Tofauti ya Radio Tumaini na Radio Maria

Wakarismatiki wanatakiwa wafundishe ukatoliki hasa. Sio kuiga Mambo ya walokole. Walokole wajifunze kwa wakatoliki sio kinyume chake. Wakarismatiki wameelewa vibaya ukarismatiki. HAKUNA askofu timamu atawaruhusu kirahisi mpaka wabadilike. Au wajitenge wafungue kanisa lap maana hawaelewi wao Ni nani
Napendekeza vipindi vya usiku wapewe Wakaristimatiki jimbo kuu la Dar badala ya kupiga muziki mfululizo. Hii itavuna wasikilizaji wengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Kwanza napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Radio Tumaini kwa kuelekea kutimiza miaka 25 toka radio ianzishwe. Wamefanya kazi nzuri sana kipindi chote hiki. Lengo la uzi huu si kubomoa bali kujenga kwa radio hizi mbili kubwa za Kikatoliki Tanzania.

Binafsi nimekuwa msikilizaji wa Radio Tumaini muda mrefu na imenisaidia mengi sana kuijua vizuri imani. Lakini miaka ya karibuni niliona nguvu ya Radio Maria kupitia mitandao ya kijamii na kuanza kufuatilia mitandao yao ikiwemo Youtube channel.

Baada ya kuwa mfuatiliaji wa Radio Maria mitandaoni nikaamua kuanza kuwasikiliza kila ninapopata fursa. Yafuatayo ni matokeo ya uchunguzi wangu kwa ufupi.

Radio Maria wana kitengo imara na bora sana kinachoendesha mitandao yao ya kijamii pengine kuliko hata baadhi ya commercial radio stations kwa ushawishi.

Mitandaoni wanaweka nukuu na habari ambazo hata kwa Wakristo wasio Wakatoliki zinawavutia hasa nukuu za maombi na kutia moyo kiimani. Lakini ukisikiliza radio yenyewe huoni ule moto unaowaka mitandaoni.

Radio Tumaini ni dhaifu mno kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii na wana follows wachache mno na hata kupost hawapost chochote! Lakini inabakia kuwa radio bora kabisa katika kuinjilisha. Kuna vipindi vingi vya kuchambua neno la Mungu na imani Katoliki.

Radio Tumaini ina vipindi ambavyo hata wasio Wakatoliki wanaweza kusikiliza na kueleweshwa mambo mengi ya imani. Radio Maria pamoja na kuwa radio ya dini kwa asilimia zote tofauti na Tumaini lakini wanahitaji maboresho makubwa ya vipindi vyao na kutoa fursa ya kutosha ya mafundisho.

Kwa mfano fungua Radio Tumaini kuanzia alfajiri na kesho yake ufungue Radio Maria uone tofauti kuanzia maombi hadi mafundisho. Ingawa malengo ya Radio yanaweza kuwa tofauti lakini malengo yote mwisho wake ni injili ya Kristo kuhubiriwa.

Viongozi wa Radio hizi mbili kama wangekutana na kubadilishana uzoefu wangejiboresha sana maana kila moja ina ubora ambao radio nyingine haina.

Wakristo wa zama zetu tuna upungufu mkubwa wa mafundisho ya kina juu ya imani na ingepaswa radio hizi zijikite huko kwa kiwango kikubwa zaidi kwa kutumia kila rasilimali za Kanisa kufikisha habari njema.

Nyongeza,

Radio Mbiu inakuja vizuri sana. Fatilia Instagram page yao utakubaliana na mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, naona wamekusikia. Tokea tarehe 1 mwezi huu Radio Maria Tanzania imefanya mabadiliko ya vipindi na muda. Wameondoa kabisa sala ya Rosari Takatifu kwa lugha ya Kilatini ambayo tulikuwa tunasali saa kumi na nusu alfajiri na saa sita kamili usiku, vilevile sisikii wakijiunga na Rwanda radio Kabeho (kama nipo sahihi) kwa sala hiyohiyo kwa lugha ya Kiingereza. Ufupi sasa Radio Maria Tanzania imekuwa ya Kibongobongo kwelikweli.
Nimevunjika moyo mno hata kuendelea kuichangia moyo unasita.
=PATER DE CAELIS, DEUS, MISERERE NOBIS=.
 
