambo furani capitalism. kwakuwa mfumo wa siasa =mfumo wa uchumi so capitalism ni siasa zinazopendelea watu/taasisi binafsi kumiliki njia kuu za uchumi na siasa za socialism/ mlengo wa kushoto hupendelea njia kuu za uchumi kuwa mikononi mwa dola. UFANANO ni kwamba zote zinalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidika na rasilimali za nchi. siasa za mlengo wa kati ni zile zinazo ruhusu dola pia watu/taasisi binafsi kumiliki njia kuu za uzalishaji yaani kama vile ipo between the two. nadhani umenisoma mkuu.
 
somo zuri sana wengine wanashabikia vyama bila kujua mlengo wa chama hayo maswali waliulizwa Nape na Marando walishindwa kutaja mwelekeo wa vyama vyao ni muhimu kabla hujasapoti chama chochote lazima uwe na mtazamo wako binafsi kama mlengo wako ni wa kulia,kushoto au kati
 
Kuna thread humu mwanzoni mwa mwaka huu kuna mwana JF mmoja aitwaye Mchambuzi aliongelea kwa kina sana kuhusu hiyo mirengo na itikadi pamoja na itiksadi za vyama vya siasa duniani. Ukiipata hiyo thread nadhani itakuwa imekata kiu yako. Kesho nitaitafuta niihuishe ili uione.
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi itikadi za vyama zimebaki katika maandishi tu. Wanasiasa wa kisasa kwenye chama wanafuata infrastructure ya chama na siyo itikadi. Ndio maana perspective politicians will consider CCM, CDM au CUF not beyond, siyo kwa sababu hivyo vyama vingine havina itikadi nzuri, ila ni kwa kuwa havina infrastructure ya kusimamia shughuli zake.
Vyama vya Tanzania vyote kimsingi ni vya mrengo wa kushoto. Vyote vinazungumzia distributive policies, ingawa katika utekelezaji so far CCM ina lean towards the right.
 
Ningependa watu wa kawaida waelewe maana ya mrengo wa kati . mrengo wa kati ninavyouelewa chadema haifuati ubepari wala ujamaa. Naomba wapenda chama tuombe chama itoe ufafanuzi kuhusu nini maana ya mrengo wa kati. Kwa sababu nchi hii ilikuwa ya ujamaa na mizizi ya ujamaa bado ipo. Baadhi mizizi ya ujama ni kama ifuatayo.SERA YA ARDHI, MASHIRIKA YA UMMA, ADHABU YA KIFO INAYOPENDWA NA WATANZANIA,HOJA YA ELIMU KUWA BURE, MADAI YA AZIMIO LA ARUSHA, Mizizi ya ubepari ambayo apendwa ni kama ifuatayo. BIASHARA HURIA, UMILIKI WA MALI, SERA YA UWEKAZAJI, NGO'S, Hayo ni baadhi tu kuonyesha ugumu wa sera nyingine zaidi ya mrengo wakati. Wito wangu kwa chama watoe ufafanuzi kwamba inaamini nini na haiiamini nini mana chama cha siasa lazima iaminishe watu wake kwa yale ambayo inayaamini.Huu ndio muda muafaka. UBEPARI HAUTAFANIKIWA KATIKA NCHI HII WALA UJAMAA. ndugu wanajamvi wapenda mabadiliko mnasemaje kuhusu falsafa hii ya Chadema ya MRENGO WA KATI.

 
Nani kakwambia baadhi ya mizizi ya ujamaa bado ipo? Hujasikia kilimo kwanza katika sera ya ardhi ambako CCM wanasema mzungu aje Mswahili akae pembeni? Mashirika gani ya umma unayozungumzia? Walishakabidhiwa wahindi wakayageuza kuwa go downs. Azimio la Arusha lilizikwa Zanzibar.
 
hayo mambo niliyotaja wameyapuuza ila watu wanayapenda kwa mfano hujasikia watu wakizungumzia azimio la arusha na angalia vita ya ardhi unajua kwa nini ni kwanini kuna vurugu inapotokea mvutano kuhusu ardhi? kwa hiyo hayo hayo yana nguvu bado katika nchi yetu
 
Mlengo wa kat maana yake tunaweza kufuata itikad yoyote inayofaa kwa wakat husika na mahali sahh,sio ccm wanajiita wajamaa wakat ndio mabepal wakubwa kwahyo mlengo wa kat usikusumbue ndugu tena ndio mzur kwa dunia ya sasa
 
Waungwana naomba nieleweshwe maana ya msemo "Mrengo wa kulia/kushoto". Huwa nawasikia sana wanahabari hasa wa vyombo vya kimataifa.
 
Ni aidiolojia ya mwelekeo na msimamo wa kisiasa hasa katika vyama na wanasiasa wa nchi za magharibi. Mrengo wa kulia husimama kwa mwelekeo wa kibepari ilhali ule wa kushoto ukiwa ni wa kishoshalisti.
 
Ni aidiolojia ya mwelekeo na msimamo wa kisiasa hasa katika vyama na wanasiasa wa nchi za magharibi. Mrengo wa kulia husimama kwa mwelekeo wa kibepari ilhali ule wa kushoto ukiwa ni wa kishoshalisti.

umekosea
vice versa is true
 
Back
Top Bottom