Tofauti ya sherehe ya kuzaliwa ukiwa 37 na 73 sehemu ya namba inabadilika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,179
Ukiwa 37 kwa wengi uko kwenye ajira, kama ni mkulima ndiyo wakati wa shamba kukutegemea kwa kiasi kikubwa au biashara inakupa changamoto.

Unahangaika kujenga na kusomesha watoto. Ndoa inapitia changamoto na kuna wakati unajuta kumuoa au kuolewa na yule.

73 Birthday Party ni surprise kutoka kwa wajukuu. Nyumba unayoishi ni ya kwako na kuna wapangaji wanakupa kodi kila mwezi.

Mke/mume wako amekuwa rafiki mkuu kama bado yuko hai. Biashara umewaachia watoto au umeuza. Mwajiriwa anapata kikokotoo.
 
Sky Eclat,
You are not serious, at 73 nowadays bado upo katika ajira ya pili maana ya kwanza (kama ulikuwa serikalini) ilikatika ukiwa 65. Kama ni biashara bado unaisimamia hata kulima
 
You are not serious, at 73 nowadays bado upo katika ajira ya pili maana ya kwanza (kama ulikuwa serikalini) ilikatika ukiwa 65. Kama ni biashara bado unaisimamia hata kulima
Haya ni kwa wachache waliotunza afya zao vizuri na waliobahatika kutokuwa na magonjwa ya kurithi.

Tena kazi za taaluma kama daktari wa wanyama, unaamka asubuhi unaitwa kwa Mzee Heri ng’ombe ana matatizo. Ukishatoa ushauri unarudi nyumbani na 20,000.
 
Hivi kwanini imekuwa ikisemwa kuwa “life starts at 40”. Je hii ina ukweli? Kama jibu ni ndiyo, Je ni kwa kiasi gani? Au ni mitazamo ya watu tu?
 
Sky Eclat,
In fact at any age, kila mtu ni survivor maana at birth ni wengi lakini kumaliza uinfansi wengi washapuputika. Kumbuka ulioanza nao darasa la kwanza au kumaliza degree yako ya kwanza walobaki ni wachache.

Unachozungumza ni sahihi kuwa waliotunza miili yao pamoja na bahati maana wakati huu ajali ni nyingi sana kama ile ndege ya Ethiopian Airlines.

Siku njema.
 
Hivi kwanini imekuwa ikisemwa kuwa

“life start at 40”

Je hii inaukweli?

Kama jibu ni ndiyo Je ni kwa kiasi gani?

Au ni mitazamo ya watu tu?
Huu ni usemi wa wazungu. Ukifika miaka 40 unakuwa na uzoefu wa maisha unaokusaidia kufika 50, 60, 70, 80 hata 90 kirahisi.

Kama ulianza biashara ukiwa 25, ukiwa 40 umeshakumbana na misukosuko mingi.

Kama uliajiriwa ukiwa 25. 40 si ajabu ni supervisor au meneja.

Kama ni mkulima hata miti ya miaka kumi utakuwa unavuna.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom