TOFAUTI YA ORDINRY BUS, SEMI LUXURY NA LUXURY BUS kwa hapa TZ

Loy MX

JF-Expert Member
Mar 26, 2012
1,253
312
Nimepitia thread moja ya mdau hapa JF ikieleza namna nauli za SUMATRA zilivyopangwa kifupi kwa hapa bongo sijajua kampuni gani ni Ordinary na nyingine ni Luxury au Semi luxury... Au mabasi gani ni Ordinary, Semi Luxury an Luxury.. Kwa mdau yoyote anaeweza kufafanua hili jambo msaada tafadhali sababu naona dalili ya kuibiwa pale ubungo nikimaanisha unaweza lipia Semi Luxury au Luxury na ukakuta Mvua ikinyesha Basi linavuja...
Natanguliza shukrani wadau
 
Tofauti ni kuwa moja limeandikwa SUPER FEO LUXURY BUS na lingine OSAKA BUS SERVICE, masuala mengine kuhusu maana ya luxury bus, kuvuja, nk. utayakuta kwa wapiga debe!!! Satr. Ila kiukweli hizo classess hazitambuliwi mara nyingi operators wanatoza nauli ya kiwango cha juu.
 
Ordinary ni yenye siti 2 upande mmoja na 3 upande mwingine. Semi luxury yenye siti 2 kila upande na AC. Luxury ni siti 2 kwa 2, AC na Choo ndani. Ni mtazamo wangu tu inaweza ikawa sio kweli. Nimejaribu kubahatisha. Wanaojua watatoa ufafanuzi zaidi.
 
nashindwa kuielewa hii nchi.
 
Ordinary ni yenye siti 2 upande mmoja na 3 upande mwingine. Semi luxury yenye siti 2 kila upande na AC. Luxury ni siti 2 kwa 2, AC na Choo ndani. Ni mtazamo wangu tu inaweza ikawa sio kweli. Nimejaribu kubahatisha. Wanaojua watatoa ufafanuzi zaidi.

Hapo mkuu si itakuwa kila nikiona 2x3 nijue ni ordinary?? sasa hawa SUMATRA kwa nini wasingetoa hizo kampuni na ili wananchi tujue?
 
Hapo mkuu si itakuwa kila nikiona 2x3 nijue ni ordinary?? sasa hawa SUMATRA kwa nini wasingetoa hizo kampuni na ili wananchi tujue?

Kampuni nyingine zina mabasi mchanganyiko yaani luxury na ordinary kama vile Simba mtoto na Raha Leo ya kwenda Tanga.
 
Kwa hapa bongo land mie naona luxury na ordinary zinatofautishwa kwa ugawaji wa pipi, vibiskuti na soda.Sasa ukiona umesafiri from mby to Dar hata ubuyu hujapewa jua umepanda O bus.Ni mtazamo tu
 
Ordinary ni yenye siti 2 upande mmoja na 3 upande mwingine. Semi luxury yenye siti 2 kila upande na AC. Luxury ni siti 2 kwa 2, AC na Choo ndani. Ni mtazamo wangu tu inaweza ikawa sio kweli. Nimejaribu kubahatisha. Wanaojua watatoa ufafanuzi zaidi.

Kinadharia hii ndio sahihi...
 
Shambalai, champion, super najimunisa ni mfano wa ordinary buses
 
Shabiby, Abood, Hood, Wifi nae, Green Star, Raha leo, Satellite ni semi luxury buses
 
Ratco, Dar Express, New Force, Shabiby sharobalo, Ndenjela, JM, Super Feo ni Luxury buses
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza, hawa SUMATRA kwa nini wasitoe kabisa criteria za kuchagua hizo category3? Ili nijue what to expect, for predicatabilityu ni muhimu kwenye any regulation otherwise inacreate a lot of uncertainties.

Mara kibao unaambiwa basi ni luxury mvua zikinyesha linavuja, au hakuna AC ni mwendo wa kupigwa jua na upepo mtindo mmoja, hakuna Tv screen au hata redio ndani basi vurugu mtindo mmoja na huku umelipa nauli ya juu?

Kama walivoaisnisha nauli, inabidi na hapo waseme basi la kawaida, nusu luxury na full luxury yanatofautishwaje?
 
Sumry zote, Upendo zote, Alsaedy zote, Tashriff zote, master city zote, Bembea zote, Sai baba zote, ni Ordinary buses
 
Kibongobongo full luxury bado sana! Kuna baadhi wanajitahidi ila hawajafikia bado!
 
Ordinary bus ni sawa na kajamba nani unapanda na kuku mbuzi jiko la mkaa masufuria maana hauna uhakika wa safari mtafika lini pia usisahau na mashuka dawa za mmbu, mende na kunguni na pia sia ajabu ukakuta siti moja mmekatiwa watu wanne so mnapangiana zamu za kukaa kwa masaa hadi mwisho wa safari mwendo kwa magari haya haujulikani kwakuwa hayana speedoometer na luxury ni kuwa unakaa kiti cha peke yako unapata huduma zote utakazo ikiwemo choo bafu maliwato kwa ujumla pia kuna chakula bia na pombe kali kuna smoking zone kuna ofisi pia kuna secretary na unaweza kusimamisha bus ukashuka ukaingia dukani mahala popote na zaidi unafikishwa hadi mlangoni kwako mwisho wa safari mwendo wa gari hili ni 50 km/h
 
Back
Top Bottom