Upo sahihi radio tumaini wapo deep katika mafundisho kuhusu dini,wanaijua liturgia vizuri sana na hata nyimbo wanazopiga usiku huwa n nzuri pia.
Radio Maria wanajitahidi nao na uzuri watu wanahamasika kuwachangia kwa sababu vpnd vyao vyote ni vya dini na pia waumini wana imani nao kubwa ndo maana wanahamasika kuwachangia michango kila uchwao
Ombi langu kitengo cha habari pale TEC ilitakiwa watake responsibility ya wakujengea uwezo watangazaji na pia kuboresha maudhui katika hizo radio za kanisa.
 
Wakuu,

Kwanza napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Radio Tumaini kwa kuelekea kutimiza miaka 25 toka radio ianzishwe. Wamefanya kazi nzuri sana kipindi chote hiki. Lengo la uzi huu si kubomoa bali kujenga kwa radio hizi mbili kubwa za Kikatoliki Tanzania.

Binafsi nimekuwa msikilizaji wa Radio Tumaini muda mrefu na imenisaidia mengi sana kuijua vizuri imani. Lakini miaka ya karibuni niliona nguvu ya Radio Maria kupitia mitandao ya kijamii na kuanza kufuatilia mitandao yao ikiwemo Youtube channel.

Baada ya kuwa mfuatiliaji wa Radio Maria mitandaoni nikaamua kuanza kuwasikiliza kila ninapopata fursa. Yafuatayo ni matokeo ya uchunguzi wangu kwa ufupi.

Radio Maria wana kitengo imara na bora sana kinachoendesha mitandao yao ya kijamii pengine kuliko hata baadhi ya commercial radio stations kwa ushawishi.

Mitandaoni wanaweka nukuu na habari ambazo hata kwa Wakristo wasio Wakatoliki zinawavutia hasa nukuu za maombi na kutia moyo kiimani. Lakini ukisikiliza radio yenyewe huoni ule moto unaowaka mitandaoni.

Radio Tumaini ni dhaifu mno kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii na wana follows wachache mno na hata kupost hawapost chochote! Lakini inabakia kuwa radio bora kabisa katika kuinjilisha. Kuna vipindi vingi vya kuchambua neno la Mungu na imani Katoliki.

Radio Tumaini ina vipindi ambavyo hata wasio Wakatoliki wanaweza kusikiliza na kueleweshwa mambo mengi ya imani. Radio Maria pamoja na kuwa radio ya dini kwa asilimia zote tofauti na Tumaini lakini wanahitaji maboresho makubwa ya vipindi vyao na kutoa fursa ya kutosha ya mafundisho.

Kwa mfano fungua Radio Tumaini kuanzia alfajiri na kesho yake ufungue Radio Maria uone tofauti kuanzia maombi hadi mafundisho. Ingawa malengo ya Radio yanaweza kuwa tofauti lakini malengo yote mwisho wake ni injili ya Kristo kuhubiriwa.

Viongozi wa Radio hizi mbili kama wangekutana na kubadilishana uzoefu wangejiboresha sana maana kila moja ina ubora ambao radio nyingine haina.

Wakristo wa zama zetu tuna upungufu mkubwa wa mafundisho ya kina juu ya imani na ingepaswa radio hizi zijikite huko kwa kiwango kikubwa zaidi kwa kutumia kila rasilimali za Kanisa kufikisha habari njema.

Nyongeza,

Radio Mbiu inakuja vizuri sana. Fatilia Instagram page yao utakubaliana na mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna moja hapo inapiga sana miziki ya ndomboro ya solo
 
Hao ni tumaini radio.
Ndo maana radio maria inapendwa sana kwa sababu wao vipindi vyao vyote ni vya dini,isipokuwa sa mbili usiku tu ndo huwa wanajiunga na TBC.
Pia hawashabikii siasa hilo nalo linafanya izidi kukubalika zaidi.
 
Ni kweli Radio Maria imekaa kiimani zaidi ila wanatakiwa kuwa makini na ndimi zao, kuna mhubiri wao mmoja anaitwa Titus Hamidu nadhani yupo Mwanza kama sijakosea SAUT alisema waprotestant ni wahuni walibadili maana ya toba na kuichanganya na msamaha kihuni kihuni akirejea vitabu vitakatifu Yoh. 20: 22-23 na Math. 18:35
 
Ni kweli kwa hayo unayoyasema ana udhaifu katika hilo pia amekuwa n mpinzani mkubwa wa kundi linaitwa karismariki ndani ya kanisa katoliki.
N mitazamo yake yeye kama yeye na hatumwi na kanisa katoliki kuhubiri mambo hasi kuhusu madhehebu mengine.
 
Anakwaza na kulipaka matope dhehebu la RC ambalo kimsingi mafundiso yake ni mazuri
 
Sikiliza kuanzia masifu asubuhi, maombi, uchambuzi wa neno n.k yaani hadi unaamka wamekuandaa kiroho kuianza siku. Usiku pia kuna mafundisho mbalimbali ya kiroho hadi saa sita (sometimes wahubiri wa Karistimatiki wanakuwepo) alafu Muziki mtakatifu safi kabisa hadi asubuhi. Mpangilio mzuri sana wanao radio Tumaini ila kwenye social media ni kama hawapo na hawataki kubadilika.
Upo sahihi radio tumaini wapo deep katika mafundisho kuhusu dini,wanaijua liturgia vizuri sana na hata nyimbo wanazopiga usiku huwa n nzuri pia.
Radio Maria wanajitahidi nao na uzuri watu wanahamasika kuwachangia kwa sababu vpnd vyao vyote ni vya dini na pia waumini wana imani nao kubwa ndo maana wanahamasika kuwachangia michango kila uchwao
Ombi langu kitengo cha habari pale TEC ilitakiwa watake responsibility ya wakujengea uwezo watangazaji na pia kuboresha maudhui katika hizo radio za kanisa.
 
Wakarismatiki wanatakiwa wafundishe ukatoliki hasa. Sio kuiga Mambo ya walokole. Walokole wajifunze kwa wakatoliki sio kinyume chake. Wakarismatiki wameelewa vibaya ukarismatiki. HAKUNA askofu timamu atawaruhusu kirahisi mpaka wabadilike. Au wajitenge wafungue kanisa lap maana hawaelewi wao Ni nani
Sawia mkuu. Pale Mabibo RC wanajenga Kanisa ila pembeni yake pana kajisehemu sasa ukipita utasikia makelele tu kwenda mbele. Mara ya mwanzo nilidhani ni Walokole ila nikaambiwa ni RC hao. Nilichefuka nyongo.
 
Anakwaza na kulipaka matope dhehebu la RC ambalo kimsingi mafundiso yake ni mazuri
Kimsingi RC lugha rasmi ni Kilatini lakini hapa kwetu wanene hawataki sie waamini tuielewe na wanatukazania Kiinglishi tu kama Wadosi. Radio Maria ilikuwa na sala ya Rozali Takatifu ya Bikira Maria kwa Kilatini saa sita usiku na kumi na nusu alfajiri. Wamefuta na kuweka saa tisa usiku kana kwamba ni wanga vile. Inakera.
 
Parokia gani kuna misa ya kilatini?
 
Kimsingi RC lugha rasmi ni Kilatini lakini hapa kwetu wanene hawataki sie waamini tuielewe na wanatukazania Kiinglishi tu kama Wadosi. Radio Maria ilikuwa na sala ya Rozali Takatifu ya Bikira Maria kwa Kilatini saa sita usiku na kumi na nusu alfajiri. Wamefuta na kuweka saa tisa usiku kana kwamba ni wanga vile. Inakera.

Wameanza kuwa walugaluga

20.12.2020 nikwa nashuka kwenye bus Morogoro saa 1:07 asubuhi nilimsikia mhubiri mmoja kwenye stesheni ya 93.10 akisema Lazaro alipokuwa akiumwa, ndugu zake walimtumia ujumbe Yesu kwa simu wakimuomba afike na kumponya, lakini Yesu hakwenda mpaka Lazaro alipokufa na kukaa ziku 4 kaburini akaenda kumfufua
 
Mpaka sasa Radio Tumaini ni bora kwa mbali mno vs Radio Maria na nimefurahi pia Radio Tumaini rasmi kuwapa Wakaristimatiki kipindi, hawa walei wapewe vipindi zaidi wako vizuri kwenda na joto la sasa chini ya muongozo wa Kanisa! Ila upande wa social media sijui kwanini wameshindwa kujifunza kwa Radio Maria! Huko Mitandaoni Radio Maria inatisha sana sana!!
 
Back
Top Bottom